Mnaomponda Rais Magufuli mnakosea sana

Mnaomponda Rais Magufuli mnakosea sana

eti unakuja na hoja za miaka ya 90 gizani,mara edward lowasa,mara ndege..hivi kwel ubongo wako uko safi au umechanganyika na usaha unahitaji utumbuliwe?unajua unanshangaza sana na kunipa wakati mgumu kuchangia huo uharo..
 
Tatizo lenu mnaongea sana kwa vitu vdogo tu mnavyo fanya mbona ndege kitu kidogo tu utalinganisha na ile hospitali ya moyo muhimbili? au ile hospitali ya aliye jenga kibamba tawi la chuo kikuumuhimbili,pale UDOM kuna hospital ya figo lakini kelele siyo kama mnazo piga kwa vitu vidogo vdogo tu.
Hicho ni kipindi cha miaka 10
 
labda nikuulze swali,wakosoaji ambao wew unawaita wapondaji,wanamponda/kukosoa kwa kuangalia enzi za JKN,AM,BWM,JMK au ni kulingana na awamu yake na matendo yake?yaan bado unanipa maswali mengi ya kukuulza lakini hata nikkuulza "you are a low mind"..
 
Ulichoandika ni sawa na kusema tumuunge mkono Idi Amini sababu alikua anapenda watoto wake, alikua anapenda nchi iwe independent, alikua ana~ndoto ya independent african, alikua anafanya sherehe kubwa na kualika kila mtu.

Ni ujinga maana unayoongea yote ni yale positive tu, wanaompinga wanatumia points negative, hizo ndizo point ilitakiwa uzionyeshe kua sio za maana, mfano ungeonyesha kwa nini uvunjaji wa katiba anaoufanya Rais kwa kujiamlia, matamko ya kila wakati, kwa nini unahisi ni positive, hapo ndo ungefanya argument yako ionekane valid. Ulichoandika unapoteza muda tu ni mambo kila mtu anajua.
 
Mwezi wa 11 mkutano mwengine wa kimataifa mungu saidia baba yetu aende.
Unadhani akihudhuria mikutano ya kimataifa anaongezea nini taifa letu? Au sifa tu kahudhuria hiyo mikutano? Na anavyowakilishwa kunakuwa na mapungufu gani?
 
Kiukweli nawashangaa sana - inawezekana vipi kila alifanyalo liwe baya kwao?
Mbona watumia barabara alizosimamia? - Mbona wanapokea waliokuwa viongozi waliowadai ni wachafu sana? wamwache JPM arudishe heshima ya tanzania aisee!
Kwani hizo barabara zimejengwa kwa kodi za nani?
 
Tusipotezeane Muda kila mtu anamaono yake sitaki mimi alinitoka pale aliposema wananchi wapige mbizi baada ya kuleta kile kivuko [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] biashara yake NA mie iliisha pale
Huwa hampendi ukweli. Mnapenda mtu wa kupambapamba maneno. Mh JPM hajaumbwa hivyo.
Ulitafasili hivyo pasipo kujua alikuwa na maana gani. Ulilishikilia hilo neno tu. Na nadhani tatizo ni uelewa wako. Aliona nauli ya awali isingeweza kumudu kuendesha hicho kivuko. Akaona ni muhimu bei iongezeke kumudu ghalama za uendeshaji. Tatizo ilikuwa ni nini hapo?
 
WanaJf, salaam!
Ninapata wakati mgumu kuona humu JF watu wanaponda kila jambo alifanyalo Mhe. Dkt Magufuli - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ni kundi linalounda vyama vya upinzani nchini hebu rejeeni mambo yafuatayo kisha njooni tuanze mjadala:
1. Wakati tunaanza vyama vingi vya siasa mwaka 1995 kundi la wapinzani likiundwa na Agoustino Lyatonga Mrema, Masumbuko Lamwai, Makongoro Nyerere, Ibrahimu Haruna Lipumba, n.k walipopanda majukwaa walinena kuwa nchi yetu haina barabara za lami - leo hii barabara zimekamilika (Sasa kwa nini msione kuwa serikali imefanya kazi kubwa kujenga barabara nchi nzima?);

2. Wakati Mhe. Dkt Magufuli ananunua ndege watu wameingia humu wakiwa na hangover wakiponda ndege hiyo - Sasa ndege hiyo imefika ndo uone jinsi kundi hilo linavyotumia ndege hizo kwa safari zao. Sasa ndege zimefika hapo hapo mnaanza oooo waandishi wamekataliwa, ooo mapanga (Jamani mbona leo tunateseka na wakwepa kodi wakiwemo viongozi wa juu wa vyama vya upinzani nchini?);

3. Miaka ya 2000 mkapata majukwaa agenda yenu kuu ilikuwa ufisadi na hapa wapinzania mlimwandama Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu) - na siku anatoka kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM kauli za viongozi na wanasiasa wa upinzani nchini zilimwandama Mhe. huyo kwa kumtaja kwenye kundi la MAFISADI wengine wakisema Nyangumi - sasa baada ya kupata rais msafi leo tena watu hao hao wanarudi kumsafisha PAPA na kumwandama Mhe Magufuli eti kwa kumuundia UKUTA;

4. Nimeenda mbali zaidi kutafakari kauli ya Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akiwa jangwani wakati wa ufunguzi wa Kampeni za uchaguzi mkuu 2015 - hapo kwa hasira alitoa maneno watu hao hao watu wale wale wakaanza kusema eti kawatukana. Hivi kwa hali ya kawaida chama kumpokea mtu aliyekuwa awali anawekwa kwenye kundi chafu mara ghafla eti kwa kuwa amebadili chama ndiyo anakuwa msafi!!!! - EPUKENI AIBU HIZI!

5. Tena wakati wa serikali iliyomaliza muda wake mlinong'ona sana sana juu ya rais aliyekuwepo kuwa na safari za kwenda nje (Hapa mliweka mpaka data za ulinganishi na marais wengine). Sasa tumepata rais anayeamini kuwa mabalozi walioko nje wanafaa kutuwakilisha vema kimataifa hivyo amewapa mamlaka za kumwakilisha - hapa napo siku chache sana toka 2015 mmesahau na kuanza kupika majungu! - REJEENI SAFARI ZA RAIS 2012 - 2015;

6. Kuhusu watanzania kuhakikisha wanatumia muda mwingi katika kuzalisha kuliko kukaa vijiweni, kushinda kwenye mikutano ya kisiasa n.k Baada ya rais kutoa maelekezo kwa viongozi waandamizi mnaanza kukurupuka na kusema ooo mara rais ni Dikteta mpaka munaunda kundi lisilokuwa na kichwa wala miguu! HIVI MNGESHINDA 2015 MNGEPENDA KUTAWALA WATU WANAOSHINDA KTK MIKUTANO NA VIJIWE VYA KISIASA?

Kimsingi mambo ya kuongea ninayo mengi sana ila leo naishia hapa - UJUMBE

''MWACHENI RAIS WETU MHE. DKT. JOHN P. J. MAGUFULI ACHAPE KAZI ILI NCHI ISONGE MBELE KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI, KIJAMII, KITEKNOLOJIA NA KIUCHUMI''

Msakila M. Kabende
MWANAHARAKATI - NIPINGE KWA HOJA BILA KUFICHA JINA TUJADILIANE KWEUPE!

SITHANI KAMA KUNA YEYOTE MPENDA HAKI NA UKWELI ATAPINGA MANENO YAKO. WATANZANIA TUNA BAHATI KUBWA SANA KUMUPATA MTU KAMA RAIS MAGUFULI. TULIKUWA TUMEKATA TAMAA. MASIKINI ALIKUWA HANA HAKI BALI MWENYE PESA. WATOTO WETU WALIKUWA NA SHIDA WAKIKAA CHINI, SASA WANAKAA KWENYE VITI. HOSPITAL ZETU ZILIKUWA ZIMESAHULIKA TUKAKIMBILIA KWA WAGANGA WA KIENYEJI, MAWAZO YETU YAKAFIFIA KWA KUKOSA MATEGEMEO. RAIS HUYU ANA MWAKA MMOJA TU, NA MABADILIKO MAKUBWA TUNAYAONO, UCHAFU MWINGI UMEONEKANA, SIJUI HATA HIYO MIAKA KUMI ITATOSHA KUISAFISHA TANZANIA. TUNAMUOMBEA MUNGU AMUWEKE SALAAMA, NA WENYE KUMUOMBEA MABAYA NI WALE WENGI WALIKUWA WAKIFAIDI SHIDA ZA WENGI, MUNGU AWASAMEHE HAWAJUI WANAFANYA NINI. AMALIZE MIAKA KUMI AONGEZEWE MIAKA MINGINE 10. TANZANIA INAHITAJI MIAKA 20 KUKAA SAWA, KISHA TUENDELEE NA KATIBA YA MIAKA MITANO. WASI WASI SIJUI NANI ATASHIKA BADALA YAKE, MUNGU ATUSAIDIE.
 
