Mnaotaka nafasi za ubunge kupitia CHADEMA mmeisoma hii?

Mnaotaka nafasi za ubunge kupitia CHADEMA mmeisoma hii?

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza mfumo mpya wa kuwapata wagombea nafasi ya ubunge kuanzia uchaguzi wa 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa alisema kuwa kuanzia uchanguzi ujao wa 2015, nafasi za wagombea ubunge majimbo yote nchini zitatangazwa kwenye magazeti.

Dk. Slaa alisema baada ya waombaji kujitokeza watafanyiwa usaili kwa kufanya mtihani utakaokuwa umeandaliwa kwa kuzingatia nafasi hizo.

“Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe amekwisha kusema kwamba kuanzia sasa hatupokei makapi kutoka Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na hili naliweka wazi kwamba uchaguzi ujao utakuwa na mfumo mpya na wenye mabadiliko makubwa, tunaamini utaleta uzalendo na kuondoa upuuzi unaojitokeza.

“Kwa wale walio na mipango ya kujitokeza dakika za mwisho kugombea nafasi za ubunge kupitia Chadema au nje ya chama, naomba wasahau hilo tunataka mtu anayetetea wananchi, mwenye uzalendo, hoja, ujasiri na mwenye kuitoa Tanzania hapa ilipo na kuisogeza mbele,”alisema.

Akizungumzia suala la mchakato wa katiba mpya alisema Chadema haitakubali kuona inakuwa sehemu ya watu walioshiriki kutengeneza katiba isiyo ya Watanzania wote.

Kuandika barua za maombi siyo kasoro, kasoro iko kwenye Bodi inayopokea maombi, kuyachambua na kuyaweka kwenye kikao. Barua zisizo za Wachaga nyingi sana zitapotea na waombaji watakaoshiriki mchakato watatokana na wale tu wenye sifa ya kupitiana Dubai. Wengine mtaambia maombi yenu hayakufanikiwa. Of course kutakuwemo na vibaraka wa kupaka rangi kama akina John Shibuda walivyokuwa wakitumiwa na CCM ya Mwinyi, baadaye wakajichunguza na kuhamia CHADEMA.

Mfumo huu uliingizwa Serikalini na Mama yetu Mary Nagu hata UHeadmaster ukawa wa kufanyiwa usaili, Malengo ni hayo hayo ya kuajili wachaga wengi iwezekanavyo kwa njia HALALI. Wakati huo nafasi zote za kuchambua maombi UTUMISHI zilikuwa TAYARI mikononi mwa Wachaga. Wanyamwezi wote akina Nkonde walipita kwenye vikao bila kujua kuwa MaHeadmster walikuwa tayari wanajulikana kabla hata ya kuingia katika ukumbi wa kuhojiwa.

Kalagi baho, mtakaa kama watazamaji wakati mikakati ya kuandalia taifa la wachaga inafanywa waziwazi na KAMA HALALI KABISA KUMBE........
 
Bravo Chadema. CCM nao waige waache kupeana kwa upendeleo.
Ningeshauri Chadema utafute timu wa watakaosaili wenye uzoefu na siasa na wasio wanachadema ili kutotoa upendeleo.

Nani aliekuambia kufanya mitihani ndo upendeleo hautokuepo?,watu wanatafuta kazi usaili wa kuongea na kuandika upo lakini kuna upendeleo sembuse kwa hao wanasiasa?...kalagabao
 
Hiki chama kimekuwa Yeboyebo hakiuziki mpaka kijitangaze kwenye Magazeti? Hii imekuwa Tender?
Hapo mwenye nyingi na atakae wahonga mlungula ndo atapita,wakati huo kishinda ni ngumu kwani CCM bado inapendwa nchi nzima.
Kweli mzimu wa Zitto ni kiboko.
Hawa wamechanganyikiwa muda wote wanawaza biashara na faida, hiki chama ni kama kampuni tu.
 
Mmoja Kati Ya Wanaharakati Nguli Wa Chadema Ambaye Atakumbukwa Sana Kwa Harakati Za Kupigania Haki Za Wanafunzi Udsm, Stephen Owawa Amesema Bado Hajaamua Kugombea Ubunge Jimbo La Rorya Mkoani Musoma Na Badala Yake Anaendelea Na Kazi Katika Ofisi Ya mkaguzi mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG mkoa wa kagera.

Owawa amesema ni kweli wananchi na viongozi wa chama ngazi ya wilaya wamekuwa wakimsihi arejee nyumbani na aanze harakati za kuliandaa jimbo ila yeye anabamwa na mkataba wa kazi kwani kwa sasa ni mwajiriwa wa serikali lakini pia amekuwa na kazi nyingi za kufanya.. amesema bado ana upendo wa dhati kwa chadema na yupo tayari kutoa hata material support kwa chama wilaya ili kijijenge zaidi.

Pia amesisitiza kuwa anafahamu kuwa anaweza kwenda rorya na kuhutubia mikutano ya hadhara na kisha akarejea kituo chake cha kazi ila si sahihi kufanya hvyo kwaajili ya kuunyemelea ubunge na zaidi ya yote amesema yupo tayari kugombea ubunge wa rorya au jimbo lolote 2015 iwapo tu wanachadema watakosa mtu wa uhakika.
 
asubiri kwanza mbowe atangaze kwenye magazeti nafasi hiyo,
 
Hivi kufanya mtihani kunakufanya uwe na haiba ya kuchaguliwa na wananchi? Halafu huo mtihani utampimaje mtu kutambua ni mzalendo? Any way ngoja nianze mishe mishe za kuchukua form ili nikagombee nyamagana.

