Jamani mmenikumbusha marehemu rafiki yangu, alikua akipenda sana huu mchezo, alikua akitoroka shule akacheze mpira na kila alipotembea alitemebea na mpira wake, yaani vidole vya miguu vyote vilikua vimechakaa kwa vidonda tulikua tunaita kupiga ndole; alikua na interest mbili, mpira na magari na kwelia alikuja kuwa fundi magari baada ya kumaliza darasa la saba kwa bahati mbaya sana siku ambayo ndio alikwenda Tanga kukabidhiwa Canter awe dereva ndio siku hio alipata ajali na kufa papo hapo.
Yaani hakuweza kuiona ndoto yake tena, it was so pianful, pumzika kwa Amani