Vyama vingi havikuanzishwa 95 bali 92,pia agenda kuu ilikuwa kuondoa rushwa na kuboresha maisha ya mwananchi wa kawaida.
wapinzani wamepiga kelele sana kuhusu ufisadi na kuibua madudu mengi wakiwa bungeni,wakati wapinzani wakisema lowassa fisadi mwanaccm gani alieunga mkono wapinzani na kusema kuwa ni fisadi ila riporti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za ufisadi dhidi yake ilitolewa bungeni na kusema hana hatia,wapo pia mafisadi kama chenge,muhongo,tibaijuka wanaccm hamuwazungumzii kuwa ni mafisadi ila wakitoka ndio utasikia wanasemwa mnatakiwa muwaseme leo hata wakiamia chama kingine wajulikane waliondolewa ccm kwa ufisadi.mwisho, kuhusu kuzuia siasa,lazima uelewe nchi hii ni ya kidemokrasia na utawala wa sheria ambayo ni katiba,sheria inaruhusu watu kukusanyika na kutoa maoni yao,kupinga,kukosoa au kupongeza,kama kiongozi utazuia inamaana huitambui sheria hii,safari za nje mbona zipo kama kawaida kwani mama samia katoka mara ngapi nje kumwakilisha rais,kwa hiyo akisafiri makamu hana gharama.
 
Mwandishi wa post kuna vitu umechanganya, kuna kupinga na kukosoa au kurekebisha, ndyo maana kuna neno vyama vya upinzani siyo vya kusifia, nikukumbushe usemi usemao" when all consensus agree then politics is redundant " .

Usitegemee kila mtu akubali unachoona wwe ni sahihi na kusifia unachodhani wwe kiko safi.
Acha watu wakosoe, wasifie ndiyo maendeleo isionekane kukosoa ni nongwa kwa hoja eti rais ni msafi kuliko hata waliokuwepo.
Kukosoana ni jambo la muhimu sana. Lkn kosoa penye makosa na sifia palipo sahihi. Lakini kwa wenzangu na mimi kila jambo ni kukosoa kisa tu limefanywa na ccm. Hatutafika.
Hebu fikilia ni mara ngapi tumekosoa nchi kukosa ndege. Sasa ndege imenunuliwa tunakosoa. Ndege hiyo ni yenye kuendana na viwanja tulivyonavyo. Haitumii umbali mrefu kutua hadi kusimama. Hii ni kutokana na uasili wa viwanja vyetu vya ndege. Je tunalaumu nini kwa hilo!! Ingenunuliwa ndege yenye uhitaji mrefu wa kutua hadi kusimama ina maana isingetua baadhi ya mikoa/viwanja. Hapo ndiyo tungekuwa na kila sbb ya kulaum.

Tumekuwa tukilaumu ufisadi umezidi serikalini. Ameanza kushughulika na hilo la ufisadi tunamwita dikteta na kwamba anawaonewa watu kwa kuwasimamisha kazi hovyo. Jema kwetu ni lipi?

Tumemlaumu saana jk kuwa anatumia pato kubwa la nchi katika safari za nje. JPM aliliona hilo. Amekuwa hasafiri mara kwa mara na kuwatumia wawakishi nayo tunakosoa.

Tulilaumu kuwa jk amekuwa mpole sana jpm amekuwa mkali tunakosoa.

Tulilaumu matumizi makubwa ya serikali. Jpm ameamua kubana matumizi ya serikali. Tunakosoa.

JE HUO NDIYO UPINZANI??!!
 
Ulichoandika ni sawa na kusema tumuunge mkono Idi Amini sababu alikua anapenda watoto wake, alikua anapenda nchi iwe independent, alikua ana~ndoto ya independent african, alikua anafanya sherehe kubwa na kualika kila mtu.

Ni ujinga maana unayoongea yote ni yale positive tu, wanaompinga wanatumia points negative, hizo ndizo point ilitakiwa uzionyeshe kua sio za maana, mfano ungeonyesha kwa nini uvunjaji wa katiba anaoufanya Rais kwa kujiamlia, matamko ya kila wakati, kwa nini unahisi ni positive, hapo ndo ungefanya argument yako ionekane valid. Ulichoandika unapoteza muda tu ni mambo kila mtu anajua.
Well said brother..
 