Kwa upeo wako mdogo unaelewa kila mtihani ni hesabu tu.
 
Hizi nguvu anazotumia kama angezitumia kujenga demokrasia ndani ya chama si ingekuwa ni afya zaidi?
 
Watu wengine wanakurupuka tu na kuanza kuropoka humu bila kuelewa hoja na kauli imekaaje.
 
Hapa ndo mi napataga shida sn na siasa za tanzania. Nimejiuliza hivi;
1. Mtihani\usaili huo utaandaliwa na nani!?
2. Kuna tofauti gani baina ya usaili huo na ule uliofanywa na ccm 2010 ambao ulipelekea ccm kupoteza majimbo ambayo ndo cdm wanamiliki kwa ss!?
3. Kutakuwa na uwazi kiasi gani ktk usaili huo!?
4. Mbona wengi wa viongozi, wabunge na madiwani wa cdm ndo makapi ya ccm? Watafukuzwa?
5. Hawatapokea mwanachama mpya kutoka ccm kwakuwa ni kapi? ilhali wenzao walipokelewa tena kwa mbwembwe kubwa?
6. Je! hayo ni mawazo ya m.kiti au ya chama!?

ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI
 
Nauo mtihani wenyewe utavujishwa tuu maana hawa wenzetu wa ksk hawata weza kuona wanamwacha mwenzao!
 
Watangaze sifa za kuingia kwenye chumba cha mtihani mapema maana nalitaka sana jimbo la mbowe!
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza mfumo mpya wa kuwapata wagombea nafasi ya ubunge kuanzia uchaguzi wa 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa alisema kuwa kuanzia uchanguzi ujao wa 2015, nafasi za wagombea ubunge majimbo yote nchini zitatangazwa kwenye magazeti.

Dk. Slaa alisema baada ya waombaji kujitokeza watafanyiwa usaili kwa kufanya mtihani utakaokuwa umeandaliwa kwa kuzingatia nafasi hizo.

“Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe amekwisha kusema kwamba kuanzia sasa hatupokei makapi kutoka Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na hili naliweka wazi kwamba uchaguzi ujao utakuwa na mfumo mpya na wenye mabadiliko makubwa, tunaamini utaleta uzalendo na kuondoa upuuzi unaojitokeza.

“Kwa wale walio na mipango ya kujitokeza dakika za mwisho kugombea nafasi za ubunge kupitia Chadema au nje ya chama, naomba wasahau hilo tunataka mtu anayetetea wananchi, mwenye uzalendo, hoja, ujasiri na mwenye kuitoa Tanzania hapa ilipo na kuisogeza mbele,”alisema.

Akizungumzia suala la mchakato wa katiba mpya alisema Chadema haitakubali kuona inakuwa sehemu ya watu walioshiriki kutengeneza katiba isiyo ya Watanzania wote.
Hv jimbo la Bunda c liko wazi muda wote wa Wassira au nakosea? Naomba mniunge mkono nikagombee kule jamani! Mm ni mzawa kabisa na mzalendo wa kweli acha huyo mzee wa kuchapa usingizi bungeni a.k.a Tumbotumbo.
Napita tu mm mwenyewe mgeni nahurumia kucha na meno yangu jamani.
 
sasa huyu bogus nani atampigia kura? kwanza ana njaa tu,mchumia tumbo sio mwanaharakati
 
Katiba haimruhusu mtumishi wa serikali kuhutubia mkutano wa hadhara wa chama cha siasa, tena cha upinzani.

Owawa kama vipi tupa makabrasha kule nenda kawakomboe wana rorya
 
Katika mtihani huo ni vizuri maswali ya bongo fleva na hip hop yakawemo maana watahiniwa wengi safari hii watatokea huko.
 
Kinajiita Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

*Demokrasia ina maana Chama husika kutoa fursa kwa Wanachama kuchagua na kuchaguliwa.
*Demokrasia ina maana watu wawe na uhuru wa kutoa maoni na kusikilizwa.
*Demokrasia ina maana kuwepo na uwazi wa kutosha juu ya shughuli za uendeshaji Chama.
*Demokrasia inahimiza uvumilivu miongoni mwa Wanachama.
*Demokrasia inahimiza falsa ya wengi wape hata Viongozi wa Chadema hupenda pia kutumia falsa ifananayo na hiyo ya 'Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu'.
*Demokrasia ni nzuri kwakuwa huboresha mitizamo na misimamo ya Chama husika,Huzuia uwezekano wa kuwepo Watawala madikteta,Huwapa nafasi Watu ya kuondokana na Viongozi wasiowataka kupitia term limits,Hutoa fursa kwa watu kutoka katika matabaka yote ya kimaisha kutimiza ndoto zao za kimafanikio ziwe za kisiasa au za kiuchumi since democracy equals to free people as well free market.

Sasa ebu tujaribu kujiuliza kwa tabia hizi zinazoonyeshwa na hawa Viongozi wa Chadema Je ni kweli wao ni Waumini wa Demokrasia?Kweli?
 
Back
Top Bottom