Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

mwafrika bado anaamini ajali zinasababishwa na kafara na mungu, unadhani hapo tatizo hili litakwisha lini?

huyo mungu tunayemwomba awajalie afya njema majeruhi kama ana uwezo huo si angewaepushia majeruhi ajali in the first place? hata Zinjatropus hakuwa na theory senseless namna hii
Hiyo yenye red he!
 
Poleni sana wafiwa na majeruhi.
Uzembe huu wa madereva mpaka lini jamani?
 
Waliofariki ajali ya Sumry watambuliwa Na John Nditi, Morogoro WATU saba kati ya nane
waliofariki katika ajali ya basi la Sumry iliyotokea kwenye barabara kuu ya Morogoro-Iringa juzi, katika Kijiji cha Masimba, wametambuliwa na ndugu zao na miili yao kuchukuliwa.

Ajali hiyo ilitokea eneo hilo katika Tarafa ya Mikumi, wilayani Kilosa saa 9 alasiri baada ya kugongana na lori aina ya Fuso mali ya Kampuni ya kutengeneza pipi ya Ivory lilipokuwa likitokea mkoani Iringa kwenda Dar es Salaam juzi.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoa wa Morogoro, Ibrahim Mwamakula alithibitisha kutambuliwa kwa maiti hao na kuchukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya maziko katika maeneo mbalimbali.

Alisema ajali hiyo ilihusisha basi hilo aina ya Nissan lenye namba T333 BCX lililokuwa likitokea mkoani Dar es Salaam kwenda Iringa na lori hilo aina ya Fuso lenye namba T 317 ASR.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, maiti waliotambuliwa ni Abubakar Laiser ( 25) ambaye ni Ofisa Masoko na mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, Mariam Jaha ( 25) Mhasibu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Iringa, Mboko Anyasime (31) Ofisa wa Mifugo na mkazi wa Iringa.

Wengine ni Saddiq Lyimo ambaye ni mtumishi wa Bohari ya Taifa ya Madawa (MSD) mkazi wa Dar es Salaam, Happy Alfred Mwakonjombe (15) Mkazi wa Iringa na Vicent Mrema (35) mfanyabiashara na Mkazi wa Kimara Dar es Salaam.

Wengine ni Doris Lwungo ( 24) mkazi wa Ipogoro mkoani Iringa na Martin Cassian ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Idiogoya ya mjini Iringa.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo mwili wa Martin Cassian bado umehifadhiwa chumba cha maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kutokana kukosa ndugu wa kuutambua na kuthibitisha.

Majeruhi wote 21 waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya St Kizito mjini Mikimu waliruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupatiwa matibabu na kupata nafuu.
 
RIP ee mungu wangu. ajali hizi zitaisha lini jamani?? This country bwana!!
 
http://1.bp.blogspot.com/_YaKHJFAZ_oc/TTB8hXeZwoI/AAAAAAAAPGM/1bG52YTf-F0/s1600/IMG_0148.JPG

http://2.bp.blogspot.com/_YaKHJFAZ_oc/TTB8hLlHzjI/AAAAAAAAPGE/lG3y_EgDFk4/s1600/IMG_0145.JPG

http://3.bp.blogspot.com/_YaKHJFAZ_oc/TTB8g9L5dmI/AAAAAAAAPF8/ciEBtC6_bok/s1600/IMG_0140.JPG

http://3.bp.blogspot.com/_YaKHJFAZ_oc/TTB8gmByHNI/AAAAAAAAPF0/O0hpM-EeV8E/s1600/IMG_0142.JPG

WATU wanne wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 8 kujeruhiwa vibaya baada ya costa yenye namba za usajili T 885 BNQ mali ya Another G ' kugongwa na lori wakati akishusha abiria .

Ajali hiyo mbaya ambayo ni ajali ya kwanza kutokea mkoani Iringa kwa mwaka huu 2011 na ajali ya pili mbaya kutokea nchini ikiwemo ajali ya basi la Sumry kugongana na Lori Mikumi mkoano Morogoro na kusababisha vifo vya watu 8 na kujeruhi 22 imetokea leo majira ya saa 10 jioni katika kijiji cha Tangangozi wilaya ya Iringa vijijini barabara kuu ya Iringa- Mbeya.

Wakizungumza na mtandao wa Francis Godwin ni mzee wa matukio daima eneo la tukio majeruhi wa ajali hiyo wamesema kuwa wakati ajali hiyo inatokea costa hiyo ilikuwa imesimama kando ya barabara eneo hilo kwa ajili ya kushusha abiria na ndipo lori hilo lilipoivaa costa hiyo ubavuni na kuigonga vibaya na kupelekea nusu ya costa hiyo kuchanwa vibaya na lori hilo.

Walisema kuwa katika ajali hiyo abiria watatu wa costa hiyo walikufa papo hapo huku mwananchi mmoja wa aeneo hilo ambaye alikuwa akitembea kwa miguu kugongwa na lori hilo ambalo lilikuwa katika mwenda wa kasi .


