Mnaotaka nafasi za ubunge kupitia CHADEMA mmeisoma hii?

Ni sahihi, kwani hii inaweza kuondoa kupitishana kiupambe, lakini atakaesahihisha huo mtihani ni nani? na nani atakaethibitisha kuwa waombaji waliokosa kwa kigezo cha mtihani wametendewa haki na si mizengwe kufanyika?
 
Mamluki ya mizigo itakuja na porojo zao mda si mrefu. Nadhani hiyo itakuwa ni hatua njema na pia ingekuwa bora kabla ya kutangazwa rasmi kugombea wakatangazwa kwenye magazeti ili kama kasoro zitakazo jitokeza iwe rahisi kumbadilisha

Mbona hujiamini shangazi??? JF ipo kwa watu kuchangia mawazo yao tofauti
 
Chadema mna mbwembwe sasa mtu kama Afande Sele,Sugu,Lema na Profesa Jay nani atawafanyia hiyo mitihani ili wafaulu na kugombea ubunge??? Chama cha kilaghai porojo hazi ishi
 
“Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe amekwisha kusema kwamba kuanzia sasa hatupokei makapi kutoka Chama Cha
Mapinduzi (CCM)

mbona hata slaa na wengine ni makapi? toka ccm angeshinda uchaguzi kura za maoni 1995 kule ndani ya ccm asingehamia chadema kwa kuwa wao wameingia wanafunga milango waliotangulia wangifunga milango wao wangeingia
 
@Dr.Slaa mngeweka time limit ya mtu tangu kuiunga na chama na kisha aruhusiwe kugombea uongozi kupitia CHADEMA.Mimi ningependekeza kipengele kuwa mtu yoyote anaejiunga na chama mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wowote asiruhusiwe kushirki katika uchaguzi huo.Uwe uchaguzi mkuu au uchaguzi mdogo.

Tukifanya hivi tutaepuka kupata watu kama kina Shibuda wanaohamia CHADEMA kimwili wakati kiroho bado wako CCM.

Naunga mkono mabadiliko haya kwani yamezingatia siasa za wakati wa sasa.Najua hata Dr.Slaa alihamia CHADEMA baada ya kufanyiwa mizengwe CCM lakini naamini mabadiliko haya ni kutokana mahitaji ya wakati.
 
Chadema mna mbwembwe sasa mtu kama Afande Sele,Sugu,Lema na Profesa Jay nani atawafanyia hiyo mitihani ili wafaulu na kugombea ubunge??? Chama cha kilaghai porojo hazi ishi

hii haisahihishwi na necta bali na mbowe ana foam six olginal hata kama wewe ni profesa utafanya mtihani tu asahihishe yeye .,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
Ni sahihi, kwani hii inaweza kuondoa kupitishana kiupambe, lakini atakaesahihisha huo mtihani ni nani? na nani atakaethibitisha kuwa waombaji waliokosa kwa kigezo cha mtihani wametendewa haki na si mizengwe kufanyika?

Nasikia Mbowe ndiye atakayesahihisha pepa!!!
 
"Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe amekwisha kusema kwamba kuanzia sasa hatupokei makapi kutoka Chama Cha
Mapinduzi (CCM)

mbona hata slaa na wengine ni makapi? toka ccm angeshinda uchaguzi kura za maoni 1995 kule ndani ya ccm asingehamia chadema kwa kuwa wao wameingia wanafunga milango waliotangulia wangifunga milango wao wangeingia

Hivi wewe unajua maana ya neno Kuanzia sasa???
Usiwe mgumu wa kuelewa na mwepesi wa kusahau, kutokana na Sera mbovu na Katiba isiyokidhi mahtaji iliibidi watu wazima wengi waanzie CCM.
 
Hivi kweli ni maswali ya aina gani yatawezwa kujibiwa na watu kama Godbless J Lema?

Bila shaka kuna watu watakuwa wanapewa mitihani yao.

Na kama ni kweli kutakuwa na mitihani na kwa tabia ya chadema kuvujisha siri za chama na sitashangaa mitihani kuvuja.

Hivi kweli chadema mnaiamini ofisi ya dr slaa kwa kutunza mitihani?

