Mnaopanga kuandamana tena

Mnaopanga kuandamana tena

Unatakiwa uwe mstari wa mbele kwenye Maandamano, usife kizembe au kindezi na njaa.
Ukifa kwenye maandamano wewe ni shujaa wa Taifa.
Tukifanikiwa watakao baki wanatakiwa wafukue makaburu yote ya mashujaa wazike upya na Mizinga ipigwe100, (Mia).

Hapo ni kama unaomba Maisha Mrefu alafu ya tabu
Unawadanganya wenzio eti ukifa kwenye maandamano ni ushujaa..?
 
Taifa lipo kwenye uvamizi wa kigaidi wewe unawaza maandazi mpumbavu mkubwa. Kwenye nature kuna kitu kinaitwa Survival of the fittest. Tafsiri yake ni kuwa watu dhaifu kama wewe ambaye hausimami na raia wengine ni lazima maandazi ukose ili ufe njaa taifa lipate raia makini wachache wajenge taifa imara.

Ni watu kama wewe ndio sababu hadi leo tanzania taifa lenye miaka zaidi ya 50+ ya uhuru bado limenasa katika stage ya umasikini wa kipato cha chini. Ni watu kama wewe ndio hawa matapeli wa siasa wanawatumia kuaminisha jamii kuwa sisi ni masikini na tunatakiwa kuombewa misaada.

Sasa ili sekeseke la mabadiliko ya kimfumo litapita na wapuuzi kama wewe hadi akili ikukae sawa ubadilike. Kama wewe unawaza maandazi unamuwazia nini mtoto wako kesho yake?
Umasikini hauwezi kuisha. Halafu umasikini ni fikra za mtu sio vitu.
 
Mtufikirie na sisi tunaoishi Maisha magumu...tunaoshindia maandazi na maji na bado na bado tunategemea kudra wengine tunajitegemea huku tuna challenge za kiafya

Vikiumana huko mtatuua wenzenu🥲
Tutakucheki mkuu, si upo around external ubungo au around hayo maeneo ?
 
Back
Top Bottom