Mnaomponda Rais Magufuli mnakosea sana

Mnaomponda Rais Magufuli mnakosea sana

Watu bwana!watu wanapokwepa kulipa kodi wanawatangaza hadharani kwa kuwaita wakwepa kodi,hao hao wanaoitwa wakwepa kodi wakilipa kodi zao zikitumika kununua ndege,kujenga barabara,shule,hospitali n.k hawaimbiwi kuwa kodi zenu mulizolipa zimetumika kununulia ndege,zimetumika kujenga shule hospitali n.k matokeo yake ana sifiwa mtu ambaye huenda hata fedha yake haimo hata katika hayo yaliyofanyika.
 
WanaJf, salaam!
Ninapata wakati mgumu kuona humu JF watu wanaponda kila jambo alifanyalo Mhe. Dkt Magufuli - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ni kundi linalounda vyama vya upinzani nchini hebu rejeeni mambo yafuatayo kisha njooni tuanze mjadala:
1. Wakati tunaanza vyama vingi vya siasa mwaka 1995 kundi la wapinzani likiundwa na Agoustino Lyatonga Mrema, Masumbuko Lamwai, Makongoro Nyerere, Ibrahimu Haruna Lipumba, n.k walipopanda majukwaa walinena kuwa nchi yetu haina barabara za lami - leo hii barabara zimekamilika (Sasa kwa nini msione kuwa serikali imefanya kazi kubwa kujenga barabara nchi nzima?);

2. Wakati Mhe. Dkt Magufuli ananunua ndege watu wameingia humu wakiwa na hangover wakiponda ndege hiyo - Sasa ndege hiyo imefika ndo uone jinsi kundi hilo linavyotumia ndege hizo kwa safari zao. Sasa ndege zimefika hapo hapo mnaanza oooo waandishi wamekataliwa, ooo mapanga (Jamani mbona leo tunateseka na wakwepa kodi wakiwemo viongozi wa juu wa vyama vya upinzani nchini?);

3. Miaka ya 2000 mkapata majukwaa agenda yenu kuu ilikuwa ufisadi na hapa wapinzania mlimwandama Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu) - na siku anatoka kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM kauli za viongozi na wanasiasa wa upinzani nchini zilimwandama Mhe. huyo kwa kumtaja kwenye kundi la MAFISADI wengine wakisema Nyangumi - sasa baada ya kupata rais msafi leo tena watu hao hao wanarudi kumsafisha PAPA na kumwandama Mhe Magufuli eti kwa kumuundia UKUTA;

4. Nimeenda mbali zaidi kutafakari kauli ya Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akiwa jangwani wakati wa ufunguzi wa Kampeni za uchaguzi mkuu 2015 - hapo kwa hasira alitoa maneno watu hao hao watu wale wale wakaanza kusema eti kawatukana. Hivi kwa hali ya kawaida chama kumpokea mtu aliyekuwa awali anawekwa kwenye kundi chafu mara ghafla eti kwa kuwa amebadili chama ndiyo anakuwa msafi!!!! - EPUKENI AIBU HIZI!

5. Tena wakati wa serikali iliyomaliza muda wake mlinong'ona sana sana juu ya rais aliyekuwepo kuwa na safari za kwenda nje (Hapa mliweka mpaka data za ulinganishi na marais wengine). Sasa tumepata rais anayeamini kuwa mabalozi walioko nje wanafaa kutuwakilisha vema kimataifa hivyo amewapa mamlaka za kumwakilisha - hapa napo siku chache sana toka 2015 mmesahau na kuanza kupika majungu! - REJEENI SAFARI ZA RAIS 2012 - 2015;

6. Kuhusu watanzania kuhakikisha wanatumia muda mwingi katika kuzalisha kuliko kukaa vijiweni, kushinda kwenye mikutano ya kisiasa n.k Baada ya rais kutoa maelekezo kwa viongozi waandamizi mnaanza kukurupuka na kusema ooo mara rais ni Dikteta mpaka munaunda kundi lisilokuwa na kichwa wala miguu! HIVI MNGESHINDA 2015 MNGEPENDA KUTAWALA WATU WANAOSHINDA KTK MIKUTANO NA VIJIWE VYA KISIASA?

Kimsingi mambo ya kuongea ninayo mengi sana ila leo naishia hapa - UJUMBE

''MWACHENI RAIS WETU MHE. DKT. JOHN P. J. MAGUFULI ACHAPE KAZI ILI NCHI ISONGE MBELE KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI, KIJAMII, KITEKNOLOJIA NA KIUCHUMI''

Msakila M. Kabende
MWANAHARAKATI - NIPINGE KWA HOJA BILA KUFICHA JINA TUJADILIANE KWEUPE!
Mbona mumekazana Sana kumsifia mh Rais mnawasiwasi gani naye?wananchi ni watu wenye akili zao wanauona utendaji kazi wa mh rais,wanafahamu ni wapi mh rais anapofanya vizuri na ni wapi anapotakiwa kukosolewa kwa kuwa naye ni binadamu anayeweza kukosea.
 
Sikulelewa kutoa matusi - njoo ujenge hoja kiongozi (Tuwapime viongozi kwa hoja na ikiwezekana ongea humu nani kwako unamwona msafi ili tumchambuwe) - Hakuna rais awezaye kuvunja rekodi ya magufuli kwa sasa
 
[QUOTE="
Usitegemee kila mtu akubali unachoona wwe ni sahihi na kusifia unachodhani wwe kiko safi.
Acha watu wakosoe, wasifie ndiyo maendeleo isionekane kukosoa ni nongwa kwa hoja eti rais ni msafi kuliko hata waliokuwepo.[/QUOTE]

Mie sishangai watu kukosoa - nashangaa watu siku zote za mwaka kuwa wapingaji wa jambo linalotekelezwa na kiongozi fulani (iwe bungeni very radical, iwe kwenye majukwaa) - siku zingine mtu ona jambo analolifany mwenzako ni zuri)
 
HV mtoa mada unalipwa per day au??
Sina haja ya kulipwa - facts ndiyo zizungumze mkuu! JPM ni lulu ya nchi yetu (sasa namfananisha na rais wa Urguay - MJIKA)
 
Shida ya CCM kila kitu kinachong'aa mnadhani ni dhahabu. By the time wapinzani wanasugua na kugundua ni gold plated is too late. Mlishangilia mkuu wenu alivyoleta halafu mnashangilia anavyotumbua. Hapo ndio mwisho wa akili zenu. Hamna know how au vision ya kusonga mbele.
 
Jamaa kajilipua kwa kuandika Jina lake ili iwe rahisi mkulu kumpata
 
Jamaa kajilipua kwa kuandika Jina lake ili iwe rahisi mkulu kumpata

Sifikirii hayo - mkulima mzuri na msomi kama wewe tu! - Mnapopata kiongozi mzuri muungeni mkono ili kwa faida ya taifa hili na kizazi hiki tuendelee mbele kwa kasi kubwa. ''KWA HARAKA HUWEZI KUMFUKUZA DR SLAA KISHA UKAMKARIBISHA MZEE''
 
[QUOTE="
Usitegemee kila mtu akubali unachoona wwe ni sahihi na kusifia unachodhani wwe kiko safi.
Acha watu wakosoe, wasifie ndiyo maendeleo isionekane kukosoa ni nongwa kwa hoja eti rais ni msafi kuliko hata waliokuwepo.

Mie sishangai watu kukosoa - nashangaa watu siku zote za mwaka kuwa wapingaji wa jambo linalotekelezwa na kiongozi fulani (iwe bungeni very radical, iwe kwenye majukwaa) - siku zingine mtu ona jambo analolifany mwenzako ni zuri)[/QUOTE]
kwani kazi ya upinzani ni kusifia serikali?
 
Sifikirii hayo - mkulima mzuri na msomi kama wewe tu! - Mnapopata kiongozi mzuri muungeni mkono ili kwa faida ya taifa hili na kizazi hiki tuendelee mbele kwa kasi kubwa. ''KWA HARAKA HUWEZI KUMFUKUZA DR SLAA KISHA UKAMKARIBISHA MZEE''
Sasa huyo jamaa kama anajihamini kwanini hazuie wengine wasiongee, anahofia nini? Kwakweli mimi sitaki ujinga
 
Back
Top Bottom