Iba SIRI Hii ya biashara kutoka kwa Watoto wa Darasa la saba!..

Seif Mselem

JF-Expert Member
Oct 16, 2023
257
441
Tarehe 4 mwezi wa 10 mwaka 2022, mida ya saa moja na robo usiku nikiwa nyumbani Singida, Shelui! Nilikuwa nimemaliza kuoga muda si mrefu, nikatoka nje kidogo kupunga upepo, nikiwa na Peruzi Peruzi kwenye simu yangu kama vile wengi tunavyofanya. Kipindi nataka kuwasha data ili niingie mtandaoni, kama unavyojua, simu nyingi huwa zina calendar karibia na sehemu ya kuwashia data. Yaani, ukitaka kuwasha data moja kwa moja utaona na siku, tarehe, na mwezi husika kwenye simu yako. Basi na mimi ilikuwa hivyo hivyo. Niliona tarehe ya hiyo siku husika, meseji, emails na notifications zikiwa zinaingia baada ya kuwasha data.

Ile nataka kuingia WhatsApp ili niangalie nani kanitafuta nimjibu meseji, mara gafla likaja wazo, 'Hivi leo si tarehe 4 Jumanne? Kesho yake Jumatano darasa la saba wananza mitihani?' Sikuwa na uhakika. Ili kuhakikisha nikaita kijana mdogo jirani kanasoma darasa la nne, nikauliza, 'Eti nkupa kesho la saba wanaanza mitihani?' Kakajibu, 'Ndio, mjomba Seif.' Hapo hapo nikazima na data!

Nikakumbuka kwamba kuna wadogo zangu, wawili na anko wangu mmoja, kesho yake wanaanza mtihani asubuhi. Nikasema kimoyo moyo, itakuwa sio vizuri kama sitawaambia chochote hawa watoto kwa ajili ya kesho, kwasababu ni siku muhimu sana kwao! Kwasababu nilikuwa najua walipokuwa wanapenda kujisomea usiku, nikaenda moja kwa moja hadi kwa baba mdogo ambako ndiko wale wadogo zangu wanaishi na kupenda kujisomea.

Bahati nzuri nikawakuta wote wako pale mezani pamoja na mtoto mwingine wa jirani yao wanayemaliza nae la saba. Kiukweli nilikuwa sijui hata naenda kuwaambia nini kwasababu nilikuwa sijajipanga na nilishasahau kabisa kuwa wana mtihani. Ila kwa uzoefu nilionao nikawa nimepata pakaunzia. Ukweli ni kwamba wale watoto ni ndugu zangu kabisa, ila kwa bahati mbaya walikuwa wanaogopa sana kuongea na mimi, ilikuwa ni salamu moja tu kisha hao wanakula kona.

Binafsi sikujua shida ilikuwa nini hasa, ila nilikuwa nahisi ni kwasababu nimewazidi miaka mingi kwa umri, kwa hiyo ilinibidi kutoa ule woga wao kwanza na kujenga uhusiano mpya na wao ili wahisi hawaongei na adui bali ni ndugu na rafiki yao wa karibu. Niliwapigisha story kwa muda kama wa dakika 7 hivi, nikaona watoto hao wanaanza kuja, nyuso zao zikaanza kubadilika mara wakaanza kutabasamu na kucheka kabisa wakati nikiongea. Kimoyo moyo, hapo ndipo nilipokuwa napataka sasa.

Baada ya kuona tushakuwa marafiki, ilibidi niende kwenye lengo sasa. Lengo langu lilikuwa ni wale watoto wafanye vizuri kwenye mitihani ya kesho, ikiwezekana wapangiwe shule za vipaji. Kwa hiyo ilibidi nitumie mbinu moja hatari ya marketing! Nitakwambia hiyo mbinu inaitwaje baada ya muda sio mrefu.

Walikuwa wako wanne (4), yaani Abdul, Ahmed, Imrani, na Khalfani. Nikaanza kwa kuwauliza hivi, "Vipi kama mtu akitokea akawapa Tsh 350,000 sasahivi hapa mtaenda kununua nini?" Nilijua wataogopa kusema kwasababu hata wewe unafahamu kwamba kitu ambacho unakipenda wewe kwa mwingine kinaweza kuwa cha kijinga, hivyo hivyo na kwako. Na kwasababu unakisema mbele za wenzako wanaweza kukucheka na ukajisikia vibaya.

