Mlipuko watokea Ubungo-TANESCO, umeme wakatika!

Hii nchi inamikasa hii jamaani!! National Grid siyo kitu kidogo, wahujumu uchumi wote mara nyingi midomo inamezea mate hiyo kitu itokee ili wale kiulaini. Sasa hii katika katika ya mara kwa mara watu hatuoni wakiwajibishwa ndo nini. Ndiyo maana katiba mpya itapunguza watu ujasiri wa kuwa na dharau kwenye vitu vyenye manufaa kwa taifa zima kama hili la umeme. Hizi ni dharau, hebu fikiria watu wangapi wanaweza kupoteza maisha, au kiasi gani cha pesa kinapotea kwa ajili ya kukosekana umeme watu/viongozi kimyaa wala hakuna hata kusema chochote?

Mapinduzi yanahitajika, siyo kwa hawa madingi ni sisi vijana kuamua na kuwaomba wakae pembeni wasubiri kushauri tu hawataki wanalazimishwa.
 
mie niko kilimanjaro maeneo ya KCMC na mida ya sa kumi na dk 40 hivi gafla nao umeme ukakatika nadhani ni issue hiyo hiyo mlipuko Ubungo ndo sababu, kazi tunayo,
Nafikiri Ngeleja aliazimisha tanesco kuzalisha umeme kwa lazima hata kama uwezo wa machines silizopo ni mdogo ili kuplease wabunge wasimwashie moto tena, sasa atakiona cha moto, ndo kimenuka!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! kweli
 
Nilikua pale ubungo kwy mataa wakati transfomer inalipuka ghafula nikawaza unaweza kutokea moto mkubwa sana kutokana na Songas kuwa karibu nilizima gari mikatoka nje nataka nikimbie bahati nzuri traffic akaruhusu gari za upande wetu duh!!

Pole mkuu
 
Mafisadi kazini, wabongo mtakomaa awamu hii, walizotengeneza kupitia matatizo ya umeme hazijatosha.
 
Mods badilisha Title hiyo...
Moto umelipuka kutoka katika transfoma ya msongo wa 220/132kV iliyopo katika Gridi ya Taifa na siyo Songas. Vituo hivyo viwili yaani Songas na Gridi ya Taifa vinatenganishwa na barabara ya Mandela. Ni vitu viwili tofauti hivyo.
 
Nilikuwepo pale kwa muda wa dk 35, hakuna cha fire wala nini, ingawa upande wa pili wa Songas kulikuwa na zimamoto la Knight Support? limepaki na wakipiga stori.Cha ajabu wale wafanyabiashara nje tu kidogo ya uzio walikuwa wanaendelea na biashara kama vile ni taka taka za TANESCO zinachomwa pale......................ndo kusema wamezoea. Ila sikuona FFU na Polisi,na JKT wakiwasili kwa speed ya Mbeya, Arusha na Tabora
 
mmh?kila ninapokatiza pale ubungo na kuona rundo la wale wafanyabiashara chini ya nyaya za umeme wazo linanijia kwamba iko siku wale binadamu pale chini tutaokota mikaa mingi tu na majivu tukazike
hakuna anayeona ile hatari pale!
 
NIKWELI, transforma limelipuka pale Ubungo!,
Ndo tushalala giza hivyo!

Ni kweli tatizo lipo na limetokana na reactor kuripuka na moto wake kuambukizia transformer ya jirani. Ijapokuwa moto umezimwa lakini madhara yake yanaweza kuwa ya muda mrefu. Ninafikiri hawana kitengo cha Predictive maintenance. Ni aibu kubwa kwa kampuni kubwa kama hii kushindwa kugundua matatizo kama haya mapema.
 
TANESCO watatoa taarifa kupitia kwa Barbara Masoud muda mchache ujao. Mia
 
Kama anavyosema mkeshaji hapo juu, ni transfomer mbili za tanesco zimepiga mzinga sasa issue hapa sidhani kama wana spare so tutarajie kuishi gizani for some days,dah!
 
Hii wamelipua makusudi ili watanzania wasisikie tamko la Mh.Mbowe kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya kupinga muswada.Lakini wanasahau kwamba Nyerere aliweza kuwasiliana na watanganyika na wakaelewana katika harakati za kudai uhuru.Mh.mbowe tumia njia za kizamani tutakuelewa tu.tumia hata sms zitawafikia wote.sms zitume hata kutokea ufaransa zitatufikia tuuuuuu!!!!
 
Back
Top Bottom