Afariki baada ya kushinda shindano la kunywa pombe kali

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,485
99,208
Hii imetokea huko Nchini Afrika Kusini ambapo Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30, amefariki dunia baada ya kumaliza chupa nzima ya pombe kali ya Jagermeister.

Tukio hilo limemkuta kijana huyo katika mashindano ya kunywa pombe, yaliyofanyika katika Mtaa wa Mashamba, Limpopo nchini Afrika Kusini.

Mkuu wa Polisi wa Limpopo, Motlafela Mojapelo amesema kijana huyo na wenzake walikuwa kwenye mashindano ya kunywa pombe kali, ambapo mshindi huyo aliahidiwa kupewa kiasi cha randi 200 za Afrika Kusini (takribani shilingi 27,000 za Kitanzania).

Hata hivyo alieleza kuwa marehemu alifanikiwa kumaliza chupa nzima ya pombe hiyo kali, lakini muda mfupi baadaye alianguka na kupoteza fahamu na kisha kupoteza maisha.

Nb: Nmeambatanisha na picha ya pombe iliyomtoa uhai mshindi wa shindano

Chanzo: mwananchi newspaper

58093dd589bbc0d260c4e97a6beea864.jpg
Screenshot_20220714-112329.jpg
 
View attachment 2289970View attachment 2289977
Hii ni whiskey kali mno wazungu wenyewe wanakunywa kwa shot ina ujazo wa lita 1 inauzwa 170,000
 
Back
Top Bottom