Kwa hiyo nikawatoa hofu kwa kuanza na mimi, nikasema nikipewa 350k nitaongezea kidogo halafu nitanunua simu. Lengo nilikuwa, nataka wanambie yale matamanio yao ya ndani kabisa ya moyoni. Baada ya kuwaambia hivyo, nikaona wakawa huru sasa kunambia na kusema mbele zao. Nakumbuka, walianza kutaja kulingana na umri wao mmoja baada ya mwingine huku nikiandika kwenye karatasi ndogo.

Abdul akasema, "Mimi nitanunua mifugo ya kufuga, ataanzisha duka la nguo, na mwisho atatoa sadaka msikitini." Ahmed akasema, "Nguo za kuvaa, vitabu, na sadaka." Imrani akasema, "Nguo za shule, ada, na sadaka." Khalfan akasema, "Laptop, nguo za kuvaa, na sadaka." For sure nilishangazwa sana, kwasababu hakuna mtu angejua walikuwa wanahitaji nini hasa toka moyoni. Kwa sababu nilikuwa nataka wapate matokeo mazuri na makubwa, basi nika waambia yoyote atakayefaulu kwenda shule ya kipaji maalumu (special school), nitampa vitu vyote hivyo hapo ambavyo amevisema plus nitampa nauli ya kuja Morogoro ninapoishi aje kusoma pre form one, huku nikiishi naye pale ninapoishi mimi.

Niliwapa ofa ambayo wasingeweza kuipata mahali popote pale, kwasababu ni ofa iliyokuwa inatimiza matamanio yao ya ndani kabisa ya moyo. Unadhani nini kilitokea? Wale watoto walibaki midomo wazi wakitamani siku zirudi nyuma wajiandae vizuri kwa ajili ya mtihani. Sijajua, ila lengo langu lilikuwa nataka wapate matokeo mazuri kwasababu ilikuwa ni muhimu kwao kwa wakati huo.

Na nashukuru Mungu hadi hapa ninapo kwambia wote wamefaulu kwenda form one. Kwahiyo ndivyo ilivyokuwa kuhusu hao wadogo zangu. Oh damn! Nilitaka kusahau kukupa ile mbinu ya marketing niliyokuahidi kukwambia. Okay, angalia hapa. Hiyo mbinu inaitwa "market backward approach." Usiangaike, utaelewa vizuri hapa chini. Twende.

Ukweli ni kwamba watu wengi wakitaka kuanza kufanya biashara huwa wanaanza kwa kutafuta bidhaa/huduma ya kuuza kwanza badala ya kutafuta kundi la watu wenye changamoto za kufanana, yaani kitaalamu tunaita "niche au starving crowd." Na kwenye hii mbinu huwa tunafanya hivi. Kabla ya kuwa na bidhaa/huduma ya kuuza, anza kwa kutafuta kikundi cha watu wenye changamoto za kufanana, yaani niche.

Baada ya hapo waulize ni vitu gani hasa vinawanyima usingizi usiku, kisha waulize tena, je wako tayari kulipia kiasi gani endapo utatatua changamoto yao? Ukishapata "pain point" zao, then unarudi kwenge drawing board yako, unaangalia ni aina gani ya ujuzi unahitaji kuwa nao ili uweze kuhudumia soko lako (niche). Baada ya hapo unaingia chimbo, unajinoa hadi uwe na uwezo wa kutatua hiyo changamoto inayowafanya wasilale, kisha unarudi sokoni tena kutoa huduma, wakati huo wewe ni mtaalamu tayari.

Njia rahisi ya kujua changamoto zao ni kufanya kitu kinaitwa "market research" (market research ni makala ya siku ingine). Kwa kufulisha tu, hicho ndicho nilichofanya kwa hawa wadogo zangu wanne. I hope umefunza kitu,

uwe na Jumatatu njema!
Gracias!

Seif Mselem
 
Una ujumbe mzuri sana Hakika Allah azidi kukupa moyo wa kutufundisha ila urefu wa mabandiko yako ni changamoto kubwa kwa wa Tanzania wengi wavivu kusoma hivo itapendeza kama utajitahidi kufupisha (summarise) kidogo iwe fupi fupi watu wengi wa some kwa wepesi
InshAllah Amini Dada Mwajuma. Nitajitahidi.
 
Back
Top Bottom