Mkuu wa Wilaya ya Kyela asimamishwa kazi baada ya kufumaniwa na mkewe

We mwenyewe umefanya kama huyo mke. Kitendo cha kumwanika Mh.Magh... pia ni kumwaibisha. Heri huyo mke alifanya kwa hasira. Wewe je,kilikusibu nini? Wewe ni mbaya zaidi ya huyo mke. Au ulikuwa na lako jambo?
 
Huyo mke nae mjinga angeyamaliza na mme wake au kifamilia tu!sasa kumchafua mme wake ndo nini?kina magufuli hadi wana vimada na mke anajua na anaishi na mtoto wa kimada wa magufuli!
Sijafurahia kitendo cha mke wa huyu mkuu wa wilaya!mimi siwezi muabisha namna hii mme wangu!wangeyamaliza kibusara tu!

Aisee!! Kweli nimeamini mchawi wa mwanamke ni mwanamke!! Kwa hiyo hiki ndicho unachomshauri mwanamke mwenzio??
 
Huyo mke nae mjinga angeyamaliza na mme wake au kifamilia tu!sasa kumchafua mme wake ndo nini?kina magufuli hadi wana vimada na mke anajua na anaishi na mtoto wa kimada wa magufuli!
Sijafurahia kitendo cha mke wa huyu mkuu wa wilaya!mimi siwezi muabisha namna hii mme wangu!wangeyamaliza kibusara tu!
Natamani nikuoe Victorie, yaani nimekupenda ghafla. Njoo tujenge familia jamaniii.....
 
Nafikiri kwenye hili wote ni losers. Huyo mwanamke naye alijua kabisa kwamba huyo ni nyumba ndogo ya mumewe, sasa kwanini apige kelele za mwizi?

Je watu wangeingia na kumuua huyo dada si ingelikuwa balaa kubwa kwa wahusika wote?

Yeye angemwandama mumewe na kama mambo yameshindikana basi akaomba talaka.

Unataka kusema kuwa kakosea kumuita mwizi? Yaani mtu anakuibia mali ya muhimu kama mume bado unaona sio mwizi? Bado umemkuta ndani kwako, sio mwizi huyo? Unaomba talaka mtu pengine unakaribia 50years unaenda wapi, umeliwa ujana wako woote halafu ujiombee talaka umuache mtu aendelee kushine....acha kumtupia lawama asiye na kosa na kuhalalisha wenye makosa kuwa wasafi.
 
Nona jinsi kila mtu anavyoijadili hii maada, mwanaume amefanya kosa la kufanya part time. Watu tunaona mkewe kakosea kwa sababu wanaume wanaona wana haki ya kuanya kazi za nje. Jamaa kaharibu, na amejiabisha wala si mkewe aliyemwaibisha. Na Kyela inavyotisha kwa ngoma lakini watu bado hawaachi kazi za nje. Tutakufa kama kuku . sasa huyo mkuu wa wilaya alikuwa anawaeleza nini kyela kuhusu ngono uzembe. tutamalizika sote namna hii.

Ujobhile gwa kwa Mwakalili. Kyela kwa ngoma ni noma. Mkuu wa wilaya alitakiwa awe mfano mzuri kwa wananchi wake. Na pia kama alishindwa kabisa then angejitahd kujificha asimuingize ndani huyo hawara yake. Kitendo cha kulala na hawara ndani ya nyumba anayoishi na mkewe ni kitendo cha dharau sana kwa mkewe.
 
Inaonekana wife alivumilia kwa muda mrefu sasa kaamua liwalo na liwe
 
hongera mama dc maana huyo mwanaume alishindwa kwenda guest kwanza ingekuwa mm ningemkung'uta humo ndani af naitia mwizi. Well done!
 
Duh! huu waya umejaa uzushi, uwongo na upotoshaji mkubwa. Tulio wengi tunatumia jamvi hili kama mahali pa kujifunza na kupata taarifa kuhusiana na mambo yanavyokwenda ndani na nje ya Tanzania sasa inapotokea mtu akakurupuka na kuzusha jambo na tukapoteza muda kusoma haipendekezi. Kifupi ni kwamba, Mkuu wa Wilaya ya Kyela anaitwa Magreth Malenga ni mwanamama huyu na si dume. Alichukua nafasi ya Rajabu Kihato aliyehamishwa miaka kadhaa wakati JK alipofanya mabadiliko ya MADC. Kihato alichukua nafasi ya DC mmoja anaitwa Mashimba, ambaye aliachwa katika awamu ya kwanza JK alipoingia madarakani. Labda utatuambia umekosea na aliyefumaniwa ni huyo mama, lakini yeye yuko ofisini kama kawaida anaendeleza libeneke. Shame
 
Umenikumbusha hilo tukio mkuu , nilikuwa KYELA siku hiyo na ilikuwa aibu sana , NAUNGA MKONO RASIMU YA WARIOBA MA - DC NA MA - RC WAFUTILIWE MBALI , KAMA NI KUKIMBIZA MWENGE MBONA KILA MTU ANAJUA BHANA !
 
Victoire
avatar11226_6.gif

Kumbe siku moja moja unajificha hapa?
c.c First Lady
 
Duh! nina shaka sana na huu waya umejaa uzushi asilimia 100. ninavyofahamu Mkuu wa Wilaya ya Kyela ni Magreth Malenga na ni mwanamama. Huyu alichukua nafasi ya Abdalah Kihato wakati JK alipofanya mabadiliko. Kihato alichukua nafasi ya Mashimba ambaye alitemwa katika awamu ya kwanza JK aliposhika madaraka. Huyu mama mpaka sasa yupo ofisini. Mtoa waya huu tunahitaji taarifa sahihi na za uhakika vinginevyo ni za uzushi na kupotezeana muda. Ikumbukwe wengi tunatumia jamvi hili kupata taarifa za masuala mbalimbali ndani na nje ya nchi hivyo, si vyema kudanganyana kama watoto. Shame
 
Mkuu wa wilaya ya kyela nimwanamke.... Huyu Mtoa hoja ni muongo na mnafiki..... Halafu watanzania bwanaaaa yaani mijitu mingine inachangiaaaa tuu bila ata kujua Kama ni habari sahihi... Shame on you all negative mind people... Admin JF onesha umakini futaa ujinga huu na uzushi wa Mtoa mada
 
Ama kweli watanzania ni wavivu wa kusoma na kufanya utafiti kwa lengo la kupata ukweli halisi wa mambo ndio maana tunadanganywa kila kukicha na kuendeshwa kama mapoyoyo. shame
 
Back
Top Bottom