Mmoja Afariki, Wanne Walazwa Wakishindana Kunywa Pombe Moshi

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,065
23,947
Mtu mmoja amefariki dunia, huku wengine wanne wakinusurika kifo wakati wakishindana kunywa pombe kali aina ya 'Smart Gin', baada ya kuahidiwa kupewa mkate, sukari na Sh50,000 kwa atakayeshinda.

Tukio hilo limetokea Juni 8, 2023 katika kata ya Sanya Juu, wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro, baada ya watu hao kuahidiwa na mtu anayedaiwa kuwa mfanyabiashara wilayani humo, ambaye sasa ametoroka.

Inadaiwa kuwa mtu huyo aliwaahidi kuwapa zawadi hizo na mpaka mmoja anafariki walikuwa wameshakunywa chupa tano kati ya tisa zilizokuwa zikishindaniwa.

Hata hivyo, baada ya kumaliza kunywa chupa tano hali zao zilianza kuwa mbaya na wengine kupoteza fahamu ambapo baadaye waliokolewa kwa kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha kupata msaada wa dharura.

Mkuu wa wilaya ya Siha, Christopher Timbuka alimtaja aliyepoteza maisha kuwa ni Benson Mshiri, mkazi wa Kijiji cha Merad na kwamba waliolazwa hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na muda wowote wataruhusiwa kwenda majumbani.

Mwananchi
 
kuna dogo mmoja nilimpa burudani 3 amalize nimpe elfu 20.alimaliza ila hakulala siku hyo.hana hamu mpaka leo
Bora umpe mtihani kwamba hawezi kufanya kitu fulani afanye umpe hiyo hela au ashindwe kuliko kuchezea vitu vya hatari kama hivyo.

Hii nchi kila kitu fake unaweza kukuta hiyo burudani ni vya wale Wachagha wa Manzese wanavyochanganya na spirit kali ukauwa mtoto wa mtu ukabaki na lawama.
 
Back
Top Bottom