Kwa utaratibu huu wa mitihani kuna watu pasi shaka hawawezi kufaulu bila kuiba mitihani.

My brother you have let me down (wankeyesa) if at all your name symbolizes where we originate. Tunachopaswa kuangalia na kutolea thathmini ni validity and reliability of CDM approach maana hakuna popote imesmwa Dr.Slaa ndiye atakuwa composer and custodian wa vetting test/exam.

Pili kutumia muda mnaongelea personalities ni too low. Twende mbali zaidi tujadili process (mchakato) CDM wameanzisha. Inabidi tukosoe utaratibu huu kama tunaona haufai na kama tunaona hautatuletea matunda tunayotarajia maana mbunge akipita anakuwa ni wa wote.

Mimi naona mtihani ni mzuri sana na ujikite katika mambo yanayomhusu mwanachi wa kawaida in relationship to social, economic and political changes/ reforms katika nchi yetu. Uelewa wa hitikadi ya CDM na jinsi ya kuhtafsiri kivitendo ili kumsaidia mwaanchi wa kawaida who has purposely been left outside the basket by architects of current politics
 
Mzalendo siku zote hawezi kujenga majengo ya kifahari USA, DUBAI NA SOUTH AFRIKA akaacha nyumbani. Kwa nini Mbowe kama ni muumini mzuri wa uzalendo aache kujenga hizo nyumba hapa nyumbani nabadala yake akazijenga nchi za nje? tena nchi 3 tofauti. Hakuna uzalendo hapo ni njia za kuzidi kuwatapeli watu.

Unamaanisha ujenga nyumba nyumbani ndicho kipimo cha uzalendo? wafanyabiashara wasiwekeze nchi nyingine kisa hawatakuwa wazalendo? dunia nzima watu wanakaribishwa kuwekeza wewe unaona sio uzalendo? kwa hiyo hata OBAMA kuja nchini na wafanyabiashara toka USA naye sio mzalendo kwa kuwatafutia fursa huku bongo badala ya kuwashauri wabaki kwao na wawekeze nyumbani? UNASUMBULIWA NA USHABIKI MANDAZI!
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza mfumo mpya wa kuwapata wagombea nafasi ya ubunge kuanzia uchaguzi wa 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa alisema kuwa kuanzia uchanguzi ujao wa 2015, nafasi za wagombea ubunge majimbo yote nchini zitatangazwa kwenye magazeti.

Dk. Slaa alisema baada ya waombaji kujitokeza watafanyiwa usaili kwa kufanya mtihani utakaokuwa umeandaliwa kwa kuzingatia nafasi hizo.

“Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe amekwisha kusema kwamba kuanzia sasa hatupokei makapi kutoka Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na hili naliweka wazi kwamba uchaguzi ujao utakuwa na mfumo mpya na wenye mabadiliko makubwa, tunaamini utaleta uzalendo na kuondoa upuuzi unaojitokeza.

“Kwa wale walio na mipango ya kujitokeza dakika za mwisho kugombea nafasi za ubunge kupitia Chadema au nje ya chama, naomba wasahau hilo tunataka mtu anayetetea wananchi, mwenye uzalendo, hoja, ujasiri na mwenye kuitoa Tanzania hapa ilipo na kuisogeza mbele,”alisema.

Akizungumzia suala la mchakato wa katiba mpya alisema Chadema haitakubali kuona inakuwa sehemu ya watu walioshiriki kutengeneza katiba isiyo ya Watanzania wote.

kwa namna hii mamluki watakosa nafasi CHADEMA. safi sana.
 
Kuandika barua za maombi siyo kasoro, kasoro iko kwenye Bodi inayopokea maombi, kuyachambua na kuyaweka kwenye kikao. Barua zisizo za Wachaga nyingi sana zitapotea na waombaji watakaoshiriki mchakato watatokana na wale tu wenye sifa ya kupitiana Dubai. Wengine mtaambia maombi yenu hayakufanikiwa. Of course kutakuwemo na vibaraka wa kupaka rangi kama akina John Shibuda walivyokuwa wakitumiwa na CCM ya Mwinyi, baadaye wakajichunguza na kuhamia CHADEMA.