Halafu anafikiri hizo barabara zimejengwa kwa pesa toka Lumumba!dah!wakati ni kodi zetu!
Kama umehitimu hata darasa la saba bado hata hiyo Elimu kidogo haikukusaidia. Ni nchi gani duniani imejenga barabara kwa pesa za chama?
Hapa kinachoongelewa ni usimamizi wa hizo pesa zakodi unazosema na hizo pesa zikajenga barabara. Hivyo inafahamika wazi kwamba pesa za kujenga barabara chanzo chake ni nini.

Kumbe ndiyo maana mliambiwa Lowasa ni fisadi papa na baada ya mda mfupi mnaambiwa Tanzania hakuna msafi kama Lowasa nanyi mnashangilia. Badala ya kuhoji kuwa amekuwa msafi tangu lini wakati nyie ndiyo mlituambia kuwa ni fisadi papa. Na tena mkatuambia atakaemchagua Lowasa inabidi apimwe akili. Kwa mwenye busara ilitakiwa tuwahoji wao wanatuambia tumchaguwe Lowasa je wamepimwa akili?

KUMBE KAZI BADO NI KUBWA. KWA WACHANGIAJI WA AINA HII!!!
 
WanaJf, salaam!
Ninapata wakati mgumu kuona humu JF watu wanaponda kila jambo alifanyalo Mhe. Dkt Magufuli - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ni kundi linalounda vyama vya upinzani nchini hebu rejeeni mambo yafuatayo kisha njooni tuanze mjadala:
1. Wakati tunaanza vyama vingi vya siasa mwaka 1995 kundi la wapinzani likiundwa na Agoustino Lyatonga Mrema, Masumbuko Lamwai, Makongoro Nyerere, Ibrahimu Haruna Lipumba, n.k walipopanda majukwaa walinena kuwa nchi yetu haina barabara za lami - leo hii barabara zimekamilika (Sasa kwa nini msione kuwa serikali imefanya kazi kubwa kujenga barabara nchi nzima?);

2. Wakati Mhe. Dkt Magufuli ananunua ndege watu wameingia humu wakiwa na hangover wakiponda ndege hiyo - Sasa ndege hiyo imefika ndo uone jinsi kundi hilo linavyotumia ndege hizo kwa safari zao. Sasa ndege zimefika hapo hapo mnaanza oooo waandishi wamekataliwa, ooo mapanga (Jamani mbona leo tunateseka na wakwepa kodi wakiwemo viongozi wa juu wa vyama vya upinzani nchini?);

3. Miaka ya 2000 mkapata majukwaa agenda yenu kuu ilikuwa ufisadi na hapa wapinzania mlimwandama Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu) - na siku anatoka kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM kauli za viongozi na wanasiasa wa upinzani nchini zilimwandama Mhe. huyo kwa kumtaja kwenye kundi la MAFISADI wengine wakisema Nyangumi - sasa baada ya kupata rais msafi leo tena watu hao hao wanarudi kumsafisha PAPA na kumwandama Mhe Magufuli eti kwa kumuundia UKUTA;

4. Nimeenda mbali zaidi kutafakari kauli ya Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akiwa jangwani wakati wa ufunguzi wa Kampeni za uchaguzi mkuu 2015 - hapo kwa hasira alitoa maneno watu hao hao watu wale wale wakaanza kusema eti kawatukana. Hivi kwa hali ya kawaida chama kumpokea mtu aliyekuwa awali anawekwa kwenye kundi chafu mara ghafla eti kwa kuwa amebadili chama ndiyo anakuwa msafi!!!! - EPUKENI AIBU HIZI!

5. Tena wakati wa serikali iliyomaliza muda wake mlinong'ona sana sana juu ya rais aliyekuwepo kuwa na safari za kwenda nje (Hapa mliweka mpaka data za ulinganishi na marais wengine). Sasa tumepata rais anayeamini kuwa mabalozi walioko nje wanafaa kutuwakilisha vema kimataifa hivyo amewapa mamlaka za kumwakilisha - hapa napo siku chache sana toka 2015 mmesahau na kuanza kupika majungu! - REJEENI SAFARI ZA RAIS 2012 - 2015;

6. Kuhusu watanzania kuhakikisha wanatumia muda mwingi katika kuzalisha kuliko kukaa vijiweni, kushinda kwenye mikutano ya kisiasa n.k Baada ya rais kutoa maelekezo kwa viongozi waandamizi mnaanza kukurupuka na kusema ooo mara rais ni Dikteta mpaka munaunda kundi lisilokuwa na kichwa wala miguu! HIVI MNGESHINDA 2015 MNGEPENDA KUTAWALA WATU WANAOSHINDA KTK MIKUTANO NA VIJIWE VYA KISIASA?

Kimsingi mambo ya kuongea ninayo mengi sana ila leo naishia hapa - UJUMBE

''MWACHENI RAIS WETU MHE. DKT. JOHN P. J. MAGUFULI ACHAPE KAZI ILI NCHI ISONGE MBELE KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI, KIJAMII, KITEKNOLOJIA NA KIUCHUMI''

Msakila M. Kabende
MWANAHARAKATI - NIPINGE KWA HOJA BILA KUFICHA JINA TUJADILIANE KWEUPE!
Wendiowalewale fuata upepo nyie ndio spy wenyewe
 
Huwa hampendi ukweli. Mnapenda mtu wa kupambapamba maneno. Mh JPM hajaumbwa hivyo.
Ulitafasili hivyo pasipo kujua alikuwa na maana gani. Ulilishikilia hilo neno tu. Na nadhani tatizo ni uelewa wako. Aliona nauli ya awali isingeweza kumudu kuendesha hicho kivuko. Akaona ni muhimu bei iongezeke kumudu ghalama za uendeshaji. Tatizo ilikuwa ni nini hapo?
Ameumbwa hivyo angekuwa babangu heeee.... Ngoja nijinyamazie
 
P
Kama unawaambia Ukawa maneno haya ukidhani wataelewa unajisumbua,Mimi wakati ule nifikiria waliokuja na jina la 'nyumbu' walikua wame exaggerate lakini sasa nimeanza kuona walifikiria mbali.
Watu wawili wakikubaliana kwa kila kitu ujue mmojawapo hafikiri.
Ipo tofauti kubwa sana kati ya kukosoa na kupinga.
Watu wanaosifia kila kitu ni hatari na breki kwa ustawi wa taifa. Mara nyingi, kama siyo mara zote, ni wanafiki. Hujipendekeza ili wapate mradi wao.
 
Mwandishi wa post kuna vitu umechanganya, kuna kupinga na kukosoa au kurekebisha, ndyo maana kuna neno vyama vya upinzani siyo vya kusifia, nikukumbushe usemi usemao" when all consensus agree then politics is redundant " .

Usitegemee kila mtu akubali unachoona wwe ni sahihi na kusifia unachodhani wwe kiko safi.
Acha watu wakosoe, wasifie ndiyo maendeleo isionekane kukosoa ni nongwa kwa hoja eti rais ni msafi kuliko hata waliokuwepo.
Ni kweli kabisa kila mtu hawezi kukubali unachokisema au kinachofanyika lakini si kkweli kuwa kila unachokisema wewe kiwe sahihi na sio kila anachofanya mwenzako sio sahihi. pia unapokosoa ni vizuri ukatoa na njia mbadala sasa wapinzani wao kila kitu kukosoa na hawatoi njia mbadala wa kufanya hivyo vitu lejea Bungeni na katika majukwaa yao ya siasa kila siku kukosoa bila busara na bila kuota njia mbadala ya kufanya mambo,
 
WanaJf, salaam!
Ninapata wakati mgumu kuona humu JF watu wanaponda kila jambo alifanyalo Mhe. Dkt Magufuli - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ni kundi linalounda vyama vya upinzani nchini hebu rejeeni mambo yafuatayo kisha njooni tuanze mjadala:
1. Wakati tunaanza vyama vingi vya siasa mwaka 1995 kundi la wapinzani likiundwa na Agoustino Lyatonga Mrema, Masumbuko Lamwai, Makongoro Nyerere, Ibrahimu Haruna Lipumba, n.k walipopanda majukwaa walinena kuwa nchi yetu haina barabara za lami - leo hii barabara zimekamilika (Sasa kwa nini msione kuwa serikali imefanya kazi kubwa kujenga barabara nchi nzima?);

