Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Ni bahati mbaya tu lakini mabasi yanayoongoza kwa kukimbia ni HOOD wakuu, hawa jamaa ni noma. TBC1 wanaonyesha saizi ajali hiyo.
 
Matukio kama haya yapo kwa ajili ya utukufu na uwepo wa Mungu.
Ni kweli kabisa, kama unavyosema "Matukio kama haya yapo kwa ajili ya utukufu na uwepo wa Mungu." Hawa watu wameuawa ili Mungu atukuzwe. Kwa hiyo tusilaumu na kunung'unika kwa kukosoa kazi ya Mungu, bali tumtukuze Mungu kwa kuwaua hawa awapendao maana, tazama imeandikwa, ina thamani machoni pa Bwana mauti ya wacha Mungu wake.

Basi shukuruni kwa kila jambo, maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu. Mungu amefurahishwa na vifo hivi na japokuwa tunawapenda, yeye anawapenda zaidi, maana, tazama imeandikwa, Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu,na kazi yake haina makosa, wala hairekebishwi na binadamu yeyote.
 
Ajali za barabarani zinaendelea kugharim maisha ya watu. Leo asb bus la Ngorika likitokea Ar kwenda Dar likagonga hiace ya abiria ambayo ilikua inamkwepa mwendesha baiskeli. Takribani watu wasiopungua 8 wamefariki on the spot. Majeruhi ni wengi wamekimbizwa Mt Meru Hosp.

Rest in peace wote waliopoteza maisha kwenye hiyo ajali na majeruhi tunawaombea a quick recovery, mpone haraka, poleni wote mliopoteza ndugu, jamaa na marafiki kwenye hiyo ajali. We have to fight these road accidents because tutaisha
 
Tuache kulaumu na kunung'unika, tutakufuru mipango ya Mungu ya ajali, kazi ya Mungu haina makosa.
kunung'unika ni ubinadamu na sio kila kitu ni mpango wa Mungu bwana mengine yanaweza kuepukika au kutafutiwa ufumbuzi, i dont believe kwamba Mungu anavyotupenda hivi anapenda tufe namna hiyo kwa kweli, hata shetani nae mara nyingi anahusika. Pole wote mliofiwa na majeruhi tunawaombea kwa Mungu mpone haraka
 
Maeneo karibia USA RIVER, ukitoka Makumira kuna kadaraja kapo kabla ya kufika usa river. Hiace ni ya abiria inatokea arusha town inalekea Maji ya chai.

Tunawapa pole waliohusika wote, RIP to the dead
 
mh!poleni wafiwa.mi ningependa kuwakumbusha wale wote tunaosafiri tukumbuke kumwomba Mungu kabla ya kuanza safari.uzembe upo ni kweli.lakini kila siku yanaongelewa na bado madereva wanaendesha kwa mwendo wa kasi na sometimes wanakuwa wamelewa.but Mungu ni mwaminifu tukumbuke kumwomba kabla ya safari na atutuepusha na ajali.naomba kuwakilisha
 
Nchi za 1st world countries,hawana ajali nyingi za brbrn.ujue nini,wenzetu wana double road,sisi watanzania tunavitega uchumi vingi sana.na serekali yetu kama ingekuwa na viongozi waadilifu,kujenga double road,inawezekana kabisa.mfano,kuna fisadi mmoja wa epa,alitafuna fedha za kuweza kujenga brbr ya kiwango cha lami,toka mbeya hadi dsm.mwisho wa siku,jamaa kaachwa kiaina tu.hii nchi mi nahisi inalaana.na kamwe haitaisha umasikini.pumbavu kabisa.inaniuma sana,kuona ndugu zetu wanapoteza maisha kila kukicha.na hata hawa madereva.mi nawaona hodari sana,kwani kuendesha gari kwenye single road ni kazi sana.wenzetu walioendelea sio kama ni madereva wazuri,ila kwa kuwa wanabarabara nzuri.viongozi wetu acheni usanii ninyi,mmeanziasha mfumo mpya wa leseni.mwisho wa siku watu wanachakachua tu.kuanzia watu wa tra na matrafiq.watu wasiokuwa na sifa,wanapata lesseni kama kawaida.rushwa si mchezo.
 
Tuache kulaumu na kunung'unika, tutakufuru mipango ya Mungu ya ajali, kazi ya Mungu haina makosa.

...Sio tunachanganya mambo? Mungu wetu huyu wa Huruma anapenda watu wake wafe kwa maumivu makali ya kukatwa katwa na mabati ya magari??? Kama hii ni kazi ya Mungu wetu Mwenye Upendo na Huruma, Kazi ya Shetani ni Ipi???
 
04_11_4a9tm0.jpg

hiace yenyewe hii hapa wandugu
 
nyingine tena imetokea huko Mtwara watu wa3 wamepoteza maisha baada ya basi la Alhamdullilah kugongana uso kwa uso na gari dogo
Poleni wafiwa.
 
