Tetesi: Mkwamo wa Uteuzi wa wagombea EALA- CCM (Ngoja niwape mbinu)

Bemendazole

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
2,363
5,883
Leo, makada wengi wa chama pendwa walitarajia Shaka angetoa orodha ya walioteuliwa kugombea nafasi za Ubunge wa Afrika Mashariki, Lakini hakufanya hivyo.

Dalili zinaonesha kuna mkwamo mahali fulani na nani apite, nani atemwe! Tathmini yangu inaonesha vigogo wengi wameleta vimemo wakipendekeza watu wao. Wengine ni watoto wa vigogo na wengine ni washirika wa karibu kiasi kwamba chama kimepata kigugumizi kisijue nani apitishwe nani aachwe.

Lakini ngoja ni wapeni mbinu, kanuni ya mchezo huu inasema, ukitaka kumuua nyani, usimuangalie usoni. Ili kupitisha majina, angalieni sifa kama kujitoa kwa mwanachama, uwezo wa mwanachama kitaaluma na kujenga hoja nk.

Msiangalie huyu ni mtoto wa mjomba, huyu tulisoma naye, mkiangalia vigezo hivyo ni sawa na kumuangalia nyani usoni na mchakato utaisha kwa maning'uniko.
 
Wajumbe wampe nafasi Pascal Mayalla.
Mkuu Tate Mkuu, kwanza asante kuniombea kupitishwa
Kiukweli amejitahidi sana kukipigania chama humu jukwaani.
Mimi sikipiganii chama, kwasababu CCM haihitaji kupiganiwa! iko imara as fit as fiddle!. Na ikitokea mimi ndie nikapitishwa, niwe nimepitishwa kwa kukidhi sifa na vigezo na sio kwa kukipigania chama!.
Amekubali kuishi kinafiki ili chama kionekane kipo imara.
Kivipi?, ili kionekane kama kipo imara!, kwani chama hakipo imara?, kivipi?. Kwa maoni yangu kwa sasa chama kiko imara kuliko hata enzi zile!.
P
 
Mkuu Tate Mkuu, kwanza asante kuniombea kupitishwa

Mimi sikipiganii chama, kwasababu CCM haihitaji kupiganiwa! iko imara as fit as fiddle!. Na ikitokea mimi ndie nikapitishwa, niwe nimepitishwa kwa kukidhi sifa na vigezo na sio kwa kukipigania chama!.

Kivipi?, ili kionekane kama kipo imara!, kwani chama hakipo imara?, kivipi?. Kwa maoni yangu kwa sasa chama kiko imara kuliko hata enzi zile!.
P
Kwanza CCM siyo Imara, pili huwezi kupitishwa kuwa mgombea wa CCM kama huna sifa ya kukipigania kiuwendawazimu chama hicho. Wasirra kila mara anachaguliwa kwa hoja kwamba yeye ndiye ana uwezo wa kushindana na CHADEMA.

Kama huipiganii CCM unataka kugombea kupitia CCM ili iweje?
 
CCM inajua kwamba Pascal Mayalla ni "Double Agent" na wakimchukua atakuwa "Mole" kwenye chama chao kwa faida ya wapinzani (Siyo CHADEMA).
Mimi sio double agent, bali ni hawa CCM mpya, contemporary, ambao ni wapenda haki, tunataka CCM ishinde kwa haki, na CCM kama chama tawala, kina wajibu wa kulea upinzani na hata kuwaachia bure kabisa baadhi ya majimbo.
Miongoni mwa ushauri wangu mzuri na wa haki kwa chama changu ni huu Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa! na huu Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi
P
 
Kwanza CCM siyo Imara, pili huwezi kupitishwa kuwa mgombea wa CCM kama huna sifa ya kukipigania kiuwendawazimu chama hicho. Wasirra kila mara anachaguliwa kwa hoja kwamba yeye ndiye ana uwezo wa kushindana na CHADEMA.

Kama huipiganii CCM unataka kugombea kupitia CCM ili iweje?
Ule ni ubunge wa EALA ni ubunge wa kupigania nchi sio kupigania chama!. Wanaotakiwa kwenda kule sio makada hiyena hiyena ni watu ma pro wenye uwezo wa kuipigania nchi!. Ushauri huu nimeutoa kwa chama changu Ubunge EALA, Wito Kwa CCM, Msiangalie Ukwasi, Tuteulieni, Wazalendo wa Kweli wa Taifa Hili, Wenye Uwezo na Uzoefu wa Kimataifa Kutuwakilisha Ipasavyo
P
 
Back
Top Bottom