Hata hivyo alisema kuwa mwendo kasi wa lori hilo ndio chanzo cha ajali hiyo na kuwa inaonyesha dereva wa lori hilo alikuwa amesinzia na ndio sababu ya kuigonga costa hiyo ambayo ndani ilikuwa na abiria zaidi ya 30 ambao walikuwa wakielekea Njombe.

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa kupitia kikosi cha usalama barabarani limethibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kuwa idadi kamili ya waliokufa itafahamika baada ya kufika hospitali ya mkoa wa Iringa alisema mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa (RTO) Kedmund Mnubi ambaye alifika eneo la tukio.

Wakati huo huo polisi Iringa imeshangazwa na taarifa zisizo za uhakika zilizotolewa na moja kati ya vituo maarufu nchini ambacho kimekuwa kikitangaza breakingnews mbali mbali baada ya kudai kuwa lori hilo limegonja Hiace na lori lilikuwa lilikuwa likienda Zambia wakati ukweli ni kuwa lori hilo lilikuwa limebeba ndizi likitokea mkoani Mbeya.

Francis Godwin ni mzee wa matukio daima
 
WATU watatu wamefariki dunia mkoani Kilimanjaro katika matukio matatu tofauti, likiwemo kuuawa la mmoja kuchomwa kisu kutokana na wivu wa mapenzi, na wengine kupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani.

Gari aina ya Nissan lilimgonga mwendesha pikipiki na kufa hapo hapo, lingine aina Toyota corolla lilipinduka na kusababisha kifo cha abiria mmoja.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Hapa, Yusuf Ilembo alisema Januari 13, mwaka huu, saa 4:00 asubuhi maeneo ya Kilema pofo Rongoma vunjo Wilaya ya Moshi vijijini, Philip Assey (35) aliuwawa kwa kuchomwa kisu chini ya mbavu, mkono wa kulia na Godfrey Baltazary (26).


Kamanda alisema chanzo cha ugomvi huo ni wivu wa mapenzi na walikuwa wakigombania mwanamke mmoja ambaye(jina lake limehifadhiwa).

Katika tukio lingine, lilitokea Januari 14 saa 1:30 asubuhi maeneo ya barabara ya viwandani Manispaa ya Moshi, gari aina ya Nissan lilimgonga mwendesha pikipiki Faustin Saria (25) na kufariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitali ya KCMC.

Januari 13, mwaka huu saa 07:00 mchana maeneo ya Kifaru Kileo, Wilaya ya Mwanga mkoani hapa gari aina ya Toyota Corolla liliacha njia na kupinduka wakati akijaribu kukwepa wanafunzi wa Shule ya Msingi Kifaru na kusababisha kifo cha Samweli Malamsha (42).

Kamanda alimtaja aliejeruhiwa kuwa ni Emmy Samweli(14) pamoja na dereva na wanaendelea na matibabu katika hospitali ya KCMC na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa Mawenzi na chazo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva.
 
Watu 4 wamekufa,8 wamejeruhiwa baada ya lori lililokuwa linaenda Zambia kugonga Hiace huko Tanangozi nje ya Iringa.
 
Hizi ajali zitaisha lini jamani?Hapo utakuta mtu kaletewa leseni nyumbani wakati hata kuendesha gari hajui ,akiweza kulliweka barabarani basi huitwa dereva bila kujua sheria za barabarani.Maafisa usalama barabarani nao ndio chanzo cha ajali hizi kwa kuendekeza mlungula hata pale wanapoona kuna hatari mbele au dereva hakidhi vigezo vya kuwa barabarani.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi
 
Hizi ajali zitaisha lini jamani?Hapo utakuta mtu kaletewa leseni nyumbani wakati hata kuendesha gari hajui ,akiweza kulliweka barabarani basi huitwa dereva bila kujua sheria za barabarani.Maafisa usalama barabarani nao ndio chanzo cha ajali hizi kwa kuendekeza mlungula hata pale wanapoona kuna hatari mbele au dereva hakidhi vigezo vya kuwa barabarani.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi
Dreva wa loli alikua amelala loli likiwa kwenye mwendo mkali
 
Watu 4 wamekufa,8 wamejeruhiwa baada ya lori lililokuwa linaenda Zambia kugonga Hiace huko Tanangozi nje ya Iringa.

Sio kweli mkuu unapotosha watu
Sio Hiace ni Kosta ya Another G na Lori sio kweli lilikuwa linaenda Zambia bali lilikuwa linaenda Dar
 
Sio kweli mkuu unapotosha watu
Sio Hiace ni Kosta ya Another G na Lori sio kweli lilikuwa linaenda Zambia bali lilikuwa linaenda Dar
Asanteni nyote kwa kutujuza!
Taarifa kama hizi huwa zinaanza na porojo nyingi, mwisho ukweli utajulikana!
 
IMG_0148.JPG


Hii Ndo kosta ilikuwa imepaki inachukua abiria

IMG_0142.JPG


Na hili ni lori lilosababisha ajali
 
Asanteni nyote kwa kutujuza!
Taarifa kama hizi huwa zinaanza na porojo nyingi, mwisho ukweli utajulikana!

Kweli mkuu lakini Radio One kupitia breaking news walipotosha ukweli halisi angalia picha hapo juu.
 
Back
Top Bottom