GE2025 Mkuwe Isale (Mamy Baby) achukua fomu ya kugombea Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora

GE2025 Mkuwe Isale (Mamy Baby) achukua fomu ya kugombea Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Mtangazaji na mwanaharakati wa kijamii, Mkuwe Abdul Isale maarufu kama Mamy Baby, ameonyesha nia ya kulitumikia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum.

IMG_5394.jpeg

Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) – Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Tabora, Mamy Baby amechukua rasmi fomu ya kuwania nafasi hiyo leo Juni 28, 2025.

IMG_5393.jpeg

Mamy Baby ambaye amejipatia umaarufu kupitia kazi zake za utangazaji na shughuli za kijamii kupitia taasisi yake ya Dada Hood, amesema ana lengo la kuwasemea wanawake wa Mkoa wa Tabora na kuendeleza juhudi za kusaidia makundi yenye uhitaji.
IMG_5392.jpeg
 
Miaka ya zamani ukiambiwa mtu ni mbunge, akianza kuongea tu, unasema huyu kweli ni mbunge. Siku hizi mtu yeyote anaweza kuwa mbunge, waziri n.k. Kila la heri kwake.
Kabisa yaaan mkuu ukiskia kimiti anatoa hoja unajua kabisa Kuna mtu anaongea, sasa Leo ebu kamsikie Babu Tale akiongea utaona aibu wakenya wasiipate
 
Nachoshukuru katoka na make up artist wake dar, na kitenge kashonea dar,

Kalunde mmemuona mke wa mjomba ,
 
Miaka ya zamani ukiambiwa mtu ni mbunge, akianza kuongea tu, unasema huyu kweli ni mbunge. Siku hizi mtu yeyote anaweza kuwa mbunge, waziri n.k. Kila la heri kwake.
Miaka hii ya sasa unaweza kumsikia kiongozi wako akiongea ukatamani uingie chini ya meza, ni kwa bahati mbaya sana meza zetu za sasa hazina mazingira ya kutosha kujificha.
 
Miaka ya zamani ukiambiwa mtu ni mbunge, akianza kuongea tu, unasema huyu kweli ni mbunge. Siku hizi mtu yeyote anaweza kuwa mbunge, waziri n.k. Kila la heri kwake.
Walifanya nini cha maana hao wabunge wa zamani?
 
Ngoja wauchimbe ubunge kijijini halafu wakiupata, haoo wanaenda zao kula maisha Dar es salaam, safi sana watu wa kijijini kwa huu upendo
 
Back
Top Bottom