Mlioko Uingereza, msaidieni huyu mama kufahamu wanawe walipo

Ni habari nzuri kuskia kwamba wamepatikana. lakini ninasikitika kwamba hadi sasa hivi March 2022 niko ofisi moja arusha na mama wa huyo binti na binti hajawasiliana na mzazi wake bado, ushauri wenye tija tafadhali kwa ajili ya kumsaidia huyu mama angalau apate kuwasiliana na binti yake. Grace aliyetoa update nilimuandikia kule michuzi lakini hajajibu bado.
Ina mana hadi leo hawajawahi onana na mama yao hao watoto?
 
Wewe ni mke wa marehemu Abbas wa Bondeni Arusha....????

Huyo Msomali Mahmood kwao ni Ngarnaro .....???

Nauliza hivyo ili nasi tuanze kukusaidia kupitia ndugu na jamaa wa Mahmood
Mcheki kwa contacts zake wewe ni msaada mkubwa sana
 
Sio mda wa kumlaumu muhusika- mpotelewa watoto.. daah sema inafikirisha sana
 
Mkuu "bond" inaanzia tumboni,unaweza kutenga kila siku asubuhi uamkapo,na jioni ulalapo ukawa unashika tumbo la Mama na kumwambia mtoto maneno ya heri,ukimwambia kuwa unamsubiri kwa hamu aje,unamfurahia kama zawadi na huku ukimsisitiza akuombee heri upate riziki ya kuja kumtunza vyema.

Siku akizaliwa,angali mchanga,unachukua faragha naye na kuongea naye kuwa wewe ni mzazi wake,unamtakia maisha mema ktk dunia,unamtakia heri na afya ili akikua akukute na uone utu uzima wake.Yaani unamsemesha kama vile ni mtu mzima.Hii inakuwa ni "Spiritual Bonding"....Sababu ni mawasiliano ya kiroho kati ya wewe na mtoto.

Baadaye ndani ya miaka 02-06 unaanza kujenga taswira yako ktk ubongo wa mtoto,ndio pale anaanza kukuita baba bila yeye kujua alianzaje kukuita baba.

Miaka 06 -16 ndio haswaa "physical bond" inaimalika.Hapa mtoto anaona kama ni Mama basi anaona ule Umama wako,kama ni baba basi anaona ule ubaba wako,ana-feel ile protection,akipigwa na wenzake anatoka mbio anakuja kusema baba nimepigwa na huyu,kama ni kwa Mama basi anaenda kusema Mama hapa panawasha nikune.

Hii ya Baba nimepigwa inakuja kwako sbb anaanza kujifunza "sense of protectionism" hutoka kwa baba,anasema Mama hapa nimeumia au hapa panawasha,sbb tayari amejifunz kuwa "sense of Sympathy(?) and Care" hutoka kwa Mama.

Ndio maana unaona ukitaka pesa ya kununulia vibama unaenda kwa Mama,lakini hela ya daftari au kalamu unamwambia Baba.Hapo ubongo wa mtoto umekuwa na kujua nani ni nani...,

Ni somo lefu sana...,Ambalo sisi tuliozaliwa na Wazee wa 1920's hatukulipata sana,ila sisi tunapaswa kuwapa upendo huu watoto wetu,iwe wa kike au kiume.
Asante kwa elimu kiongozi👌
 
Where We Dare To Talk Openly

Mlioko Uingereza, msaidieni huyu mama kufahamu wanawe walipo​

MSAADA TUTANI: OMBI LA KUWASILIANA NA WATOTO WALIOPO UINGEREZA KWA ZAIDI YA MIAKA 22 SASA.

87a7dba21b625a50ae6f47a140659a2c.jpg

Picha za awali za wahusika wa waraka huu ikiwa ni pamoja na watoto Amina na Seleman Kichawela na Bw. Mahmud Hassan Mihile aliyewachukua miaka 22 iliyopita ili kuwasaidia masomo huko Uingereza.

