Mna deal vipi na machinga wanaoziba duka

pole sana mkuu hiki ni kisiki kizito na sio rahis kupata suluhisho haraka wakati kodi inaenda

Kuna namna kadhaa chagua itakayokufaa

1. kutengeneza hali ya kutegemeana kwa maana uwe unauza jumla wao wananunua kwako kwa kuwa wewe unafrem utakuwa nau mtaji na utaalam hivyo tafuta machimbo ya mzigo ya bei nzuri uwauzie

2. Kuuza na kutangaza kwa bei ya chini ili washindwe kushindana na wewe waondoke kwa maana uza jumla na rejareja kwa bei moja

3. njia isiyo rasmi ni kutumia fitna kwa serikali za mitaa na polisi kuwatoa ingawa hii ni ngumu na sio ustaarabu kumbuka na wao wanfamilia zinawategemea

Angalizo hao mara nyingi huwa kuna watu wamewakodisha maeneo haya fanya tafiti ujue nani ndio anakula hela yao udeal naye au ulipwe wewe kwa kuwa wako mbele yako

usikate tamaa bila shaka uko sehem nzuri ndio maana kuna vibanda nje pambana tu
 
Back
Top Bottom