WATU wawili wamekufa papo hapo na wengine 70 kujeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Mugumu wilayani Serengeti kwenda wilayani Bunda kuacha njia na kupinduka.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Mambo Masige, amesema ajali hiyo ilitokea jana saa 4:00 asubuhi, katika eneo la Chirige mjini Bunda.
Ajali hiyo imelihusisha basi la kampuni ya A.M Coach, aina ya Scania, lenye namba za usajili T. 740 AQD, mali ya Ahmed Mhamed, mkazi wa mjini Bunda.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk. Rainer Kapinga alisema waliokufa papo hapo ni
wanawake lakini majina yao hayajafahamika na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya teule ya Bunda.
Dk. Kapinga alisema majeruhi waliopokelewa hospitalini hapo ni 70 wanawake wakiwa ni 30 na wanaume 40 na kati yao, watoto wadogo wakiwa 12.
Majeruhi wengine watano wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza, kutokana na hali zao kuwa mbaya.
Dk. Kapina aliwataja baadhi ya majeruhi ambao wamepelekwa Bugando kuwa ni Fatuma Koleni, Anania Manyama na mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja tu la Pendo.
Aliwataja majeruhi ambao wamelazwa katika hospitali ya Bunda kuwa ni Fatuma Wambura (9), Wambura J. (6) na Happy Jonh, wakazi wa kisiwani Ghana, mkoani Kagera.
Wengine ni Stephen Henry (11) na Janet Henry (12), wote wakazi wa Kambarage mkoani Shinyanga, Guti Guti (7), mkazi wa Sanzate Bunda, Silora Charles (4), Judith Charles (7) na Agripiner Charles (11), wakazi wa Mugumu Serengeti.
Wengine ambao ni wakazi wa Mwanza na umri kwenye mabano ni Lusia Julius (11), Neema Samwel (12), Grace Maunda (6) na Bahati Maunda (15), Christina Magige (11), Daines Kunani (10), Pendo Suleimani (9) na Festo Amos (10) mkazi wa Busweru Mwanza.
Wengine ni Stephen William (8, Mugumu), Sesilia Alphan (16, Mwanza), Frenus Peter (14, mwanafunzi wa sekondari ya Maina), Robert Makindi (16, mwanafunzi wa Makoko Seminari), Horuman Amos (12, Busweru Mwanza) na Dominick Juma (18, Mugeta Bunda) na Simon Joseph (18, Bariadi Shinyanga).
Wengine ni Godfrey Rukaka (21), Tabu Chamriho (40), Chacha Aramali, Wambura Julius (20), Mgendi Stima, Igone Kihiri (32), Nyamhanga Mrimi (81), Mariamu Bira (20), Scholastika Mashauri (21), Mengi Sao (30), Grishon Namoni (22), Mango Maliganya (18), Bahati Guti (60), Mary Sumara (29) na Masatu Mang'ari (20), wote wakazi wa wilayani Bunda.
Wengine ni Mashaka Julius (22), Julius Masirori (52), Wambura Julius (20) na Martha Satuta (30), ambao wote ni wakazi wa Isenyi wilayani Serengeti. Wengine ni Hellena Mang'oa (19), Kichere Ngochoge (33), Asha Hassan (39), Theresia Rabani (46), Enos James (20), Samson James (23) na Emilliana Charles (27), ambao wote ni wakazi wa Mugumu wilayani Serengeti.
Wengine na umri na makao yao kwenye mabano ni pamoja na Buyugu Nchege (43, Sengerema), Chacha Maseke (22, Igunga Tabora), Mkula Mashauri (25, Sengerema), Raphael Sakenge (75, Ngasamo Magu) na Christopher Malongo Bukani (62, Kwimba Mwanza).
Wengine ni Daud Nomolomo (42, Sengerema Mwanza), Michael Ezekiah (35, Iramba Singida), Nyambesa Sarora (30, Itembiri Serengeti), Yohana Semakweli (33 Butimba Mwanza), Mary John (45, Kambarage Shinyanga) na Amos Makanga (30, Busweru Mwanza).
Majina ya majeruhi wengine hayakupatikana mara moja kutokana na kuwa kwenye vyumba vya upasuaji.
HabariLeo | Wawili wafa katika ajali, 70 waliojeruhiwa watajwa