2. Wakati Mhe. Dkt Magufuli ananunua ndege watu wameingia humu wakiwa na hangover wakiponda ndege hiyo - Sasa ndege hiyo imefika ndo uone jinsi kundi hilo linavyotumia ndege hizo kwa safari zao. Sasa ndege zimefika hapo hapo mnaanza oooo waandishi wamekataliwa, ooo mapanga (Jamani mbona leo tunateseka na wakwepa kodi wakiwemo viongozi wa juu wa vyama vya upinzani nchini?);

3. Miaka ya 2000 mkapata majukwaa agenda yenu kuu ilikuwa ufisadi na hapa wapinzania mlimwandama Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu) - na siku anatoka kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM kauli za viongozi na wanasiasa wa upinzani nchini zilimwandama Mhe. huyo kwa kumtaja kwenye kundi la MAFISADI wengine wakisema Nyangumi - sasa baada ya kupata rais msafi leo tena watu hao hao wanarudi kumsafisha PAPA na kumwandama Mhe Magufuli eti kwa kumuundia UKUTA;

4. Nimeenda mbali zaidi kutafakari kauli ya Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akiwa jangwani wakati wa ufunguzi wa Kampeni za uchaguzi mkuu 2015 - hapo kwa hasira alitoa maneno watu hao hao watu wale wale wakaanza kusema eti kawatukana. Hivi kwa hali ya kawaida chama kumpokea mtu aliyekuwa awali anawekwa kwenye kundi chafu mara ghafla eti kwa kuwa amebadili chama ndiyo anakuwa msafi!!!! - EPUKENI AIBU HIZI!

5. Tena wakati wa serikali iliyomaliza muda wake mlinong'ona sana sana juu ya rais aliyekuwepo kuwa na safari za kwenda nje (Hapa mliweka mpaka data za ulinganishi na marais wengine). Sasa tumepata rais anayeamini kuwa mabalozi walioko nje wanafaa kutuwakilisha vema kimataifa hivyo amewapa mamlaka za kumwakilisha - hapa napo siku chache sana toka 2015 mmesahau na kuanza kupika majungu! - REJEENI SAFARI ZA RAIS 2012 - 2015;

6. Kuhusu watanzania kuhakikisha wanatumia muda mwingi katika kuzalisha kuliko kukaa vijiweni, kushinda kwenye mikutano ya kisiasa n.k Baada ya rais kutoa maelekezo kwa viongozi waandamizi mnaanza kukurupuka na kusema ooo mara rais ni Dikteta mpaka munaunda kundi lisilokuwa na kichwa wala miguu! HIVI MNGESHINDA 2015 MNGEPENDA KUTAWALA WATU WANAOSHINDA KTK MIKUTANO NA VIJIWE VYA KISIASA?

Kimsingi mambo ya kuongea ninayo mengi sana ila leo naishia hapa - UJUMBE

''MWACHENI RAIS WETU MHE. DKT. JOHN P. J. MAGUFULI ACHAPE KAZI ILI NCHI ISONGE MBELE KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI, KIJAMII, KITEKNOLOJIA NA KIUCHUMI''

Msakila M. Kabende
MWANAHARAKATI - NIPINGE KWA HOJA BILA KUFICHA JINA TUJADILIANE KWEUPE!
Pole sana ndugu yangu Msakila M. kabende
Hakuna anaye mpinga rais wetu, watu wanamshauri afanye vizuri zaidi. Hawezi kujenga barabara kana kwamba gharama yake ni kuzuia uhuru wa kikatiba wa watu kukutana na kujadili mstabali wa maisha yao. Watanzania tumekuwa tukijilisha miaka yote na hakuna aliyetupangia tufanyeje kazi. Kuwanyima watu uhuru wa kikatiba ni udikiteita, klia aliyemkweli kwa nafsi yake anatakiwa kusema ukweli huu. Sio kosa la kisheria na wala sio dhambi kwa Mungu.

Serikali ya Mheshimiwa Mkapa, imejenga sana barabara kuliko vipindi vyote vya marais waliomtangulia. Mhe. Kikwete ameongezea pale alipoachia na Rais wa sasa anaendeleza pale aliposhia mtangulizi wake. Msahihishe sana Rais wetu, yeye amekuwa Rais baada ya uchaguzi na kuapishwa Nov. 2015, anamponda Rais aliyetangulia kwa kuharibu mambo mengi, lakini anapokuja kwenye barabara sifa za mtangulizi wake anazichukua yeye kwa kisingizio kuwa alikuwa waziri mwenye dhamana ya barabara. Sio kweli yeye atuonyeshe za kipindi chake alichokuwa rais.
 
Back
Top Bottom