Mnaotaka nafasi za ubunge kupitia CHADEMA mmeisoma hii?

Mnaotaka nafasi za ubunge kupitia CHADEMA mmeisoma hii?

Mzalendo siku zote hawezi kujenga majengo ya kifahari USA, DUBAI NA SOUTH AFRIKA akaacha nyumbani. Kwa nini Mbowe kama ni muumini mzuri wa uzalendo aache kujenga hizo nyumba hapa nyumbani nabadala yake akazijenga nchi za nje? tena nchi 3 tofauti. Hakuna uzalendo hapo ni njia za kuzidi kuwatapeli watu.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza mfumo mpya wa kuwapata wagombea nafasi ya ubunge kuanzia uchaguzi wa 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa alisema kuwa kuanzia uchanguzi ujao wa 2015, nafasi za wagombea ubunge majimbo yote nchini zitatangazwa kwenye magazeti.

Dk. Slaa alisema baada ya waombaji kujitokeza watafanyiwa usaili kwa kufanya mtihani utakaokuwa umeandaliwa kwa kuzingatia nafasi hizo.

“Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe amekwisha kusema kwamba kuanzia sasa hatupokei makapi kutoka Chama Cha
Mapinduzi (CCM)
na hili naliweka wazi kwamba uchaguzi ujao utakuwa na mfumo mpya na wenye mabadiliko makubwa, tunaamini utaleta uzalendo na kuondoa upuuzi unaojitokeza.

“Kwa wale walio na mipango ya kujitokeza dakika za mwisho kugombea nafasi za ubunge kupitia Chadema au nje ya chama, naomba wasahau hilo tunataka mtu anayetetea wananchi, mwenye uzalendo, hoja, ujasiri na mwenye kuitoa Tanzania hapa ilipo na kuisogeza mbele,”alisema.

Akizungumzia suala la mchakato wa katiba mpya alisema Chadema haitakubali kuona inakuwa sehemu ya watu walioshiriki kutengeneza katiba isiyo ya Watanzania wote.

Binafsi wao ni nini iwapo nao walitoka huko?
 
huu utaratibu ungeanza toka 1994 dr Slaa leo angekuwa mwanaCCM mtiifu na pengine waziri mzigo
 
Mmmh. Hili kweli linawezekana kwa siasa za Tanzania?.

Nahofia Dr. Slaa na washauri wake wasije wakala matapishi yao ya kisiasa.

Kisiasa kuwaita Wanachama waliotoka vyama vingine na kujiunga na CHADEMA ambao kwa sasa ni viongozi ndani ya CHADEMA kwa jina la MAKAPI ni dharau au ni kuidharaulisha CHADEMA kama taasisi. Hii ina maana kuwa baadhi ya nafasi ndani ya CHADEMA zinashikiliwa na MAKAPI ambayo kwa jina jingine ni uchafu (useless).

Kuna viongozi kwa sasa wengi tu wa Msingi, Tawi, Kata/wadi, Wilaya, Mkoa, Jimbo na Taifa ambao wapo ndani ya CHADEMA kutokana na 'kudandia Meli' kwa sababu mbali mbali wakati ikiondoka kuelekea kwenye chaguzi za ndani na nje.

Siyo wote wanaotoka vyama vingine na kujiunga na CHADEMA ni MAKAPI na pia siyo wote ambao wako CHADEMA na hawakuwahi kujiunga na chama kingine zaidi ya CHADEMA wanaweza wakawa siyo MAKAPI.

Hizi rhetoric inawezekana hapa zisiisaidie CHADEMA huko mbele ya safari ya kisiasa kwa sababu zinawagawa viongozi waliopo kwa sasa katika makundi.
 
Demokrasia bai bai Chadema.Najua hiki ni kitanzi kwaajili ya wale wote wasio upande wa Mbowe.Waweza ukafaulu mtihani huu vizuri sana lakini kwakuwa wewe sio mfuasi wa Mheshimiwa utafelishwa tu na wale wafuasi wa Mbowe watafaulishwa tu hata kama watafeli hiyo mitihani.Sadly but true!!
 
Mamluki ya mizigo itakuja na porojo zao mda si mrefu. Nadhani hiyo itakuwa ni hatua njema na pia ingekuwa bora kabla ya kutangazwa rasmi kugombea wakatangazwa kwenye magazeti ili kama kasoro zitakazo jitokeza iwe rahisi kumbadilisha

aliyewaroga ashakufa chochote atakachosema babu yenu hakuna kubisha akisema mnywe gongo twende kaz yaan mmeshakuwa mandondocha.
 
Mmmh. Hili kweli linawezekana kwa siasa za Tanzania?.

Nahofia Dr. Slaa na washauri wake wasije wakala matapishi yao ya kisiasa.

Kisiasa kuwaita Wanachama waliotoka vyama vingine na kujiunga na CHADEMA ambao kwa sasa ni viongozi ndani ya CHADEMA kwa jina la MAKAPI ni dharau au ni kuidharaulisha CHADEMA kama taasisi. Hii ina maana kuwa baadhi ya nafasi ndani ya CHADEMA zinashikiliwa na MAKAPI ambayo kwa jina jingine ni uchafu (useless).

Kuna viongozi kwa sasa wengi tu wa Msingi, Tawi, Kata/wadi, Wilaya, Mkoa, Jimbo na Taifa ambao wapo ndani ya CHADEMA kutokana na 'kudandia Meli' kwa sababu mbali mbali wakati ikiondoka kuelekea kwenye chaguzi za ndani na nje.

