Mnaotaka nafasi za ubunge kupitia CHADEMA mmeisoma hii?

Mbaga Michael

Verified Member
Nov 17, 2011
2,883
1,250
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza mfumo mpya wa kuwapata wagombea nafasi ya ubunge kuanzia uchaguzi wa 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa alisema kuwa kuanzia uchanguzi ujao wa 2015, nafasi za wagombea ubunge majimbo yote nchini zitatangazwa kwenye magazeti.

Dk. Slaa alisema baada ya waombaji kujitokeza watafanyiwa usaili kwa kufanya mtihani utakaokuwa umeandaliwa kwa kuzingatia nafasi hizo.

“Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe amekwisha kusema kwamba kuanzia sasa hatupokei makapi kutoka Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na hili naliweka wazi kwamba uchaguzi ujao utakuwa na mfumo mpya na wenye mabadiliko makubwa, tunaamini utaleta uzalendo na kuondoa upuuzi unaojitokeza.

“Kwa wale walio na mipango ya kujitokeza dakika za mwisho kugombea nafasi za ubunge kupitia Chadema au nje ya chama, naomba wasahau hilo tunataka mtu anayetetea wananchi, mwenye uzalendo, hoja, ujasiri na mwenye kuitoa Tanzania hapa ilipo na kuisogeza mbele,”alisema.

Akizungumzia suala la mchakato wa katiba mpya alisema Chadema haitakubali kuona inakuwa sehemu ya watu walioshiriki kutengeneza katiba isiyo ya Watanzania wote.
 

Comi

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
3,329
1,500
Mamluki ya mizigo itakuja na porojo zao mda si mrefu. Nadhani hiyo itakuwa ni hatua njema na pia ingekuwa bora kabla ya kutangazwa rasmi kugombea wakatangazwa kwenye magazeti ili kama kasoro zitakazo jitokeza iwe rahisi kumbadilisha
 

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,403
2,000
Hilo ni wazo zuri, for consistency ingependeza iwe kwa nafasi zote, sio ubunge tu maana nina uhakika wakati wa kuchambua waombaji hata vetting itafanyika
 

AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,505
2,000
Naenda kugombea ubunge kigoma kaskazini kwa Zitto, wakuu mniunge mkono.
 
Last edited by a moderator:

ichenjezya

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
1,007
2,000
Mi nataka nikagombee Mbozi Mashariki pale pa yule kipolokoto Zambi,niungane na kamanda Silinde,maana wanainchi wanapata shida sana,tulimpa kura yule zolombwe msaliti na mchumia tumbo Stellah Mwampamba akaachia jimbo kwa milioni saba njaa mbaya sana!
 

Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,520
2,000
, tunaamini utaleta uzalendo na kuondoa upuuzi unaojitokeza. .

Hapa ndipo nikiwa mlipa kodi wa nchi hii napata hasira, ina maana tunamlipa mtu wa kuandaa hizi press conference na bado anakwenda kumuandalia maneno kama haya babu wa watu. Ndio maana mmemgeuza huyu babu kuwa kituko day in day out.
 

NYACHA

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
273
225
Naenda kugombea ubunge kigoma kaskazini kwa Zitto, wakuu mniunge mkono.

We unamatatzo! Utaambulia kura yako, ya mkeo na hawa;ra ako tu! Zitto mfarume wa Kg! LEKA TUTIGITE WI SHAVU AMENEKE!!
 
Last edited by a moderator:

Tozeshai Kiagha

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
210
225
Uwazi na Ukweli ndio msingi Imara wa kuendesha shughuli zote za kisiasa,kiuchumi na kijamii.
Hongera CHADEMA kwa ubunifu makini utakaoleta tija katika uteuzi wa watu makini ili kukidhi haja ya Uongozi Bora ndani ya Chama na Taifa kwa ujumla.
 

Rockcity native

JF-Expert Member
Dec 31, 2012
2,139
2,000
Hivi kufanya mtihani kunakufanya uwe na haiba ya kuchaguliwa na wananchi? Halafu huo mtihani utampimaje mtu kutambua ni mzalendo? Any way ngoja nianze mishe mishe za kuchukua form ili nikagombee nyamagana.
 

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
0
Hapa ndipo nikiwa mlipa kodi wa nchi hii napata hasira, ina maana tunamlipa mtu wa kuandaa hizi press conference na bado anakwenda kumuandalia maneno kama haya babu wa watu. Ndio maana mmemgeuza huyu babu kuwa kituko day in day out.

Tofauti na wewe, mimi huwa nasema ukweli ambao mtu yeyote anaweza kuu-verify! Nimeshawahi kupigwa ban hapa hapa kwa kusema ukweli ambao (naambiwa) kuwa ulikiuka sheria za JF! Invisible, nimwambie kinachomstahili huyu mtu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom