Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Ni msiba mzito kwakweli; tumewapoteza ndugu zetu bila kutalajia, hatuna la kufanya zaidi ya kumwachia Mwenyezi Mungu.

Ila ninabaki na kushangaa juu ya utendaji kazi wa Askari wa barabarani. Ukiwa unasafiri wakati wa mchana kupitia barabara ya Dar/Mbeya/Songea utakutana na polisi wakifanya patrol(raod patrol)

Cha kujiuliza, patrol ya barabara ni kwa mchanu tu? Ukiangalia ajari iliyopelekea vifo vya wasanii wa taarabu usiku wa kuamukia jana, ilitokea baada ya basi dogo walilokuwa wanasafiria kuligonga kwa nyuma gari lililokuwa limepaki barabarani mara baada ya kuwa limearibika na bila kutoa ishara kwa magari yanayotokea nyuma au mbele kwa taazali zaidi.

Askari wa Patrol wangekuwa wako kazini, nina imani ajari kama hii usingetokea. Hivyo sioni haja ya askari kufanya patrol ya barabarani mchana tu kana kwamba barabara usiku uwa zinafungwa.
 
Ajali hapa Tanzania imekuwa kama jambo la kawaida, visingizio eti ajali haina kinga. Mimi kwangu naona si kweli, ajali zinaweza kuepukika au kupungua kwa kuwa na madereva wenye mafunzo sahihi na kuongeza adhabu kwa madereva wasiozingatia sheria za barabarani. Imefika wakati wa kulivalia njuga suala hili la ajali. Nafahamu kuwa serikali inaweza kulisimamia suala hili kikamilifu kama inavyosimamia masuala mengine nyeti.Serikali ipitie upya umri unaofaa kwa dereva wa gari la abiria.Vile vile ningependekeza kifaa kinachoonyesha kasi ya gari kiwekwe mahali pa wazi ili kila abiria aweze kujua kama dereva amezidisha kasi inayoruhusiwa kisheria. Naomba kuwasilisha!!!
 
inasikitisha kwa kweli,hasa baadhi ya mabasi yanayoenda mikoani,madereva sijui huwa wanakimbilia nini,mwendo wa kasi ajabu.labda akipata ajali rais,ndio watalichukulia serious
 
Jamani ajali nyingine barabara ya. Iringa Morogoro, basi la Upendo limegongana na lori dogo na watu watatu wanatajwa kufa papo hapo
 
Basi hilo lilikua limebeba askari Magereza wakitokea Mbeya kuelekea Dar es Slaam.

Imetokea leo saa 5.30 asubuhi katika eneo la N’gapa, mpakani mwa mikoa ya Morogoro na Iringa.
Marehemu wametajwa kuwa ni Ibrahim Chimvu, Pekile Mariot na mwanamke mmoja ambaye jina wala makazi yake havijaweza kutambulika.
 
Ajali tena Mikumi, watu 3 wamekufa papo hapo baada ya Canter kugongana uso kwa uso na bus la Luck Star ikiwa inakwepa mwendesha baiskel - RASIO1 STERIO
 
je KIKWETE ATATOA SALAMU ZA POLE KWA WAFIWA?

Nimesikia katoa salamu za pole kwa wasanii kwanini na hawa hasitoe pole?

Kwanini Rais anakimbila kutoa pole bila ya kuwawajibisha wausika wa barabarani??
 
Mh mikumi tena tuanhitaji kupafanyia maombezi pale
 
je KIKWETE ATATOA SALAMU ZA POLE KWA WAFIWA?

Nimesikia katoa salamu za pole kwa wasanii kwanini na hawa hasitoe pole?

Kwanini Rais anakimbila kutoa pole bila ya kuwawajibisha wausika wa barabarani??

Kama kawaida, utasikia ni "Mapenzi ya Mungu" nyingi kwa tulivyokosa aibu mbele ya umma wa dunia!!! Jana (5 Stars Taarab) wanasema wazi kuwa dereva ali over speed na walimuonya! Tatizo letu WaTZ kwa sasa imebakia <1% (less than) tunaoamini katika kufuata sheria na taratibu.
 
I think our driving skills are killing us. People drive defensively. I know the roads are bad, but there is a lot of things that can help us if we change our attitudes on the road. We should stop the Simile motokaa yangu attitude ( oh kuna watu hapa ambao hawatajua reference ya simile motokaa yangu. Lakini mashangazi namababa wakubwa watakuwa wanajua cheki nao LOL)
 
dah jaman kuna nin hapa mikumi, tuombe mungu atuepushe na balaa hili
 
five star na hili bus ni lucky star mh hii STAR!! ina nini?

Usiniambie kuwa kina Ghibuu, Zubeda, Majimshindo, NM Hafif n.k wawe makini sana wakati wa kurudi Kojani na ile Sea Star.... Ah, kumbe ile haipiti Mikumi, mantakhofu AMI zangu!
 
Back
Top Bottom