Mnaomponda Rais Magufuli mnakosea sana

Mnaomponda Rais Magufuli mnakosea sana

mkafrend

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2014
Posts
3,045
Reaction score
1,503
WanaJf, salaam!
Ninapata wakati mgumu kuona humu JF watu wanaponda kila jambo alifanyalo Mhe. Dkt Magufuli - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ni kundi linalounda vyama vya upinzani nchini hebu rejeeni mambo yafuatayo kisha njooni tuanze mjadala:
1. Wakati tunaanza vyama vingi vya siasa mwaka 1995 kundi la wapinzani likiundwa na Agoustino Lyatonga Mrema, Masumbuko Lamwai, Makongoro Nyerere, Ibrahimu Haruna Lipumba, n.k walipopanda majukwaa walinena kuwa nchi yetu haina barabara za lami - leo hii barabara zimekamilika (Sasa kwa nini msione kuwa serikali imefanya kazi kubwa kujenga barabara nchi nzima?);

2. Wakati Mhe. Dkt Magufuli ananunua ndege watu wameingia humu wakiwa na hangover wakiponda ndege hiyo - Sasa ndege hiyo imefika ndo uone jinsi kundi hilo linavyotumia ndege hizo kwa safari zao. Sasa ndege zimefika hapo hapo mnaanza oooo waandishi wamekataliwa, ooo mapanga (Jamani mbona leo tunateseka na wakwepa kodi wakiwemo viongozi wa juu wa vyama vya upinzani nchini?);

3. Miaka ya 2000 mkapata majukwaa agenda yenu kuu ilikuwa ufisadi na hapa wapinzania mlimwandama Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu) - na siku anatoka kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM kauli za viongozi na wanasiasa wa upinzani nchini zilimwandama Mhe. huyo kwa kumtaja kwenye kundi la MAFISADI wengine wakisema Nyangumi - sasa baada ya kupata rais msafi leo tena watu hao hao wanarudi kumsafisha PAPA na kumwandama Mhe Magufuli eti kwa kumuundia UKUTA;

4. Nimeenda mbali zaidi kutafakari kauli ya Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akiwa jangwani wakati wa ufunguzi wa Kampeni za uchaguzi mkuu 2015 - hapo kwa hasira alitoa maneno watu hao hao watu wale wale wakaanza kusema eti kawatukana. Hivi kwa hali ya kawaida chama kumpokea mtu aliyekuwa awali anawekwa kwenye kundi chafu mara ghafla eti kwa kuwa amebadili chama ndiyo anakuwa msafi!!!! - EPUKENI AIBU HIZI!

5. Tena wakati wa serikali iliyomaliza muda wake mlinong'ona sana sana juu ya rais aliyekuwepo kuwa na safari za kwenda nje (Hapa mliweka mpaka data za ulinganishi na marais wengine). Sasa tumepata rais anayeamini kuwa mabalozi walioko nje wanafaa kutuwakilisha vema kimataifa hivyo amewapa mamlaka za kumwakilisha - hapa napo siku chache sana toka 2015 mmesahau na kuanza kupika majungu! - REJEENI SAFARI ZA RAIS 2012 - 2015;

6. Kuhusu watanzania kuhakikisha wanatumia muda mwingi katika kuzalisha kuliko kukaa vijiweni, kushinda kwenye mikutano ya kisiasa n.k Baada ya rais kutoa maelekezo kwa viongozi waandamizi mnaanza kukurupuka na kusema ooo mara rais ni Dikteta mpaka munaunda kundi lisilokuwa na kichwa wala miguu! HIVI MNGESHINDA 2015 MNGEPENDA KUTAWALA WATU WANAOSHINDA KTK MIKUTANO NA VIJIWE VYA KISIASA?

Kimsingi mambo ya kuongea ninayo mengi sana ila leo naishia hapa - UJUMBE

''MWACHENI RAIS WETU MHE. DKT. JOHN P. J. MAGUFULI ACHAPE KAZI ILI NCHI ISONGE MBELE KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI, KIJAMII, KITEKNOLOJIA NA KIUCHUMI''

Msakila M. Kabende
MWANAHARAKATI - NIPINGE KWA HOJA BILA KUFICHA JINA TUJADILIANE KWEUPE!
 
Hawa watu wana wivu sana, wanataman wangekuwa wao
Kiukweli nawashangaa sana - inawezekana vipi kila alifanyalo liwe baya kwao?
Mbona watumia barabara alizosimamia? - Mbona wanapokea waliokuwa viongozi waliowadai ni wachafu sana? wamwache JPM arudishe heshima ya tanzania aisee!
 
Halafu nimewaomba mjitokeze hadharani tujenge hoja na si kujificha katika vichaka vya karanga!
 
Kiukweli nawashangaa sana - inawezekana vipi kila alifanyalo liwe baya kwao?
Mbona watumia barabara alizosimamia? - Mbona wanapokea waliokuwa viongozi waliowadai ni wachafu sana? wamwache JPM arudishe heshima ya tanzania aisee!
Wanasumbuliwa na wivu.. sasa vichwa vyao vinasahau haraka ajabu, jana wanasema safari za nje hazifai leo wanataka rais aende nje, jana wanasema n aibu nchi haina ndege leo wanasema n mtumba na pangaboi, yaani hawana hoja tena, siku hizi wamebaki kuvizia rais kasema nn il wapate pa kusemea, siku akikaa kmya wiki nzima hutawaskia pia
 
WanaJf, salaam!
Ninapata wakati mgumu kuona humu JF watu wanaponda kila jambo alifanyalo Mhe. Dkt Magufuli - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ni kundi linalounda vyama vya upinzani nchini hebu rejeeni mambo yafuatayo kisha njooni tuanze mjadala:
1. Wakati tunaanza vyama vingi vya siasa mwaka 1995 kundi la wapinzani likiundwa na Agoustino Lyatonga Mrema, Masumbuko Lamwai, Makongoro Nyerere, Ibrahimu Haruna Lipumba, n.k walipopanda majukwaa walinena kuwa nchi yetu haina barabara za lami - leo hii barabara zimekamilika (Sasa kwa nini msione kuwa serikali imefanya kazi kubwa kujenga barabara nchi nzima?);

2. Wakati Mhe. Dkt Magufuli ananunua ndege watu wameingia humu wakiwa na hangover wakiponda ndege hiyo - Sasa ndege hiyo imefika ndo uone jinsi kundi hilo linavyotumia ndege hizo kwa safari zao. Sasa ndege zimefika hapo hapo mnaanza oooo waandishi wamekataliwa, ooo mapanga (Jamani mbona leo tunateseka na wakwepa kodi wakiwemo viongozi wa juu wa vyama vya upinzani nchini?);

3. Miaka ya 2000 mkapata majukwaa agenda yenu kuu ilikuwa ufisadi na hapa wapinzania mlimwandama Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu) - na siku anatoka kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM kauli za viongozi na wanasiasa wa upinzani nchini zilimwandama Mhe. huyo kwa kumtaja kwenye kundi la MAFISADI wengine wakisema Nyangumi - sasa baada ya kupata rais msafi leo tena watu hao hao wanarudi kumsafisha PAPA na kumwandama Mhe Magufuli eti kwa kumuundia UKUTA;

4. Nimeenda mbali zaidi kutafakari kauli ya Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akiwa jangwani wakati wa ufunguzi wa Kampeni za uchaguzi mkuu 2015 - hapo kwa hasira alitoa maneno watu hao hao watu wale wale wakaanza kusema eti kawatukana. Hivi kwa hali ya kawaida chama kumpokea mtu aliyekuwa awali anawekwa kwenye kundi chafu mara ghafla eti kwa kuwa amebadili chama ndiyo anakuwa msafi!!!! - EPUKENI AIBU HIZI!

5. Tena wakati wa serikali iliyomaliza muda wake mlinong'ona sana sana juu ya rais aliyekuwepo kuwa na safari za kwenda nje (Hapa mliweka mpaka data za ulinganishi na marais wengine). Sasa tumepata rais anayeamini kuwa mabalozi walioko nje wanafaa kutuwakilisha vema kimataifa hivyo amewapa mamlaka za kumwakilisha - hapa napo siku chache sana toka 2015 mmesahau na kuanza kupika majungu! - REJEENI SAFARI ZA RAIS 2012 - 2015;

6. Kuhusu watanzania kuhakikisha wanatumia muda mwingi katika kuzalisha kuliko kukaa vijiweni, kushinda kwenye mikutano ya kisiasa n.k Baada ya rais kutoa maelekezo kwa viongozi waandamizi mnaanza kukurupuka na kusema ooo mara rais ni Dikteta mpaka munaunda kundi lisilokuwa na kichwa wala miguu! HIVI MNGESHINDA 2015 MNGEPENDA KUTAWALA WATU WANAOSHINDA KTK MIKUTANO NA VIJIWE VYA KISIASA?

Kimsingi mambo ya kuongea ninayo mengi sana ila leo naishia hapa - UJUMBE

''MWACHENI RAIS WETU MHE. DKT. JOHN P. J. MAGUFULI ACHAPE KAZI ILI NCHI ISONGE MBELE KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI, KIJAMII, KITEKNOLOJIA NA KIUCHUMI''

Msakila M. Kabende
MWANAHARAKATI - NIPINGE KWA HOJA BILA KUFICHA JINA TUJADILIANE KWEUPE!
Tatizo lenu mnaongea sana kwa vitu vdogo tu mnavyo fanya mbona ndege kitu kidogo tu utalinganisha na ile hospitali ya moyo muhimbili? au ile hospitali ya aliye jenga kibamba tawi la chuo kikuumuhimbili,pale UDOM kuna hospital ya figo lakini kelele siyo kama mnazo piga kwa vitu vidogo vdogo tu.
 
Tusipotezeane Muda kila mtu anamaono yake sitaki mimi alinitoka pale aliposema wananchi wapige mbizi baada ya kuleta kile kivuko [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] biashara yake NA mie iliisha pale
 
Hivi Tanzania kuna barabara....ebu niambie ni barabara ipi unaweza endesha gari 20ks bila kukwepa shimo.??

Kiukweli nawashangaa sana - inawezekana vipi kila alifanyalo liwe baya kwao?
Mbona watumia barabara alizosimamia? - Mbona wanapokea waliokuwa viongozi waliowadai ni wachafu sana? wamwache JPM arudishe heshima ya tanzania aisee!
 
Mwandishi wa post kuna vitu umechanganya, kuna kupinga na kukosoa au kurekebisha, ndyo maana kuna neno vyama vya upinzani siyo vya kusifia, nikukumbushe usemi usemao" when all consensus agree then politics is redundant " .

Usitegemee kila mtu akubali unachoona wwe ni sahihi na kusifia unachodhani wwe kiko safi.
Acha watu wakosoe, wasifie ndiyo maendeleo isionekane kukosoa ni nongwa kwa hoja eti rais ni msafi kuliko hata waliokuwepo.
 
Back
Top Bottom