Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Hilo ni uzembe wa daywaka na sio suala la katiba wala la kisiasa. Lakini haina maana kwamba ndio tusiumie kusikia maana uhai wa ndugu zetu umetoka hapo. Sielewi kwa nini wengine wanachomekea mistari ya siasa moja kwa moja nadhani wanataka kuharibu mada. Sawa Liz Senior? msiba hautaniwi, ni vizuri ukajifunza kuheshimu hilo. Hata wewe yaweza kukukuta. Hata adui akifa unasikitika lau kidogo kuonyesha unajali utu wa wenzio.

Poleni mliofikwa na majonzi hayo. Kama polisi wangekuwa makini ndiyo masuala ambayo walihitajika kushughulikia kwa makini badala ya kukimbizana na wapinzani wa CCM, kwa kutokuwapo kwenye responsibility zao za kimsingi maafa kadha wa kadha hutokea.
 
Baada ya kufuatilia, kati ya watu watatu waliosadikiwa kufa, wawili walisalimika kwani walikuwa chini ya gari na watu walifanikiwa kuwatoa. Mtu wa tatu ambaye alikuwa ni mmachinga ndiye aliyejeruhiwa vibaya na alikimbizwa hospitalini, japo hali yake ilikuwa mbaya sana. Kondakta aliye sababisha mahafa hayo aliokolewa na polisi baada ya watu kutaka kumpinga. Polisi walimpeleka kituo cha polisi Arusha. Pia Gari na dreva wake amepelekwa kituoni.
 
Tunashukuru kwa taarifa mkuu ila hiyo AVATAR mheshimiwa angalia uwezekano wa kuibadilisha
 
Watu wawili wamekufa papo papo na wengine zaidi ya 70, wamejeruhiwa vibaya, baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Mugumu wilayani Serengeti, kuelekea wilayani Bunda, mkoani Mara kuacha njia na kuanguka.




Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Mambo Masige, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, iliyotokea jana majira ya saa 4:00 asubuhi, katika eneo la Chirige, mjini Bunda.
Ajali hiyo ililihusisha basi la kampuni ya A.M Coach aina ya Scania namba T. 740 AQD, mali ya Ahmed Mhamed, mkazi wa mjini Bunda.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk. Rainer Kapinga, alisema watu wawili ambao wote ni wanawake walikufa papo hapo na kwamba majina yao bado hayajafahamika, na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya DDH-Bunda.
Dk. Kapinga alisema majeruhi waliopokelewa hospitalini hapo ni zaidi ya 70, ambapo 12 kati yao ni watoto wadogo, na kwamba 30 ni wanawake na 40 ni wanaume.
Alisema majeruhi wengine watano wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, kutokana na hali zao kuwa mbaya.
Dk. Kapinga aliwataja baadhi ya majeruhi ambao wamepelekwa Bugando kuwa ni Fatuma Koleni, Anania Manyama na mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la Pendo.
Majeruhi ambao wamelazwa katika Hospitali ya DDH-Bunda ni Fatuma J. Wambura (9), Wambura J. (6) na Happy John, wakazi wa kisiwani Ghana, mkoani Kagera.
Wengine ni Stephen Henry (11) na Janet Henry (12), wote wakazi wa Kambarage mkoani Shinyanga, Guti Guti (7), mkazi wa Sanzate Bunda, Silora Chalres (4), Judith Charles (7) na Agripiner Charles (11), wakazi wa Mugumu Serengeti.
Wengine ni Lusia Julius (11, Mwanza), Neema Samwel (12, Mwanza), Grace Maunda (6) na Bahati Maunda (15 Mugumu), Chrisitina Magige (11, Mwanza) Daines Kunani (10, Mwanza), Pendo Suleimani (9, Mwanza) na Festo Amos (10, Busweru Mwanza).
Wengine ni Stephen William (8, Mugumu), Sesilia Alphan (16, Mwanza), Frenus Peter (14, mwanafunzi wa sekondari ya Maina), Robert Makindi (16, mwanafunzi wa Makoko Seminari), Horuman Amos (12, Busweru Mwanza) na Dominick Juma (18, Mugeta, Bunda) na Simon Joseph (18, Bariadi, Shinyanga).
Wengine ni Godfrey Rukaka (21), Tabu Chamriho (40), Chacha Aramali, Wambura Julius (20), Mgendi Stima, Igone Kihiri (32), Nyamhanga Mrimi (81), Mariamu Bira (20), Scholastika Mashauri (21), Mengi Sao (30), Grishon Namoni (22), Mango Maliganya (18), Bahati Guti (60), Mary Sumara (29) na Masatu Mang'ari (20), wote wakazi wa wilayani Bunda.
Wengine ni Mashaka Julius (22), Julius Masirori (52), Wambura Julius (20) na Martha Satuta (30), wakazi wa Isenyi wilayani Serengeti.
Wengine ni Hellena Mang'oa (19), Kichere Ngochoge (33), Asha Hassan (39), Theresia Rabani (46), Enos James (20), Samson James (23) na Emilliana Charles (27), ambao wote ni wakazi wa Mugumu wilayani Serengeti.
Wengine ni Buyugu Nchege (43, Sengerema), Agnes na Chacha Maseke (22, Igunga Tabora), Mkula Mashauri (25, Sengerema), Raphael Sakenge (75, Ngasamo Magu) na Christopher Malongo Bukani (62, Kwimba, Mwanza).
Wengine ni Daud Nomolomo (42, Sengerema Mwanza), Maico Ezekiah (35, Iramba, Singida), Nyambesa Sarora (30, Itembiri, Serengeti), Yohana Semakweli (33 Butimba Mwanza), Mary John (45, Kambarage Shinyanga) na Amos Makanga (30, Busweru, Mwanza).
Majina ya majeruhi wengine hayakupatikana mara moja kutokana na kuwa kwenye vyumba vya upasuaji.
Watu walioshuhudia ajali hiyo wamesema walishutukia gari hilo linakosa mwelekeo na kugonga nguzo ya umeme na kisha kupinduka, kabla ya kumpitia mwanamke mmoja aliyekuwa akitembea njiani na kufa papo hapo.




CHANZO: NIPASHE
 
WATU wanane wamefariki dunia papo hapo na wengine ishirini kujeruhiwa katika eneo la Mikumi, wilayani Kilosa, mkoani Morogoro, baada ya basi walilokuwa wakisafiria la Kampuni ya Sumry kugongana uso kwa uso na lori.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 9 mchana katika eneo la Kijiji cha Msimba, barabara kuu ya Morogoro na Iringa na kuhusisha basi la Kampuni ya Sumry lenye namba za usajili T 333 BCX, Nissan, na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 317 ASR.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani hapa, Ibrahimu Mwamakula, amesema kuwa majeruhi wa ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizito Mikumi, wilayani Kilosa.

Alisema kuwa majeruhi wa ajali hiyo bado hawajafahamika majina yao pamoja na maiti hazijatambulika na kwamba zinapelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kuhifadhiwa na kutambuliwa na ndugu zao.

Imedaiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa gari la Sumry lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Iringa.
 
Eee Mwenyezi mungu zilaze pema peponi roho za marehem pia wajalia afya njema majeruhi wote.:director::director:
 
Eee Mwenyezi mungu zilaze pema peponi roho za marehem pia wajalia afya njema majeruhi wote

Miezi hii ni yakutoa kafara,
mwafrika bado anaamini ajali zinasababishwa na kafara na mungu, unadhani hapo tatizo hili litakwisha lini?

huyo mungu tunayemwomba awajalie afya njema majeruhi kama ana uwezo huo si angewaepushia majeruhi ajali in the first place? hata Zinjatropus hakuwa na theory senseless namna hii
 
Back
Top Bottom