GE2025 Mkuwe Isale (Mamy Baby) achukua fomu ya kugombea Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora

GE2025 Mkuwe Isale (Mamy Baby) achukua fomu ya kugombea Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Miaka hii ya sasa unaweza kumsikia kiongozi wako akiongea ukatamani uingie chini ya meza, ni kwa bahati mbaya sana meza zetu za sasa hazina mazingira ya kutosha kujificha.
Sahihi kabisa
 
Kabisa yaaan mkuu ukiskia kimiti anatoa hoja unajua kabisa Kuna mtu anaongea, sasa Leo ebu kamsikie Babu Tale akiongea utaona aibu wakenya wasiipate
Sahihi kabisa mkuu
 
Miaka ya zamani ukiambiwa mtu ni mbunge, akianza kuongea tu, unasema huyu kweli ni mbunge. Siku hizi mtu yeyote anaweza kuwa mbunge, waziri n.k. Kila la heri kwake.
Zamani gani? Wabunge wa 95 tu hapo walikua hamna kitu
 
Mtangazaji na mwanaharakati wa kijamii, Mkuwe Abdul Isale maarufu kama Mamy Baby, ameonyesha nia ya kulitumikia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum.

View attachment 3386763
Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) – Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Tabora, Mamy Baby amechukua rasmi fomu ya kuwania nafasi hiyo leo Juni 28, 2025.

View attachment 3386765
Mamy Baby ambaye amejipatia umaarufu kupitia kazi zake za utangazaji na shughuli za kijamii kupitia taasisi yake ya Dada Hood, amesema ana lengo la kuwasemea wanawake wa Mkoa wa Tabora na kuendeleza juhudi za kusaidia makundi yenye uhitaji.
View attachment 3386766
Haka si kalikuwa ka dj kanapiga piga kelele pale clouds?
 
Uyo Munde jina lake kamili ni nani
Munde Tambwe kama sijakosea ..Mbunge wa CCM viti Maalum Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa..
Mama yake nadhani nae alishakuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora miaka ya nyuma...ila wacha yakanyagane
 
Kabisa yaaan mkuu ukiskia kimiti anatoa hoja unajua kabisa Kuna mtu anaongea, sasa Leo ebu kamsikie Babu Tale akiongea utaona aibu wakenya wasiipate
"Nimekua nikiomba barabara kwa miaka mitano" 🚮
 
Zamani gani? Wabunge wa 95 tu hapo walikua hamna kitu
Endelea kuangalia aina ya watia nia wanaoutaka ubunge leo angalia na wabunge wa hapo nyuma mpaka kuja kwa Sitta na mama Makinda, utaelewa namaanisha nini.
 
Miaka hii ya sasa unaweza kumsikia kiongozi wako akiongea ukatamani uingie chini ya meza, ni kwa bahati mbaya sana meza zetu za sasa hazina mazingira ya kutosha kujificha.
Nimeisoma kwa kumaanisha sana yaani mbunge anaongea bungeni Dodoma ila aibu napata mimi wa Kantalamba Rukwa huko😂
 
Walifanya nini cha maana hao wabunge wa zamani?
Walifanya deni la taifa kuwa dogo sana hd kiongozi alikuwa anaogopa kukopa ovyo. Walifanya wananchi wajione tuko na wawakilishi wetu bungeni ndo maana kutekana tekana haikuwepo maana bunge lilikuwa linaongea ya wananchi. Hili la sasa limefanya nini?
 
Back
Top Bottom