Mmoja adaiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa na polisi katika vurugu huko Tegeta, Rufiji

Kama kawa kama dawa,CHADEMA hawajafanya mikutano siku nyingi wamekosa pa kuua wameamua kuwafuata makwenu, hii ndo policcm bana
 
Hii inatokea mida hii huko Tegeta Dsm,wakati polisi wakifanya opetesheni ya kuondoa magari maeneo hayo,eti raia wanawazuia! matokeo yake risasi zmeshaleta madhara kwa nn msiwaache polisi wafanye kazi zao?

.........Kwa kweli kuzuia polisi kufanya kazi zao sio vema lakini... polisi wamejiwekaa doa kwa jamii katika kufanya kazi zao... wanapotumia nguvu kubwa bila ya sababu... kama swala ni kuondoa magari... hapo ilitakiwa elimu itumike kwa wahusika... waelimishwe... wapewe muda... mabavu hayasaidii na wala hayajengi ....... ni sifa mbaya kwa jamii.....
 
Hii inatokea mida hii huko Tegeta Dsm,wakati polisi wakifanya opetesheni ya kuondoa magari maeneo hayo,eti raia wanawazuia! matokeo yake risasi zmeshaleta madhara kwa nn msiwaache polisi wafanye kazi zao?
Kuna kitu kinaitwa "proportional" ,
Je nguvu waliotumia askari inalingana na nguvu ya madereva hao???
Kwa mdau yoyote anayejua haki za binadamu, hakuna sababu ya kutumia nguvu kubwa kupitiliza pale panapotokea mzozo baina ya askari na raiya.
Je raiya walikua wanatumia risasi za moto kupinga operesheni iyo??
Askari wamepiga risasi za nini mpaka wamemuua mtu aliyekua mbali na eneo la tukio(kwenye duka la magodoro)?.
Siungi mkono raiya kuzuia operesheni iliyokua inaendelea ila pia siungi mkono matumizi ya nguvu kubwa(risasi) yanayotumiwa na polisi dhidi ya raiya.
Watanzania wamezoea kupelekeshwa kama kondoo, ingekuwa ni Kenya tungesikia mengine mda huu.
 
Hiri ndiro jeshi ra polishhi;

Kisha Afande SELE atasema kuwa ameuawa na mlipuko toka kwa wananchi na siyo Risasi ya Polisi.

TANZANIA NAKULILIA.
 
pumba.... hivi unafurahia mauaji?? Mtu yuko dukani akifanya shopping, kosa lake liko wapi?
Moja kati ya kigezo bayana cha mtu mjinga ni kutoweza kuelewa " kwamba ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji kichwa". Ralphrider anajifanya kwamba yeye yuko katika kundi la wanaolindwa..uwezo wake wa kuelewa hamwezeshi kujua kesho atakua kama huyo kijana ambaye amepoteza maisha kwa sababu ya matumizi ya nguvu kuliko akili.
 
Kijana mmoja huko Tegeta amepigwa risasi ya moto na kufariki na wengine kujeruhiwa vibaya sana baada ya polisi kurusha risasi hiyo wakiwa kwenye operesheni ya kuondoa magari yanayopaki barabarani.

Kijana huyo alikuwa kwenye duka la magodoro akifanya manunuzi.

Chanzo: Redio One stereo(Renatus Mutabuzi) sasa hivi(saa 5 :20).

Siku hizi polisi wanaona raha sana kuua raia wasiokuwa na hatia. Hata kama kuna sintofahamu kati ya polisi na raia na raia hao hawana hata jiwe mkononi, akili za polisi kwa sasa ziko kwenye kupiga risasi za moto tu.

Wangekuwa na akili basi wangekuwa wanalenga miguuni lakini hawa polisi wetu wanalenga vichwani tu. Inaonekana huo ndio mtaala mpya wa mafunzo ya polisi siku hizi.
 
Sasa hivi kuna mtu kauwawa na polisi na watu wengine wamejeruhiwa, wasiwasi wagubikwa wasije wakasema kapigwa na kitu kizito, mwandishi Renatus wa Itv yupo eneo la tukio, juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa kinondoni ndg. Charles Kenyera zinaendelea
mwenye taarifa zaidi atujuze
nipo mbali sina picha.

Wana JF,

Where are we heading as a country? Why have we reached this stage of not valuing the right to life of our fellow citizens? Where have we gone wrong? Dont we know that the right to life is the right from which other rights depends? Why are we forgetting that every one is presumed to be innocent until proven guilty by a competent court of law?

As a country we need to hold responsible the individuals perpetrating such extra judicial killings (individual responsibility). If we do it, I am sure the members of the police force will hesitate carrying such brutal killings knowing that their fate, including their employment, will be in trouble. But the problem the country is facing is the absence of the person to "bell the cat", is it Mwema or Kikwete? Can Kikwete really make his brother in law (Mwema) responsible for the acts or omissions of Mwema and or his subordinates? Kikwete MUST go. The time is now
 
pumba.... hivi unafurahia mauaji?? Mtu yuko dukani akifanya shopping, kosa lake liko wapi?

Asante kwa matusi yako! ila uelewe kuwa mara zote siku hizi kumekuwa na kamtindo ka kupinga kali maagizo yanayotolewa na kusimamiwa na polisi, ili dhahama kama hii itokee mpate la kusema! kisa eti nguvu ya umma! we vp? mi sifurahii mauaji naomba unielewe,nachosema kwa nini watu wasitii sheria mara zote kuepusha vurugu?
 
Mkuu sibishani kabisa na wazo lako,lakini kwa nini kuwatunishia misuli? huoni mara zote anaeathirika ni yule asie na mamlaka? mwisho wa siku unapoteza uhai unaacha familia yako inateseka! kweli,wangepashwa kutumia risasi bandi lakini kwa nini tuwe tunawajaribu kila mara? why do have to come to that extent?!

Hata hizo risasi za bandia hazipaswi kutumiwa, pia kumtoa mtu uhai ni kosa ambalo linatakiwa lishuhulikiwe vema na kubadili approach ya polisi kuanzia mafunzo ya CCP mpaka mwenendo mzima kwa ujumla.
Nashindwa kuelewa tume mbalimbali zinazoundwa baada ya raiya kuuliwa na askari huwa zinatoa mapendekezo gani juu ya kutatua ukatili wa askari dhidi ya raiya??
 
.........Kwa kweli kuzuia
polisi kufanya kazi zao sio vema lakini... polisi wamejiwekaa doa kwa
jamii katika kufanya kazi zao... wanapotumia nguvu kubwa bila ya
sababu... kama swala ni kuondoa magari... hapo ilitakiwa elimu itumike
kwa wahusika... waelimishwe... wapewe muda... mabavu hayasaidii na wala
hayajengi ....... ni sifa mbaya kwa jamii.....

Kweli mkuu,ila siku hizi kuna wrong percetion kwa polisi! kila wafanyalo watu wanata kupima nguvu na uwezo wao! kweli kutumia risasi za moto ktk jambo kama hili ni ni Use of excessive force,sikatai! hatua zinaweza kuchukuliwa lakini ameshaathirika? kwa nini tusicomply na law and order? and then kama kuna complaints ni badae?
 
Mkuu sibishani kabisa na wazo lako,lakini kwa nini kuwatunishia misuli? huoni mara zote anaeathirika ni yule asie na mamlaka? mwisho wa siku unapoteza uhai unaacha familia yako inateseka! kweli,wangepashwa kutumia risasi bandi lakini kwa nini tuwe tunawajaribu kila mara? why do have to come to that extent?!

Sikiliza ndugu, polisi anayo mamlaka lakini haimaanishi yachukue haki yako. Mimi sidhani kama watu wanaweza kupinga endapo polisi wangefuata taratibu za kazi zao vyema. Hapo ukifuatilia, utagundua hilo zoezi lina walakini fulani na ndio maana watu wanaligomea.

Kuhusu kupata hasara, inategemea kwako hasara ni ipi. Kuna mtu anaishi kwa haki hiyo anayoona pollisi wanaiondosha na ndio maana anaipigania.

Kudhihirisha ujinga wa mawazo ya polisi kutumia nguvu, ona sasa aliyeuwawa alikuwa amesimama mbali kwenye duka la godoro. Je utawaonya na watanzania wasisimame kwenye maduka ya magodoro kwa kuwa polisi wana mamlaka?
 
Kuna kitu kinaitwa "proportional" ,
Je nguvu waliotumia askari inalingana na nguvu ya madereva hao???
Kwa mdau yoyote anayejua haki za binadamu, hakuna sababu ya kutumia nguvu kubwa kupitiliza pale panapotokea mzozo baina ya askari na raiya.
Je raiya walikua wanatumia risasi za moto kupinga operesheni iyo??
Askari wamepiga risasi za nini mpaka wamemuua mtu aliyekua mbali na eneo la tukio(kwenye duka la magodoro)?.
Siungi mkono raiya kuzuia operesheni iliyokua inaendelea ila pia siungi mkono matumizi ya nguvu kubwa(risasi) yanayotumiwa na polisi dhidi ya raiya.
Watanzania wamezoea kupelekeshwa kama kondoo, ingekuwa ni Kenya tungesikia mengine mda huu.
hivi unadhani hawa vijana na wazee wa ccp wanajua lolote juu ya hiyo red??? Ili kujua hiyo kitu inabidi mtu afikiri na hawa wenzetu kufikiri kabla ya kutenda kwao ni la mwisho kabisa
 
Asante kwa matusi yako! ila uelewe kuwa mara zote siku hizi kumekuwa na kamtindo ka kupinga kali maagizo yanayotolewa na kusimamiwa na polisi, ili dhahama kama hii itokee mpate la kusema! kisa eti nguvu ya umma! we vp? mi sifurahii mauaji naomba unielewe,nachosema kwa nini watu wasitii sheria mara zote kuepusha vurugu?

wanaoiba kura, meno ya tembo, madini, wanyamapori, pesa e.t.c wanatii sheria? Je wameshapigwa risasi?
 
Mkuu sibishani kabisa na wazo lako,lakini kwa nini kuwatunishia misuli? huoni mara zote anaeathirika ni yule asie na mamlaka? mwisho wa siku unapoteza uhai unaacha familia yako inateseka! kweli,wangepashwa kutumia risasi bandi lakini kwa nini tuwe tunawajaribu kila mara? why do have to come to that extent?!

Sasa unataka watu wapelekwe kama kondoo? Unaona polisi wako sahihi kutumia silaha za moto isipo lazima?
 
Back
Top Bottom