Maisha ya mwanadamu ni mafupi sana ,yapita kama umande jua lituapo,Mola na awe mfariji kwa ndugu ,jamaa, marafiki na wapenzi wote wa 5 star modern taarab
RIP marehemu wote na Mungu awape speedy recovery majeruhi!. Sijui mpaka lini ndio hawa wakubwa zetu watakuwa serious na sheria za barabarani tutakufa kila siku kwa sababu ya uzembe tu malori mabovu huwa yanapakiwa hovyo bila hata signs (reflectors) za kujulisha madereva arghhh! sick!
RIP wasanii wetu. Poleni sana wafiwa.
Hii habari nilipoisikia tu nikakumbuka thread ya Mkuu Majimoto - Biashara ya Uchawi. Ilitaja matukio kama haya yanavyopikwa/tengenezwa katika ulimwengu usioonekana. Imeniuma sana.
Tunaangamia, Mungu tunusuru.
Yaan nimeumia sana kwa vifo hivi hasa kifo cha Issa kijoti .da,nimeguswa sana,siamini ila inabidi nikubali ukwl kuwa mmoja wa wanamziki nimzimiaye hayupo duniani na bendi niipendayo ni km imekufa
Jana wanamziki wa 5 star modem taarabu wamepata ajali maeneo ya Moro na kusababisha umauti kwa wanamziki wapatao 13...mimi sio mpenzi wa taarabu kabisa na naichukia mno...lakini kama binadamu na mtanzania nazililia roho za ndugu na rafiki zetu tuliowapenda sana....nalo jiuliza
Nani alaumiwe kwa hizi ajali za mara kwa mara zinazo maliza roho za ndugu zetu?
Je hakuna njia kuwadhibiti madereva wazembe na wahuni wanaoendesha magari bila kuzingatia sheria za barabarani?
Bila kupata majibu ya maswali haya tutakufa kama kuku kila siku barabarani........
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.