Mliowahi kutumia bati za kampuni ya BATI BOMBA LTD au kampuni zozote ndogo za mabati

Mkuu bado unataka kutumia hizi bati bomba au umebadili mawazo?
Nimetumia hizo hizo kaka. Budget ilishanikataa
20230909_162223.jpg
 
Hivi tunapozungumzia ubora wa bati tunaangalia muda mpaka bati ianze kupata kutu au muda ambao rangi itaanza kupauka?

Maana hizo unazosema za bei ndogo zimepitishwa na TBS,na wanatoa warranty ya miaka 10,sasa kigezo cha kuzipitisha ni nini? ina maana zinakidhi viwango.

Mi naona mambo mengine hapa ni mfuko wa mtu,weka bati kulingana na uwezo wako,kwani wengi wetu nchi nzima tunaweka haya viwanda vidogo na hayo maswala ya kutu au rangi tutadanganyana tu humu...
Yaani bado unawaamini TBS hawa hawa pole sana,
 
Ili kufanya ulinganifu wa haki yabidi kujiuliza maswali haya kuhusu vipimo.
1. Bati unazotaka kununua zina vipimo gani kwa upana na urefu? Huwezi kufanananisha bei bila kujua upana kwa mfano kuna za upana halisi (effective width) 75cm, 80cm, 90cm nk.
2. Unene wa bati l; geji 26, 28, 30,32?

Pamoja na vipimo, kikubwa kinachotofautisha sana ubora ni kiasi cha aluzinc (aluminium na zinc) kilichotumika kulinda bati dhidi ya kutu. Kuna mabati yanatumia kiasi kidogo cha aluzinc ili kupunguza gharama za uzalishaji (aluzinc ni ghali kati ya malighali za utengenezaji wa bati).
Bati nyingi hapa Tanzania hazitengenezwi hapa, wanaagiza hapa wanakunja na kukata tu.
 
Back
Top Bottom