Mlipuko watokea Ubungo-TANESCO, umeme wakatika!

Kweli mwaka huu hatutoki. Matatizo kila upande. Hii serikali kwa kweli ipo ICU
 
Ni kweli Ila sio Mlipuko Mkubwa ila Moto Unaendelea Taratibu!! Katika Kitondo cha air release Friction imekuwa Kubwa Hadi Moto Ukatokea!! Sijajua Kama Wataweza Kuudhibiti!!
 
Nilikua pale ubungo kwy mataa wakati transfomer inalipuka ghafula nikawaza unaweza kutokea moto mkubwa sana kutokana na Songas kuwa karibu nilizima gari mikatoka nje nataka nikimbie bahati nzuri traffic akaruhusu gari za upande wetu duh!!
 
Morogoro pia hakuna umeme nipo maeneo ya forest huku umekatika wakati mechi ya stars inaenda mapumziko baada ya hapo radio zote hazipatikani mpaka sasa hakuna umeme
 
Nadhani ni matatizo kidogo. Mafundi watakuwa wanalifanyia kazi. Hizo ni changamoto ndogondogo.
 
Moto mkubwa umelipuka katika National Grid Control Centre iliyopo Ubungo jijini Dsm. Moto huo umedhibitiwa na wazima moto wa kampuni binafsi ya Knight Support ambao walikuwa wameweka Base yao maeneo ya karibu. Inasemekana kampuni hiyo haikuwa tayari kuzima moto huo hadi ilipothibitishiwa malipo na TANESCO.

Vikosi vya zimamoto vya jiji kama kawaida vilikuja huku vikiwa vimechelewa sana.

Habari zaidi na picha baadae kidogo.
 
Ubungo nako, kila siku mabalaa.
Foleni Ubungo, Milipuko hukohuko Ubungo, uhaba wa maji hukohuko Ubungo, yaani ka kalala paka
 
du kaaaazi kweli kweli,arusha pia umekatika. alie na mawasiliano na ile mikoa ya kiswahili lindi,mtwara,tanga pwani atujuze maana huko ndo ngome ya magamba sidhani kama wataweza wakatia na kura zote walizowapa. maana wadau niloona wanalala mika giza ni toka arusha,dar,mwanza. pia tunahitaja verification ya kulipuka kwa hizo transforma
 
Hata uku Zanzibar umeme umekatika mida iyo ya saa kumi na moja kasoro.
Basi hii inaweza tuchukua masaa mengi tukiwa kizani.
Kama huwa tnakua kizani bila sababu leo je?
 
Hata hapa kakola umekatika lakini tunamagenerator ya dharula tumeisha washa maisha yanaendelea sasa hivi kama kawa. Poleni wengine kwa sababu huku tumeambiwa itachukua muda mrefu.
 
Back
Top Bottom