Serengeti: Mhasibu wa Halmashauri apiga milioni 213

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
476
1,244
HABARI Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amemwagiza Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, ACP Salum Morcase amkamate Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti, Saad Mutunzi Ishabailu kwa kosa la kuhamisha shilingi milioni 213,748,085 kwa awamu nne kwa njia ya uhamisho wa ndani kwa kushirikiana na watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi.

Ametoa agizo hilo leo Jumanne, Februari 27, 2024, wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti kwenye kikao kilichofanyika katika Halmashauri hiyo, mkoani Mara.

"Mkamate huyo bwana sasa hivi aende polisi akafunguliwe mashtaka, huyu ni wa kupeleka mahakamani moja kwa moja. DPP aelezwe afungue jalada la mashtaka, wale wenzake tumewapeleka mahakamani tayari sababu tulibaini walihusika na wizi kama huu kwenye Manispaa ya Kigoma mwaka jana," amesema Waziri Mkuu

Amesema Juni 21, mwaka jana Bw. Ishabailu alianza kufanya matumizi ya hizo fedha kwa kushirikiana na mfanyabiashara wa hapa Mugumu, Bw. Daudi Matinde Chacha kupitia kwenye akaunti zake za NMB na CRDB kwa kupitia miamala minne ya sh. milioni 76.3, sh. milioni 57.7, sh. milioni 47 na sh.milioni 32.5.

Amesema alipoulizwa na timu ya uchunguzi Bw. Matinde alikiri kuwa haidai fedha yoyote Halmashauri ya Serengeti isipokuwa Mweka Hazina huyo aliomba apitishie fedha zake kwenye akaunti zake kwa sababu zinahitajika haraka kwa matumizi ya ofisi. “Aliambiwa atoe shilingi milioni 189 akamkabidhi zote Bw. Ishabailu na zilizobakia (sh. milioni 24) akaambiwa abaki nazo,” amesema Waziri Mkuu.

Chanzo: EastAfricaTV
 
Nchi hii imeoza ILA wao ndio wanasababisha unamlipa mwasibu wa halmashauri laki 9 halafu mwasibu wa psssf unamlipa 15M. Hii ndio Nini ??

Hakuna usawa wa kimaslahi na hii ndio sababu pia ya kukosekana Kwa ufanisi serikalini...
 
Mhasibu Mutunzi sio mjinga, na sio mlevi, hawezi kukosa milioni 20 ya hakimu mfawidhi na milioni tano ya faini. Kwa mtazamo wa hakimu, akikufunga anapata nini? Na akipindisha haki anahojiwa na nani nchi hii? Hukumu ni faini. Ukifanya ujambazi tenga hela ya mahakama.

Ndo maana Mwenezi Makonda, give the devil his due, kasema huko mahakamani nimewaambia msende jamaniiiiii...
 
Serikali imechelewa sana kung'amua mbinu hii ya Wizi. Imetumika toka enzi za JK, too late kustuka leo. Hiii mifumo ya Kielektroniki kuna wajanja wanajua kucheza nayo.
Mfano Makusanyo yanaweza kukusanywa 170 Milioni ikapigwa 70 kwamba imeingia kimakosa kutokana na entry mbaya za numbers. Kwa kifupi Vijana wa IT wanatunyoosha sana kushirikiana na Wahasibu
 
Nchi hii imeoza ILA wao ndio wanasababisha unamlipa mwasibu wa halmashauri laki 9 halafu mwasibu wa psssf unamlipa 15M. Hii ndio Nini ??

Hakuna usawa wa kimaslahi na hii ndio sababu pia ya kukosekana Kwa ufanisi serikalini...
True
Mtumishi ukipata gap piga,kukamatwa ajali kazini
Halmashauri mishahara na marupurupu ni madogo
Maisha gharama juu,hata mie nilipata gap nabutua
 
HABARI Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amemwagiza Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, ACP Salum Morcase amkamate Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti, Saad Mutunzi Ishabailu kwa kosa la kuhamisha shilingi milioni 213,748,085 kwa awamu nne kwa njia ya uhamisho wa ndani kwa kushirikiana na watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi.

Ametoa agizo hilo leo Jumanne, Februari 27, 2024, wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti kwenye kikao kilichofanyika katika Halmashauri hiyo, mkoani Mara.

"Mkamate huyo bwana sasa hivi aende polisi akafunguliwe mashtaka, huyu ni wa kupeleka mahakamani moja kwa moja. DPP aelezwe afungue jalada la mashtaka, wale wenzake tumewapeleka mahakamani tayari sababu tulibaini walihusika na wizi kama huu kwenye Manispaa ya Kigoma mwaka jana," amesema Waziri Mkuu

Amesema Juni 21, mwaka jana Bw. Ishabailu alianza kufanya matumizi ya hizo fedha kwa kushirikiana na mfanyabiashara wa hapa Mugumu, Bw. Daudi Matinde Chacha kupitia kwenye akaunti zake za NMB na CRDB kwa kupitia miamala minne ya sh. milioni 76.3, sh. milioni 57.7, sh. milioni 47 na sh.milioni 32.5.

Amesema alipoulizwa na timu ya uchunguzi Bw. Matinde alikiri kuwa haidai fedha yoyote Halmashauri ya Serengeti isipokuwa Mweka Hazina huyo aliomba apitishie fedha zake kwenye akaunti zake kwa sababu zinahitajika haraka kwa matumizi ya ofisi. “Aliambiwa atoe shilingi milioni 189 akamkabidhi zote Bw. Ishabailu na zilizobakia (sh. milioni 24) akaambiwa abaki nazo,” amesema Waziri Mkuu.

Chanzo:EastAfricaTV
Pale jambazi la kupora kwa silaha benki linapoamrisha kibaka muibaji wa kuku akamatwe....
 
True
Mtumishi ukipata gap piga,kukamatwa ajali kazini
Halmashauri mishahara na marupurupu ni madogo
Maisha gharama juu,hata mie nilipata gap nabutua
Hahaaaaa, mi nilibutua sehemu. Mbona hao akina Majaliwa, February na Bashe bila kusahau bi.tozo wanabutua tu. Nchi hii hakuna mwaminifu, ni blah blha na mbwembwe. PM atuambie, zile pesa walizochota Hazina na Mpango, Katibu Mkuu Utumishi ndugu Bashiru Ally na akina Dotto James wakati wa kifo cha JPM waliipeleka wapi?
 
Back
Top Bottom