Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Jamani mjue yale mananiliu ya pale mwembechai hayakutoshea pale magogoni!?yapo kitaa ndo mana ajali hazipungui
 
Yanazungumzwa mengi kuhusiana na chanzo cha ajali. Ila mimi kinachonichefua kwa polisi, kila basi au gari linapopata ajali, chanzo ni "Mwendo Mkali", "Uzembe". Kama mna kumbukumbu mwaka jana, magari aina ya toyota yalipata ajali sana na mwisho wakagundua chanzo chake kuwa ni mechanical problem, yaani hitilafu katika matengo ya mfumo wa breki na pedal. Hawakuzungumzia mwendo mkali wala uzembe. Walichowaamba wateja wao ni kuyarudisha magari yenye matatizo.

Ukitoka arusha au Dar au Mwanza kwenda Mbeya, Bukoba, Mtwara, Iringa au kwingineko, ni matuta tu ya kila design, ukubwa, mchongoko na muundo. Tuta zinakata tayari, zinalegeza vipuri na ikibidi kuvimega/kumeguka na uharibifu wa kila aina. Tairi ya gari inapata joto sana kutokana na msuguano na barabara. Hilo tayari lenye joto linapokutana na tuta za kila sampuli unategemea itabaki kwenye hali yake. Ajali ya basi la Sumry ilikuwa ni kupasuka kwa tayari. Hatujuia chanzo chake japo polisi walisema ni mwendo mkali. Ukikimbia sana unapasua tairi kweli. Inafika wakli inabidi tuwe na wakemia wa kufanya uchunguzi wa kisayansi kuliko kuropoka kunakofanywa na hawa jamaa zetu.
 
Muda wa dk 20 zilizopita imetokea ajali barabara ya mandela eneo la gereji ambapo costa ya gmboto imeigonga gari ndogo penye kizuizi cha barabara na kutumbukia mtaroni. Inasadikika wamefariki abiria watatu hivi. Mi nilikuwa napita tu (kwa taarifa sahihi ni kuwa ndani ya hilo gari kulikuwa na abiria wawili. Dereva ndiye aliyeumia vibaya maana aligongesha upande wake)
 
Of course hamna zaidi ya hilo na kuwahi abiria huwa hawafikirii abiria waliowabeba ndani ya gari
 
hamjakosea. Yalikuwa mabasi mawili. Lililopata ajali lilikuwa likiwahi vichwa relini wakati mwenzake aliwahi hapo gereji
 
hamjakosea. Yalikuwa mabasi mawili. Lililopata ajali lilikuwa likiwahi vichwa relini wakati mwenzake aliwahi hapo gereji

Daladala za Gombs an m.Rangi 3 zinapenda sana ligi kuwahi vichwa mbele
 
That is another tragedy! We are loosing innocent souls daily becuase or reckless drivers!!!
 
sababu kubwa ni kwamba hakuna madereva wanaofungwa kwa kusababisha ajali na vifo na hata sie vijana tukipata ajali tunakua wa kwanza kusaidia kumaliza kesi nje ya mstari
 
Muda wa dk 20 zilizopita imetokea ajali barabara ya mandela eneo la gereji ambapo costa ya gmboto imeigonga gari ndogo penye kizuizi cha barabara na kutumbukia mtaroni. Inasadikika wamefariki abiria watatu hivi. Mi nilikuwa napita tu
Hakuna aliyefariki isispokuwa dereva ameumia vibaya. kulikuwa na abiria wawili tu kwenye daladala, alikuwa akiwawahi wengine pale relini
 
Hakuna aliyefariki isispokuwa dereva ameumia vibaya. kulikuwa na abiria wawili tu kwenye daladala, alikuwa akiwawahi wengine pale relini

bora umeweka sawa maana palikuwa na umati na mi nilikuwa kasi kidogo, sasa kutokana na kauli za mashuhuda ndo nami nikapata hiyo taarifa hapo
 
Wajameni na sie abiria tusisubiri tumenusurika na tunaanza kutoa ushahidi tukiwa Muhimbili ooh dereva alikuwa akienda mbio!
ukondo, sijui ujinga, au tumelogwa, au malezi, inashangaza.
Nawaomba askari wa usalama barabarani kuwa ajali yeyote iliyosababishwa na mwendokasi, dereva na abiria Wawajibishwe wote!
Na kama sheria hiyo haipo mbunge aliye shapu apeleke hoja upesi.
si haki kupeana pole kwa uzembe!
 
Nilisha wahi kuwaambia madereva wengi IQ zao ni ndogo wengine wakanibishia - watu wanaingia kwenye kazi ya udereva baada ya mambo yote kushindikana sasa haya ndiyo matokeo yake. Reasoning ndogo mno kiasi cha kutojua thamani ya maisha yao wenyewe na abiria waliowabeba.


Bila kuwa na adhabu kali hata kufungiwa leseni zao maisha basi wataendelea kutubemenda.
 
Back
Top Bottom