COARTEM
JF-Expert Member
- Nov 26, 2013
- 3,598
- 3,644
Lengo la serikali kuruhusu maduka hayo kuwepo maeneo ya hospitali lilikuwa zuri tu. Waliagizwa kuuza dawa kwa bei nafuu na maduka hayo yafunguliwe saa 24 kila siku. Lakini baada ya maduka hayo kuanza kufanya kazi, kuna watendaji wa serikali wasiokuwa waaminifu walianza kuweka maslahi yao kwenye maduka hayo. Wenye maduka hayo wakaanza kukiuka maelekezo ya serikali na kufanya mambo wanayo yajuwa wao. Bei za dawa zilipandishwa maradufu kuliko hata maduka ya dawa yaliyo mbali na hospitali.
Mfano
NAUNGA MKONO AGIZO LA SERIKALI KUFUNGA MADUKA HAYO PEMBENI MWA HOSPITALI ZA UMMA!
Agizo liko hapa Maduka yote ya dawa nje ya hospitali za Serikali marufuku
Mfano
- Dawa inayouzwa hospitali Tshs 800/= ( maduka pembeni mwa hospitali wanauza Tshs 4000/=) wakati maduka yaliyo mbali kidogo just mwendo wa dk 10 wao wanauza dawa hiyoTshs 1000/= hadi 1500/=.
- Dawa inayouzwa hospitali Tshs 5000/= ( maduka pembeni mwa hospitali wanauza Tshs 35,000/=) wakati maduka yaliyo mbali kidogo just mwendo wa dk 10 wao wanauza dawa hiyoTshs 15,000/= hadi 20,000/=.
- Dawa inayouzwa hospitali Tshs 1000/= ( maduka pembeni mwa hospitali wanauza Tshs 5000/=) wakati maduka yaliyo mbali kidogo just mwendo wa dk 10 wao wanauza dawa hiyoTshs 2000/= hadi 2500/=.
- Maduka hayo hayafunguliwi saa 24 kama ilivyokubaliwa, lugha za watoa huduma ni mbovu kama zilivyo za watoa huduma wa ndani ya hospitali. Ukitaka kuamini nilicho kiandika nenda Hospitali ya Mkoa Morogoro kwenye lile duka la nje ya geti kuu la hospitali hiyo utaelewa hiki nilicho kiandika. Lile duka nje ya geti la Hospitali ya mkoa Morogoro ni zaidi ya wezi. Nunua dawa ndani ya hospitali hiyo kisha nenda kanunue dawa hiyo hiyo kwenye hilo duka nje ya geti maweeee......utalia.
NAUNGA MKONO AGIZO LA SERIKALI KUFUNGA MADUKA HAYO PEMBENI MWA HOSPITALI ZA UMMA!
Agizo liko hapa Maduka yote ya dawa nje ya hospitali za Serikali marufuku