Kutokana na kichwa cha habari hapo juu mimi AZAMA ABBASI KICHAWELE ambae kwa sasa ni mjane, mwenye namba ya simu +255 784 697319 na mkazi wa Majengo Arusha, Tanzania, na ambae ni mama wa nyumbani, nachukua nafasi hii kukutaarifu kama ifuatavyo.

Mume wangu kwa majina ABBASI ALLY KICHAWELE ambaye kwa sasa ni marehemu alikua na rafiki wake wa karibu kwa majina MAHMUD HASSAN MIHILE aliekuwa akitumia namba ya simu +441332270462 wakati huo mwenye asili ya Kisomali na uraia wa Uingereza na Tanzania walikubaliana awachukue watoto wetu ambao ni:

SELEMAN ABBASI KICHAWELE aliekuwa na umri wa miaka kumi na AMINA JABIRI KICHAWELE aliekuwa na umri wa miaka saba aende nao Uingereza kwa ajili ya kuwasomesha.

Siku ya kuondoka watoto hawa ilikuwa ni mwaka 1994 na waliondoka na mke wa huyo Msomali kwa majina RAHMA MIHILE.

Mji wa kwanza walioshukia huko UINGEREZA unaitwa LEICESTER.

Baada ya hapo mawasiliano yaliendelea kuwepo kati ya mzazi wa kiume wa watoto na Msomali.

NB: Katika hawa watoto huyu wa kike, Amina Jabiri alikuwa ni wa mdogo wake mume wangu yaani shemeji yangu.

Kwa bahati mbaya mume wangu, aliugua maradhi ya cancer na ilipofika mwaka 1998, nikampoteza (alitangulia mbele ya haki).

Baada ya kifo cha mume wangu hakukua na mawasiliano yoyote kati yangu na huyu bwana aliyechukua watoto wangu.

Alikata mawasiliano kabisa na wala hakutaka watoto wajue kuwa baba yao hayupo tena Duniani.

Kwa bahati mbaya sikua na mtu mwingine mbadala wa kuweza kuniunganisha na huyu bwana ikizingatiwa pia mimi ni mama wa nyumbani sikuwa na PR kubwa. Leo hii ninapoandika barua hii, huu ni mwaka wa ishirini na mbili (22) toka nitengane na watoto wangu. Sisi pamoja na wanafamilia tutaendelea kutoa shukrani zetu kwa serikali ya Uingereza iwapo watoto hawa wapo salama na kwenye ajira zao. Kwetu hilo sio tatizo.

Jambo kubwa linaloniumiza ni kutokua na MAWASILIANO na watoto wangu kwa miaka ishirini na mbili sasa. Wakati mwingine najenga wasiwasi kwamba je, wako hai? Na hali hii nitaendelea nayo mpaka lini?

Huyu bwana Mahamudu (msomali) nini kimemsukuma kuwa na ujasiri wa kuwaficha watoto wangu hata nisiwe na mawasiliano nao? Ana dhamira gain?

Kutokana na maelezo mafupi hapo juu nimefikia hatua ya kuiomba ofisi yako tukufu kunisaidia kupata namna ya kuwasiliana na watoto wangu wapendwa huko waliko.

Jambo hili likifanikiwa litaleta faraja sana kwangu na kwa wana familia kwa ujumla.

Pia itakuwa ni fursa kwa watoto kutambua kuwa baba yao mpendwa alishafariki lakini mimi mama yao bado nipo hai, taarifa ambazo tuna hakika hawajazipata.

Naambatanisha picha za watoto ambazo walipigwa wakati wanakaribia kuondoka mwaka 1994.

Pia naambatinisha na picha ya Mahmud Hassan Mihile (Msomali) ya wakati huo aliyewachukua watoto kwa makubaliano na mume wangu.