95% ya ajali za brbrn hapa kwetu zinatokana na mwendo kasi wa magari as we know brbr zetu ni sawa na kinywa cha bb kizee please madereva kuweni makini jamani vinginevo tutakua tunashughulika na misiba siku zote.MUNGU awape pumziko la milele Marehemu wote
AMIN​
 
Basi lililokuwa likitokea Masasi kwenda Mtwara limegongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya Land Cruser na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo akiwemo dereva wa gari hiyo ndogo, pia dereva wa basi amevunjika miguu yake na watu wengine wengi wamejeruhiwa vibaya. Aisee ajali hizi ni balaa...
Source:. ITV Breaking News at 1600hours.
 
RIP waliofariki, poleni majeruhi!

Magari yetu mengi ni mitumba! na hakuna mpango wa sisi wenyewe kutengeneza magari yetu yanayoendana na hali za barabara zetu.
 
Si yote kazi ya Mungu, kwa yeyote aliyewahi kufanya mitihani kupata leseni ya kuendesha gari nchi zilizoendelea atakubaliana nami kuwa ajali nyingi kwetu ni hasa uzembe,ulevi na hata kutojua, mwendo kasi pia katika barabara ambazo haziruhusu kwenda kasi. Kwa wastani nchi nyingi za ulaya highway ambako barabara zimetenganishwa(one way) mwendo ni kati ya 110-130 kmph na barabara za nje ya miji ambako unapishana na magari toka upande mwingine ambazo zinafanana na za huku kwetu mwendo hutakiwi kuzidi 90kmph hata pale unapo overtake gari jingine.
 
Mungu wetu huyu wa Huruma anapenda watu wake wafe kwa maumivu makali ya kukatwa katwa na mabati ya magari??? Kama hii ni kazi ya Mungu wetu
Nini kukatwa na bati, kama ni mipango ya Mungu hata misumari utapigiliwa.

Usikufuru kama haramia aliyemwambia Yesu mbona tunateseka na kupigwa nyundo misalabani hapa, kama ni mwana wa Mungu si utushushe?

Lakini Yesu machungu yalipomzidi alipoomba msaada akasema kama ni mapenzi yako basi endelea na mpango wako wa kutesa na kuua. Yesu alijua Mungu ndio anapanga. Mungu amewaua abiri hawa kwa kuwa japo sisi tunawapenda, Mungu anawapenda zaidi. Kwani Mungu angeshindwa kuepusha ajali hii? Kazi ya Mungu haina makosa.
 
17th April 2011
Watu watatu wamefariki dunia papo hapo na wengine 22 kujeruhiwa baada ya basi kugongana uso kwa uso na gari dogo mkoani Mtwara.
Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 10:20 kati eneo la kijiji cha Madango na Msapula, wilaya ya Mtwara ambapo magari hayo yaligongana baada ya dereva wa gari dogo kushindwa kuhimili usukani wakati akikata kona.
Katika ajali hiyo, dereva wa gari dogo aina ya Land Cruiser yenye namba T 436 AVR, Karim Kaile Shingu alifariki papo hapo.
Wengine waliofariki katika ajali hiyo ni mtoto Aneth Gabriel (mwezi mmoja) na kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 18 ambaye jina lake halijatambulika ambao walikuwa kwenye basi la Coaster ambalo namba yake haijafahamika.
Mwandishi wa gazeti hili ambaye alikuwepo eneo la tukio, alishuhudia maiti za watu hao zikiwa zimetupwa nje ya basi huku mwili wa dereva wa gari dogo ukiwa umenasa ndani ya gari baada ya gari hilo kupondeka vibaya.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, chanzo cha ajali hiyo imetokana na dereva wa gari dogo lililokuwa likitoka Mtwara kwenda Masasi kuendesha kwa kasi na hivyo kushindwa kulimudu gari wakati akikata kona kali na kusababisha kugongana na basi hilo lililokuwa likitoka Masasi kwenda Mtwara.
Alisema, mara baada ya tukio hilo wananchi wanaoshi katika vijiji hivyo walitokea kusaidia kunasua mwili wa dereva wa gari dogo kwa kuvunja mlango pamoja na kuwasaidia waliojeruhiwa kuwafikisha katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo aliyefahamika kwa jina la Dk. Mdoe, alithibitisha kupokea miili mitatu ya watu hao na majeruhi walipatiwa matibabu.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara hakuweza kupatikana kwenye simu yake ya mkononi kuthibitisha ajali hiyo.
Wakati huo huo, mwandishi Asraji Mvungi kutoka Arusha anaripoti kwamba idadi ya watu waliokufa katika ajali ya basi la Ngorika lililogongana na daladala katika eneo la Makumira wilayani Arumeru mkoani Arusha imeongezeka na kufikia kumi baada ya majeruhi mmoja kufariki akiwa hosipitalini.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye amemtaja marehemu kuwa ni Milka Bwanga (25), mkazi wa Usariver ambaye alikuwa miongoni mwa majeruhi wanne ambao hali zao zilikuwa mbaya.
Kamanda Andengenye amesema sasa hivi majeruhi waliobaki wakiwa wanaendelea na matibabu ni watatu, wawili wakiwa katika hospitali ya wilaya ya Arumeru iliyoko Tengeru na mmoja akiwa katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru. Ameongeza kuwa bado wanamshikilia dereva wa daladala iliyohusika katika ajali hiyo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Back
Top Bottom