Siyo wote wanaotoka vyama vingine na kujiunga na CHADEMA ni MAKAPI na pia siyo wote ambao wako CHADEMA na hawakuwahi kujiunga na chama kingine zaidi ya CHADEMA wanaweza wakawa siyo MAKAPI.

Hizi rhetoric inawezekana hapa zisiisaidie CHADEMA huko mbele ya safari ya kisiasa kwa sababu zinawagawa viongozi waliopo kwa sasa katika makundi.
Kwa hiyo unataka kusema kuwa Chadema ni chama cha Makapi?
 
hivi wewe kwanini umheshimu kamanda lema ? Kafuta ccm arusha bado tu hukubali ? Utapoteza muda wako kumpinga lema , humuwezi hata kwa kumchangia na marehemu ndugu zako !

mkuu nahofia watu kuchora mazombi kwenye mitihani ya dr slaa na mbowe.
 
Nchimbi aanze kuaga kabisa,
Mimi ndio Chaguo Jipya la Wana-Songea.
 
mmmh. Hili kweli linawezekana kwa siasa za tanzania?.

Nahofia dr. Slaa na washauri wake wasije wakala matapishi yao ya kisiasa.

kisiasa kuwaita wanachama waliotoka vyama vingine na kujiunga na chadema ambao kwa sasa ni viongozi ndani ya chadema kwa jina la makapi ni dharau au ni kuidharaulisha chadema kama taasisi. Hii ina maana kuwa baadhi ya nafasi ndani ya chadema zinashikiliwa na makapi ambayo kwa jina jingine ni uchafu (useless).

kuna viongozi kwa sasa wengi tu wa msingi, tawi, kata/wadi, wilaya, mkoa, jimbo na taifa ambao wapo ndani ya chadema kutokana na 'kudandia meli' kwa sababu mbali mbali wakati ikiondoka kuelekea kwenye chaguzi za ndani na nje.

Siyo wote wanaotoka vyama vingine na kujiunga na chadema ni makapi na pia siyo wote ambao wako chadema na hawakuwahi kujiunga na chama kingine zaidi ya chadema wanaweza wakawa siyo makapi.

Hizi rhetoric inawezekana hapa zisiisaidie chadema huko mbele ya safari ya kisiasa kwa sababu zinawagawa viongozi waliopo kwa sasa katika makundi.

kwakweli Dr.W.Slaa anapenda kutukana wenzie na ana sahau hata yeye kajitukana katika hili.
 
Last edited by a moderator:
kamanda Mungi chukua fomu upige mtihani uchukue nafasi ya lema.kbb
 
Last edited by a moderator:
Mzalendo siku zote hawezi kujenga majengo ya kifahari USA, DUBAI NA SOUTH AFRIKA akaacha nyumbani. Kwa nini Mbowe kama ni muumini mzuri wa uzalendo aache kujenga hizo nyumba hapa nyumbani nabadala yake akazijenga nchi za nje? tena nchi 3 tofauti. Hakuna uzalendo hapo ni njia za kuzidi kuwatapeli watu.

Usiropoke tuu toa picha za nyumba hzo tuzione kama udhibitisho na sii picha tuu toa na nakala za hati ya nyumba hzo tukuamini sio unatuletea story za vijiwen kwenu humu ndan.
 
Kwa hiyo unataka kusema kuwa Chadema ni chama cha Makapi?
Inabidi hilo swali ulielekeze kwa viongozi wakuu wa CHADEMA wanaodai kuwa mwaka 2014/2015 hawatachukua MAKAPI kutoka vyama vingine kwa maana nyingine wanasema kuwa walichukua MAKAPI huko nyuma!.

Ndiyo maana nimehoji kisiasa hii dhana ya kuita wanasiasa wengine MAKAPI wakati kwa sasa ni viongozi ndani ya chama wanachokiongoza wakiwa ni viongozi wakuu.

Mimi sijasema!.
 
kwakweli Dr.W.Slaa anapenda kutukana wenzie na ana sahau hata yeye kajitukana katika hili.
Ndiyo maana hata mimi ninashangaa kuzisikia hizi lugha za dharau kwa viongozi wengine hasa ikichukuliwa kuwa kuna viongozi wachache sana ndani ya CHADEMA ambao hawakuwa wanachama wa vyama vingine kabla ya kujiunga na CHADEMA.

Uongozi makini pia unapimwa kwa kuwa juu ya hizi lugha za dharau zinazojenga matabaka ndani ya vyama.
 
Inabidi hilo swali ulielekeze kwa viongozi wakuu wa CHADEMA wanaodai kuwa mwaka 2014/2015 hawatachukua MAKAPI kutoka vyama vingine kwa maana nyingine wanasema kuwa walichukua MAKAPI huko nyuma!.

Ndiyo maana nimehoji kisiasa hii dhana ya kuita wanasiasa wengine MAKAPI wakati kwa sasa ni viongozi ndani ya chama wanachokiongoza wakiwa ni viongozi wakuu.

Mimi sijasema!.

Acha kupotosha umma ww. Elewa kauli iliyosemwa iko katika wakat gan bana sio kuongea ongea tuu. Kaul iko katika wakat ujao "hatuta chukua makapi" na sio wakat uliopita eti "tulichukua makapi" ukielewa nyakati za kauli husika utaelewa mbowe alikuwa anamaanisha nini na utajenga hoja.
 
Back
Top Bottom