Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Kwa mjibu wa breaking news ya ITV/Radio one ni kuwa Bus hilo limegonga lori na kupinduka.Wamejeruhiwa 27,kati ya hao 3 hali zao mbaya,Majeruhi wapo hospitalini Moro.
 
Duh huko moro kuna nini!!? Pole nyingi sana kwa majeruhi,wapone haraka.
 
Wadau,
Nimejuliwa kutokea kwa ajali nyingine leo asubuhi nje ya mji wa morogoro. Kwenye ajali hiyo (jina la basi bado kujulikana) hakuna aliyepoteza maisha yake lakini baadhi ya majerui walikuwa nanatibiwa hospitali ya morogoro. Inasemakana ajali ilitokea mwendo wa saa 3 asubuhi (24/03/2011) kati ya mikese na kingolowira. Hii ni ajali ya tatu kwa siku tatu mfululizo kuukumba mkoa wa morogoro. Nafuatlitia nitaleta habari zaidi kadri nitakazo zipata

Tuombe Mungu atunusuru na hizi ajali
 
huo mkoa si ndio walipokutana yule mtoto wa mkubwa na wale jamaa wanaopanga kumuua msaidizi wa Magufuli?
 
Kuna ajari imetokea morogoro lilokuwa likitokea Bukoba kwenda Dar, jana lililala msamvu sasa dereva anaonekana alilewa akawa anabadilishana usukani na konda wake. Majeruhi 24, na hakuna waliofariki ambao list yao nimeiona hapa hospitali ya mkoa. Majeruhi waliowengi wanaendelea vema ila kasoro watu 4. Mwanaume mmoja amepata severe head injury na mwanamke mmoja amekatika kiganja, na wengine wanapain tu. Tuwaombee majeruhi wapone haraka.
 
Mwendesha piki piki mmoja amekufa papo hapo alipogongana uso kwa uso na canter mjini Singida muda mfupi uliopita.
 
Hawa jamaa wa pikipiki wanalo mwaka huu, sijui ajali ya ngapi hii...
 
Watu kumi na watatu wamekufa na wengne kumi na watatu wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wanasafiria aina ya coaster lililokuwa linatokea moro kuja dar kugoganga na lori aina ya FUSO maeneo ya kibaha,source tymz fm
 
Hii imetokea lini? Leo au jana. RIP marehemu wote.
 
Ajali nyingine mbaya imetokea eneo la Kibaha saa nne usiku wa kuamkia leo. Watu 13 wamekufa na 13 wamejeruhiwa vibaya. Ajali imetokana na basi aina ya coaster toka Morogoro kwenda Dar ilipoivaa lorry semi trela kwa nyuma. Maiti na majeruhi wapo Tumbi hospital.SOURCE:Times Fm Radio. Jamani mbona maisha ya watu yanapukutika kinyama namna hii. Wenye habari zaidi mtujuze.
 
Ni kweli, hiyo ajari imetokea saa 4 usiku wa kuamukia leo. Haya magari (maroli)mabovu yanayoruhusiwa kutembea kwenye hizi barabara nyembamba inaonekana ndiyo yanasababisha ajari kwa kiasi kikubwa.
 
Inasikitisha sana...lakini
malori mengi ni mabovu
yanaharibika na kuegeshwa hovyohovyo
hakuna ishara wala taa zaidi ya majani ambayo usiku hayaonekani vema
mwendo kasi
ulevi
traffic wanakula rushwa
abiria wengi hawaelewi somo,ikitokea mmoja anamlalamikia dereva basi wengine watampinga au kwa uoga na ignorance watakaa kimya
Jamani mambo haya mpaka lini???
 
Duh inauma sana kupoteza maisha watu wengi kwa mtindo huu na ikizingatiwa kuwa wafiwa hawatapata fidia ya bima yoyote!
Magari mabovu,trafic wala rushwa,madereva wazembe na walevi,abiria waoga wasiojua haki zao na abiria washabikiao mwendo kasi,matuta kama milima barabarani highway...
Tz bado sana tuna kasoro nyingi cjui tutafanya nini..RIP na poleni wafiwa
 
RIP brodas and sistos!
Hizi ajali zote za wiki hili ni 100% uzembe!
Poleni ndugu wa wafiwa, maana hakuna la ziada tunachoweza kuwaambieni zaidi ya hilo.
 
Innalillah wainailaih rajiun, POLENI NDG WOTE MLIOFIKWA NA MSIBA HUU.
 
Jamani ajali hizi??

Poleni wafiwa wote mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu
 
RIP hv abiria huwa hawaoni dreva anapokimbiza gari?pia kwanini askari hawakagui haya magari?
 
Back
Top Bottom