Mfumo huu uliingizwa Serikalini na Mama yetu Mary Nagu hata UHeadmaster ukawa wa kufanyiwa usaili, Malengo ni hayo hayo ya kuajili wachaga wengi iwezekanavyo kwa njia HALALI. Wakati huo nafasi zote za kuchambua maombi UTUMISHI zilikuwa TAYARI mikononi mwa Wachaga. Wanyamwezi wote akina Nkonde walipita kwenye vikao bila kujua kuwa MaHeadmster walikuwa tayari wanajulikana kabla hata ya kuingia katika ukumbi wa kuhojiwa.

Kalagi baho, mtakaa kama watazamaji wakati mikakati ya kuandalia taifa la wachaga inafanywa waziwazi na KAMA HALALI KABISA KUMBE........

Ndugu yangu kama kweli Tanzania ya leo tuna watu mnaoongelea ukabila kwa kuwaleng watu fulani mjue tuna muda mrefu wa kupiga maendeleo kiuchumi na kifikra. Na bahati nzuri watu unaowapa jina baya nawasifu maana walipotambua mnawabagua wakawekeza katika elimu na uchumi. Wakati mnaangaika na shule kila kata wao washapita huko zamani maana wao wanaongelea sekondari 4 na zaidi kwa kila kata. Wako too strategic maana wanasoma focusing on the industry from which they can be employed or self employed and extract cream. Wenzetu wametuzidi hata kama mtawapaka matope. Hamna ukabila kwao bali uwezo. That's the bottomline
 
@Dr.Slaa mngeweka time limit ya mtu tangu kuiunga na chama na kisha aruhusiwe kugombea uongozi kupitia CHADEMA.Mimi ningependekeza kipengele kuwa mtu yoyote anaejiunga na chama mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wowote asiruhusiwe kushirki katika uchaguzi huo.Uwe uchaguzi mkuu au uchaguzi mdogo.

Tukifanya hivi tutaepuka kupata watu kama kina Shibuda wanaohamia CHADEMA kimwili wakati kiroho bado wako CCM.

Naunga mkono mabadiliko haya kwani yamezingatia siasa za wakati wa sasa.Najua hata Dr.Slaa alihamia CHADEMA baada ya kufanyiwa mizengwe CCM lakini naamini mabadiliko haya ni kutokana mahitaji ya wakati.

Salary Slip, very informed input kwa mistari miwili ya kwanza lakini tuwe na reservation kwa mtu aliyefikisha miaka 18 ndani ya mwaka mmoja na kama ameiva kiitikadi na ana upeo kwa siasa za ndani na kimataifa
 
Wakuu na mimi natangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la kigoma kaskazini kwa Zitto.
 
Last edited by a moderator:
nawaonea huruma waliozoea na wanaopenda viti maalum, hivi si vimefutwa katika katiba ijayo inacase itatumika wakat wa uchaguzi? kama tutaendelea kutumia katiba ya zamani wakati wa uchaguzi na wa viti maalaum wataaply kama hao wengine si ndio ehh
 
Ndugu yangu kama kweli Tanzania ya leo tuna watu mnaoongelea ukabila kwa kuwaleng watu fulani mjue tuna muda mrefu wa kupiga maendeleo kiuchumi na kifikra. Na bahati nzuri watu unaowapa jina baya nawasifu maana walipotambua mnawabagua wakawekeza katika elimu na uchumi. Wakati mnaangaika na shule kila kata wao washapita huko zamani maana wao wanaongelea sekondari 4 na zaidi kwa kila kata. Wako too strategic maana wanasoma focusing on the industry from which they can be employed or self employed and extract cream. Wenzetu wametuzidi hata kama mtawapaka matope. Hamna ukabila kwao bali uwezo. That's the bottomline

Hofu ya watu wengi ni juu ya uwezekano wa kuwapata akina Anthony Komu wengine kupitia APPROACH hii mpya.Si mnakumbuka kilichotokea mwaka 2012 katika uchaguzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki ambapo Chadema kiliwachinjia baharini Wagombea wengine wa Ubunge na kumpitisha kinyemela Anthony Komu?Wengine bado tunakumbuka Mkuu!Tunaishi kwa kuona wala sio kusikia.
 
Back
Top Bottom