Nitumie mabati gani kati ya Bomba na Dragon?

Nchiyanguu

JF-Expert Member
Sep 3, 2021
258
467
Habari za asubuhi wana jukwaa wenzangu.

Naenda moja kwa moja kwenye maada nipo kwenye hatua ya kupau nyumba. Nimeumiza kichwa sana kuwa ni bati gani ambazo zitaendana na uwezo wangu ALAF achana nazo bei zake za moto sana.

Je kati ya bati bomba na dragon mnanishauri ipi? Au kampuni ipi nyingine ni bora na nafuaa?

Na je nimesikia kuwa mabati ya migongo mipana haidumu kama ya migongo midogo. Je, hili lina ukweli?

Ahsanteni sana, naomba mawazo yenu.
 
Usijaribu kuhangaika na bati ya aina yoyote zaidi ya ALAF. Vinginevyo bora uendelee kuvumilia kama ulivyovumilia mpaka kufikia hapo. ALAF za moto lakini ndio kilicho bora. Ukichukua tu aina nyingine utakuja kujuta milele
 
Nimesikia sana ubora wa mabati ya ALAF lakini kuna mabati hawa KAMAKA wanaleta yeyote mwenye info?
 
Habari za asubuhi wana jukwaa wenzangu.

Naenda moja kwa moja kwenye maada nipo kwenye hatua ya kupau nyumba. Nimeumiza kichwa sana kuwa ni bati gani ambazo zitaendana na uwezo wangu ALAF achana nazo bei zake za moto sana.

Je kati ya bati bomba na dragon mnanishauri ipi? Au kampuni ipi nyingine ni bora na nafuaa?

Na je nimesikia kuwa mabati ya migongo mipana haidumu kama ya migongo midogo. Je, hili lina ukweli?

Ahsanteni sana, naomba mawazo yenu.
Bati ni alaf au Nabaki Africa hizo zingine ni takataka
 
Back
Top Bottom