Mmoja adaiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa na polisi katika vurugu huko Tegeta, Rufiji

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,215
2,000
Kijana mmoja huko Tegeta amepigwa risasi ya moto na kujeruhiwa vibaya shavu na wengine kujeruhiwa vibaya sana baada ya polisi kurusha risasi hiyo wakiwa kwenye operesheni ya kuondoa magari yanayopaki barabarani.

Kijana huyo alikuwa kwenye duka la magodoro akifanya manunuzi.

Chanzo: Redio One stereo(Renatus Mutabuzi) sasa hivi(saa 5 :20).
Sasa hivi kuna mtu kauwawa na polisi na watu wengine wamejeruhiwa, wasiwasi wagubikwa wasije wakasema kapigwa na kitu kizito, mwandishi Renatus wa Itv yupo eneo la tukio, juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa kinondoni ndg. Charles Kenyera zinaendelea
mwenye taarifa zaidi atujuze
nipo mbali sina picha.source: Radio one./ capital

KITAIFA


Na Joseph Zablon Dar na Amini Yasini, Rufiji (email the author)

Posted Alhamisi,Novemba29 2012 saa 22:34 PM

KWA UFUPI
NI KATIKA VURUGU ZILIZOTOKEA TEGETA, IKWIRIRI, MMOJA HOI MUHIMBILI


POLISI wamewajeruhi watu watatu kwa mabomu, mmoja kati yao akiwa katika hali mbaya katika matukio mawili tofauti ya kusambaratisha mikusanyiko iliyotokea Tegeta, Dar es Salaam na Rufiji mkoani Pwani.


Aliyejeruhiwa vibaya ametambuliwa kuwa mkazi wa Tegeta, John Paul ambaye baada ya tukio hilo alipelekwa katika Hospitali ya Mwananyamala na baadaye Muhimbili.
Tukio la Tegeta lilitokea wakati polisi walipokuwa wakiwatawanya wananchi waliokuwa wakipinga operesheni ya kuwaondoa katika hifadhi ya barabara katika eneo hilo saa nne asubuhi baada ya wafanyakazi wa Kampuni ya Udalali ya
Mwankinga wakiwa na polisi waliyolikamata gari la mkazi mmoja wa eneo hilo.

Hali hiyo ilizua ubishi na baadaye vurugu baada ya wakazi hao kutaka gari hilo lisichukuliwe na polisi.


Vurugu hizo ziliwafanya polisi kutumia nguvu kuwatawanya wakazi hao, kazi ambayo hata hivyo, haikuwa rahisi kwani nao walikuwa wakijibu kwa kuwarushia mawe na fimbo, hali iliyodumu kwa saa kadhaa na kufanya eneo hilo kugeuka uwanja wa mapambano kusababisha maduka kufungwa na mali kuharibiwa.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Chales Kenyela alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kueleza kuwa, kijana huyo alijeruhiwa shavuni na kitu ambacho bado hakijafahamika na kupelekwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.
Kamanda Kenyela alisema kuwa, polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na taarifa zaidi zitatolewa baadaye. Alisema awali, wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa na polisi, walifika eneo hilo na kuanza operesheni ya kuondoa magari."Walipokamata gari la mmoja wa wakazi wa eneo hilo wananchi hao walipinga na kuanza kuwafanyia vurugu polisi ambao walijibu mapigo kwa kupiga mabomu ya machozi na kuwatawanya. Kijana huyo alionekana baadaye akiwa amejeruhiwa na kupelekwa Mwananyamala," alisema. Katibu wa Afya katika Hospitali ya Mwananyamala, Edwin Bisakala alithibitisha kupokewa kwa majeruhi huyo na kudai kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa alijeruhiwa kwa bomu.Bisakala alisema hali ya majeruhi huyo ilikuwa mbaya na uongozi wa hospitali ulilazimika kumpeleka Muhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
Mmoja wa mashuhuda wa vurugu hizo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisimulia jinsi eneo hilo lilivyokuwa: "Polisi wanarusha mabomu na wananchi wanawarushia mawe, ilikuwa tafrani kubwa hapa."Alisema hali hiyo iliwafanya polisi wajibu kwa kupiga risasi hewani na kufyatua mabomu ya machozi hali iliyozua taharuki na baada ya watu kutawanyika, kijana huyo alionekana akiwa ameanguka chini, huku damu zikimvuja.Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Eligaeshi alithibitisha kufikishwa kwa kijana huyo katika hospitali hiyo akimtaja kwa jina la John Massawe. Alisema alikuwa amejeruhiwa vibaya kichwani.Mabomu 22 Rufiji
Wilayani Rufiji, polisi walitumia mabomu 22 ya machozi kuwatawanya wananchi wa Kijiji cha Mgomba Kati waliozingira jengo la kufua umeme wakipinga hatua ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuondoa mashine mbili za kufua umeme bila wao kuwa na taarifa na kuzipeleka wilayani Liwale, Mkoa wa Lindi.Mwandishi wa habari aliyekuwapo eneo la tukio saa nne asubuhi alishuhudia umati mkubwa wa watu wakiwa katika eneo hilo wakipinga kuondolewa kwa mashine hizo.
Wananchi hao walisema licha ya kuwa na umeme unaotumia gesi ya Songosongo, jenereta hizo huwasaidia wakati umeme huo wa gesi unapokosekana huku wakisema hawakushirikishwa katika uhamishwaji huo.Askari wawili walifika katika eneo la tukio na kuwaamuru wananchi hao kuondoka katika eneo hilo bila mafanikio. Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya, polisi hao walikimbia huku wananchi wakiwa na mawe wakiwafukuza. Askari mmoja aliyekuwa na bomu la machozi alidandia pikipiki na kukimbia na kumuacha mwenzake ambaye alishambuliwa vibaya kwa mawe.Askari huyo aliyeachwa aliepuka kipigo baada ya kukimbilia katika nyumba moja ya msamaria mwema na kujificha.

Baadaye polisi wenye silaha waliwasili eneo la tukio na kuanza kufyatua mabomu mfululizo kuwasambaratisha wananchi hao waliokuwa wamelizunguka jengo hilo wakitaka gari ambalo linasadikiwa kuwa lilikodiwa kwa ajili kunyanyua mashine hizo liondoke.

Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Ikwiriri, Dk Idi Malinda alisema raia wawili na polisi mmoja aliyetambulika kwa jina la Ali walifikishwa hapo kwa matibabu baada ya vurugu hizo.

Aliwataja raia waliofikishwa hapo kuwa ni Seif Baja ambaye alijeruhiwa mkono wa kushoto, Hemedi Juma aliyeumia kichwani na askari Ali ambaye aliumia sehemu mbalimbali za mwili. Wakati hayo yakitokea katika eneo la tukio, wananchi wengine katikati ya Mji wa Ikwiriri walifunga Barabara Kuu ya Kibiti kwenda Lindi kwa zaidi ya saa moja na kusababisha usumbufu mkubwa kwa abiria waliokuwa wanatumia njia hiyo.

Hali ilitulia ilipofika saa 8:46 mchana baada ya polisi kuongeza nguvu kukabiliana na wananchi hao. Meneja wa Tanesco Tawi la Ikwiriri, Ladslaus Kalisa alisema mashine hizo mbili zilikuwa zikipelekwa Liwale kwa kuwa Ikwiriri ilipoanza kutumia umeme wa gesi, mashine hizo hazifanyi kazi.


Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu alilaani tukio hilo akisema Serikali iliamua kuzipeleka mashine hizo Liwale kwa nia njema ya kuwasaidia wananchi wenzao ambao wanakabiliwa na shida ya umeme.Babu aliwataka wananchi wa Ikwiriri kufuata taratibu za kisheria kudai kile wanachoamini akisema Wilaya ya Rufiji kuonekana kila mara kuwa chanzo cha matatizo siyo sifa njema.

