Mnaotaka kuoa Zanzibar, Samaki hageuzwi

Mnaotaka kuoa Zanzibar, Samaki hageuzwi

Dr. Mariposa

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
4,636
Reaction score
15,247
Guys ninaandika haraka haraka maana nampepea bwana harusi mtarajiwa amezimia baada ya kukataliwa kuoa binti mzuri wa kizanzibar,

Huyu jamaa baada ya kuposa na kulipa mahari yote akapata mualiko maalum wa kuonana na familia ya wakwe zake watarajiwa na kupata chakula cha mchana pamoja, nilimwambia kua akipewa samaki ale kiduchu tu ila chonde chonde asimgeuze,

Basi bwana na mie nilikua mmoja wa wapambe wa bwana harusi mtarajiwa kama mjuavyo tamaduni ni kua wanawake hukaa sehemu yao na wanaume hukaa sehemu yao lakini wakati tunaachana akakae upande wa wanaume nikamkumbusha tena "huku Zenji ukiwa ukweni samaki hagaezwi" akasema nisikonde "chill, i got this...." hayo ndio maneno ya mwisho kunambia kabla hajazimia 😭😭😭😭

Huyu bwana akapewa bonge la samaki unajua samaki wa kupaka weweeee, jamaa akapagawa akasahau onyo nililompa akaanza kumgegedua samaki upande wa kwanza ukaisha akamgeuza na kuendelea kumfakamia kwa fujo huku akijiramba vidole daah!🥺 hapo hapo baba wa bibi harusi akasimama kwa hasira na kuanza kumfokea sana kwanini kamgeuza yule samaki, akasema ndoa haipo tena mahari yake amtume mshenga wake akaifate kesho asubuhi sana na kuondoka huku akirusha rusha mikono, taharuki ikatokea jamaa tunamuuliza vipi hajajibu akadondoka na kuzimia......

Nitaendelea kuwapa updates ila ndio hivyo mkija Zanzibar kuoa chonde chonde msimgeuze samaki.
 
Zinaa imekuwa rahisi kwa sababu ya ujinga ,ndoa ni process kuliko kumfanya single mother...Vijana msiende kuoa ni kazi ngumu kweli ,labda binti awe simple .

Jamaa wanamtumia magettoni ,sasa wewe nenda uone hayo masharti....Kwa sasa hata Gauni wanataka la laki sita ili wafanane na wenzao ....Ukiona dharau tu ondoka kwani ni kwenu huko.

Kuna dogo alikuwa kaziniwa sana mpaka kafika miaka 30 ila hana mtoto , inawezekana kachoropoa mimba ..Jamaa kaenda kumposa a demu anajulikana ni kicheche ni vile katulia kwa vile umri umeenda ...Duh! Hayo masharti aliyopewa na mwanamke anataka harusi kubwa mtaa mzima wajue ,gauni la laki 7 ,mahari na mambo mengine yaani sherehe kubwa ...Atoe huduma za mwanamke kipind cha uchumba na harusi kapewa kalenda miezi miwili na nusu mbele ... Oneni ujinga wa watu ,bora kuwazini hawa katika mazingira haya.


Anayetaka kuoa anapewa mlolongo mrefu ,nikitaka kuoa naingia kwa wasambaa wenzangu sio washamba ,hawana shobo na pesa za mtu ..Unapewa jiko ,kitu bikra siku moja hakuna mlolongo wala utapeli wa mshenga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom