Mnaoagiza magari nje mnapata wapi dola?

Mnaoagiza magari nje mnapata wapi dola?

Wakuu habari zenu.

Naomba kuuliza kwa wajuzi wa mambo hasa kwenye kufanya malipo kwenda nje ya nchi. Leo nimeshindwa kulipia gari Japan sababu kubwa ni dollar, niliienda NMB wakasema mwisho kuchange ni $100.

Nimeshindwa kuelewa, ina maana hata kama Pesa ipo kwa account yangu inakuwa ngumu kufanya payment? Hata kuexchange pesa juu kwa juu inakuwa shida?

Nilikuwa najua kupata noti ya dollar ndo kipengele, hata kwa Pesa iliyo kwa account kubadili kuwa dollar nayo ni kipengele???.

Nataka kulipia gari Japan, naombeni msaada bank ambayo haina MBAMBAMBA.
Jiulize mtu kama niffer anayesafiri kila day na kuleta mizigo ya milions anazipataje. Mjini hapa watu wanafanya biashara ya dollar fresh tu
 
Wakuu habari zenu.

Naomba kuuliza kwa wajuzi wa mambo hasa kwenye kufanya malipo kwenda nje ya nchi. Leo nimeshindwa kulipia gari Japan sababu kubwa ni dollar, niliienda NMB wakasema mwisho kuchange ni $100.

Nimeshindwa kuelewa, ina maana hata kama Pesa ipo kwa account yangu inakuwa ngumu kufanya payment? Hata kuexchange pesa juu kwa juu inakuwa shida?

Nilikuwa najua kupata noti ya dollar ndo kipengele, hata kwa Pesa iliyo kwa account kubadili kuwa dollar nayo ni kipengele???.

Nataka kulipia gari Japan, naombeni msaada bank ambayo haina MBAMBAMBA.
Kuna watu wanazo USD ila watakuuzia bei kubwa inaweza kufika 2900 mpaka 3000, Kama uko Dar nenda ofisi za befoward au SBT kuna namna wanaweza kukusaidia ila kuwa makini sana hela ni ngumu usitembee na cash kubwa mkononi.
 
Jaribu hata Equity mkuu.
Fungua account 2 ya Usd na Tshs, weka pesa kwenye Tshs sawa na pesa unayotaka transfer, halafu waambie wahamishie kwenye USD.

Inaweza kusaidia au jaribu kufika ofisi za beforward.
Ndomana beforward wanauza gari juu sana kumbe hii nayo ni sababu. Sijatumia beforward sababu gari zao za kawaida afu wanauza gharama sana.
 
Nyie ndo mnapigwa(Kuingizwa Town) vibaya mno!!Ivi kuagiza gari mpaka uwe na Dola? mi najua ukiwa na Mastercard na Visa card ukifanya Malipo kwa Tsh kuna exchange automatically hayo ya kuwa na dola mnatolea wapi wakuu au mimi ndo mshamba?
 
Back
Top Bottom