NB: Kwa mawasiliano tumia namba hizi za barua pepe
hasatathuman@gmail.com
emfinanga4@gmail.com
Au Athuman Rashid Mfinanga
Box 2614, - Arusha Tanzania
Ph: 0754375602/0784375602/0689653424

Wako,
Katika ujenzi wa Taifa
Azama Abbasi Kichawele


Chanzo: Michuzi blog

============================
======================================
UPDATES kuhusu kupatikana kwa watoto
 
Umaskini Mbaya sana.
Hapa ukute watoto walishadhurika kisa njaa na umaskini wa akili na kipato kwa wazazi.
Nimeangalia picha mara kadhaa na kujawa na majonzi. Tunaona binadamu wakitumika kufanya makafara na matambiko tuombe Ndugu zetu na watoto wetu hawa wawe salama.

Lkn mpaka hapo mama alitakiwa awekwe chini ya ulinzi ahojiwe kwa kushindwa kuwalinda watoto wake.
 
Umaskini Mbaya sana.
Hapa ukute watoto walishadhurika kisa njaa na umaskini wa akili na kipato kwa wazazi.
Nimeangalia picha mara kadhaa na kujawa na majonzi. Tunaona binadamu wakitumika kufanya makafara na matambiko tuombe Ndugu zetu na watoto wetu hawa wawe salama.

Lkn mpaka hapo mama alitakiwa awekwe chini ya ulinzi ahojiwe kwa kushindwa kuwalinda watoto wake.
kwa hiyo akishawekwa chini ya huo ulinzi ndo utasababisha watoto wapatikane.....
 
That was more than confidence. Nimpe mtu watoto wangu wa umri mdogo hivi aende Nao abroad. Inaonyesha Mume wako alikuwa na agenda ya Siri Kati yake na Rafiki yake. Isitoshe hata huyo Msomali hayuko hai
 
10 + 22 = 32yrs wa kike
7 + 22 = 29yrs wa kiume

Mama hapa anawataka watoto wake aishi nao au awaone tu ???maana kwa hiyo miaka hakuna chemistry(kama wakiwa hai) au mama kwa msoto wa maisha anataka ateljee kwa watoto wake.

Ujinga alishaufanya kuwatoa watoto waende wakakae mbali na mtu baki ilihali yupo hai
 
Amekutuma mwenyewe au? maana hiyo habari ni ya toka 2017.


Huyo Mahmood Mihile ukitaka kumpata ‘google search’ inaonyesha sio muda mrefu alishirikiana na taasisi moja ya maji kwenye charity ya mpira watakuwa na details zake.

Number ya 01332 hiyo ni area code ya Derby na sio mbali na Leicester ni miji jirani, hayo maeneo kuna wabongo wasomali kadhaa, ukimpata mwenyeji wa Derby anampata.

Sasa shutuma za wizi wa watoto (sio za mzaha uingereza) na watoto wenyewe ukute wamejipiga wasomali kama njia ya kupata makaratasi yao. Ukiingiza polisi na immigration usije kuharibia kila mtu na hao watoto wenyewe.

Ni ushauri tu vitu vya kuzingatia kabla kukurupuka. Halafu hao watoto sasa hivi watakuwa washakuwa wakubwa wanajitegemea. Huyo mama angetafuta mtu anaemfahamu U.K. mradi huyo Mahmood Mihile anatumia jina hilo hilo atakuwa tu kwenye data base za serikali na kupatikana kwa njia za mtaa.

Kuliko haya makelele akaenda wapelekea matatizo makubwa kwa njaa zake, utampaje mtu watoto wako kisa waende ulaya.
 
10 + 22 = 32yrs wa kike
7 + 22 = 29yrs wa kiume

Mama hapa anawataka watoto wake aishi nao au awaone tu ???maana kwa hiyo miaka hakuna chemistry(kama wakiwa hai) au mama kwa msoto wa maisha anataka ateljee kwa watoto wake.

Ujinga alishaufanya kuwatoa watoto waende wakakae mbali na mtu baki ilihali yupo hai
Inafikirisha sana:confused:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom