Ni kweli...daladala,Bodaboda,Malori mawili na Toyota Starlet ambayo watu wote wanne waliokuwemo wamefariki... moja ya ma-lorry lilikuwa limesheheni bia nyingi ambazo wakazi wa Kunduchi machimbo wamejikuta wamepata bia za bure na baadhi yao wameonekana wakiwa wamelewa chakariiiii... na Miili ya waliokuwa kwenye Starlet ilizamika kupelekwa kwenye Garage iliyo Kunduchi Mbuyuni ili iweze kutolewa ni ajali ya kutisha sana... sababu ni Trafiki Police zaidi ya 20 hivi waliosimamisha magari ovyo ovyo... na hii si mara ya kwanza.... Trafiki police hao waliponea chupuchupu kuuawa na wananchi wenye hasira kali... walikimbizwa na Mawe na chupa za bia huku wakimwacha,Trafiki kike aliyepigwa mawe na kuja kuokolewa na wanajeshi wa Jeshi lililopo jirani na eneo hilo... watu nane wamedhibitishwa kupoteza maisha...