Alisema mashine hizo haziendi kuuzwa kama ambavyo wananchi hao wanadai bali zinakwenda Liwale kuwasaidia watanzania kama wa Ikwiriri ambao kwa sasa wanauhakika wa Umeme wa gesi.
 

Ralphryder

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
4,616
2,000
Hii inatokea mida hii huko Tegeta Dsm,wakati polisi wakifanya opetesheni ya kuondoa magari maeneo hayo,eti raia wanawazuia! matokeo yake risasi zmeshaleta madhara kwa nn msiwaache polisi wafanye kazi zao?
 

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,180
1,195
Kuna taarifa kuwa huko Tegeta polisi wamewapiga risasi raia na kadhaa wamejeruhiwa na mmoja amepoteza maisha!
Kwa walioko Dar hebu tujuzeni kisa ni nini?
 

Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,189
2,000
Ralphryder sawa kuna kuwaachia polisi wafanye kazi zao ila kwa nini risasi za moto hakuna risasi za plastic kwa issue kama hiyo au ni mpaka mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya watu ambao hawana silaha yoyote
 
Last edited by a moderator:

Mgelukila

JF-Expert Member
May 27, 2012
224
0
Sasa hivi kuna mtu kauwawa na polisi na watu wengine wamejeruhiwa, wasiwasi wagubikwa wasije wakasema kapigwa na kitu kizito, mwandishi Renatus wa Itv yupo eneo la tukio, juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa kinondoni ndg. Charles Kenyera zinaendelea
mwenye taarifa zaidi atujuze
nipo mbali sina picha.

source: Radio one./ capital
 

Ralphryder

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
4,616
2,000
Ralphryder sawa kuna kuwaachia
polisi wafanye kazi zao ila kwa nini risasi za moto hakuna risasi za
plastic kwa issue kama hiyo au ni mpaka mabomu ya machozi na risasi za
moto kuwatawanya watu ambao hawana silaha yoyote

Mkuu sibishani kabisa na wazo lako,lakini kwa nini kuwatunishia misuli? huoni mara zote anaeathirika ni yule asie na mamlaka? mwisho wa siku unapoteza uhai unaacha familia yako inateseka! kweli,wangepashwa kutumia risasi bandi lakini kwa nini tuwe tunawajaribu kila mara? why do have to come to that extent?!
 
Last edited by a moderator:

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,027
2,000
Hii inatokea mida hii huko Tegeta Dsm,wakati polisi wakifanya opetesheni ya kuondoa magari maeneo hayo,eti raia wanawazuia! matokeo yake risasi zmeshaleta madhara kwa nn msiwaache polisi wafanye kazi zao?
Kwa nini magari yanaondolewa(kwa nguvu)? Hivi hayo magari yasingeweza kuondolewa bila kutumia nguvu?
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
53,052
2,000
pumba.... hivi unafurahia mauaji?? Mtu yuko dukani akifanya shopping, kosa lake liko wapi?
Heading yako imekaa kishabiki! umesha conclude kabisaa! hivi kwa nini raia wawavimbie polisi ambao wamepewa mamlaka kisheria? halafu unadhani bunduki wamepewa wapige nini? ni watu wakorofi wasiotii sheria! waacheni polisi wafanye kazi zao!
 

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,054
2,000
Kama sosi una na mimi pia nimeona breaking news itv kwanini unaandika ni tetesi?
Hao policeccm kuua watu ishakuwa fasheni sasa?
 

baba junior

Senior Member
Sep 21, 2012
143
170
Huyo Mwandishi anaripoti kuwa amefika duka la Magodoro na kushuhudia dimbwi kubwa la damu kufuatia kijana huyo kupigwa risasi.
Najiuliza hata kama walikuwa wanatawanya wanaopaki magari, kulikuwa na sababu gani za kufyatua risasi za moto?

thnx,bt cna cha kucomment mpaka sasa.
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
11,654
2,000
Mwaga Picha hata km una kasimu ka Mchina utasaidia waandishi sasa hivi watatujuza hatahivyo Thanx kwa taarifa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom