Ni kweli uliyo yasema Gorika hukimbia sana linalotoka dar hufika Arusha saa saba na kutoka Arusha mpka dar ni wastani wa km 660...hivyo hukimbia wastani 94kph pata picha bado halijasimama kwenye kwenye vituo mbalimbali....Hakuna mtu ambae alikuwa hajui kuwa Ngorika ipo siku litauwa,nadhani hata police na vyombo vingine vya barabarani vilikuwa vinasubiri tu siku.ngorika ni kampuni ya mabasi ambayo tangu enzi ilikuwa inasifika kwa speed kali barabarani nahata baadhi ya askari wanajua hilo na walikuwa hata wakidiriki kusifia mwendo wa yale mabasi.binafsi nilishaapa kutopanda lile basi milele baada ya kuona jinsi linavyoenda na hata ukiangalia wahudumu wa bus lile kuanzia conductor hadi dereva ni mirungi tu kwa kwenda mbele,kwa ufupi ni mabasi ambayo yanaonekana matatizo yake yameanzia kwa tajiri wao.
nashauri waziri husika na viongozi wa jeshi la police usalama barabarani wajiuzulu kwa hili.maana tumeshachoka na ajali kila siku.
Abiria ndiyo tatizo kuu mkuu huo ndiyo ukweli....Ngorika inajulikana kwa mwendo kasi lakini watu ndiyo huligombania unategemea nini.....Jamani poleni sana.
Mimi nasema ukweli sisi wote kama wahusika wa tatizo hili wananchi, serikali na taasisi zote zinazohuiska hatujalipatia ufumbuzi janga hili.
Njia nzuri ya kupata ufumbuzi wa kudumu wa tatizo ni kuanza na kukubali kuwa hatujapata ufumbuzi. Tukatae propaganada wanazokuja nazo kina wakuu wa traffic kila kukicha kuwa leo tumepata dawa hii kesho ile na ajali zinaendelea kupoteza wapendwa wetu - kukubali kushindwa siyo afande mpinga, fanya hivyo na uombe msaada iitishwe mijadala ya kitaifa ili amkundi mbalimbali yajadili na kutoa mawazo juu ya jinsi ya kuondoa janga hili.
Ni mawazo yangu nasema kwa uchungu.
Pole sana mkuu, Nasikia dereva angeweza kupona kama wangechukua uamzi wa kumuokoa mapema kuliko kusubilia gari la kuja kunyanyua basi...Mfanyakazi mwenzetu amefiwa na baba yake
yey alikuwa kwenye Hiace
Poleni sana wafiwa wote
Mungu awaponye majeruhi wote
Dereva wa Ngorika amefariki
Tuache kulaumu na kunung'unika, tutakufuru mipango ya Mungu ya ajali, kazi ya Mungu haina makosa.
Matukio kama haya yapo kwa ajili ya utukufu na uwepo wa Mungu. Lakini mungu hachangui watu wakutokewa na matukio ila watu wenyewe kulingana na mazingira na akili zao. Ajali ipo tangi zamani kama njia mojawapo ya kutoa roho ya binadamu, lakini huwezi kuniambia mungu anamnywesha pombe dereva na kumuamru aendeshe gari ili apate ajali. NO. Dereva aliyelewa yy mwenyewe kajisababishia ajali kwa uzembe na wala siyo mungu wala kazi yake. Tusimsingizie mungu. Mungu katupa uchanguzi wa mema na mambaya, moto na maji, kifo na uzima, etc.Tuache kulaumu na kunung'unika, tutakufuru mipango ya Mungu ya ajali, kazi ya Mungu haina makosa.