Kuhani
JF-Expert Member
- Apr 2, 2008
- 2,944
- 64
Wakuu naomba kuuliza hivi kuwa DC wa Wilaya ni lazima uwe member wa CCM au? Eti hata ishu za uzinzi nazo ni za vyama pia?
Na hii habari hivi ni kweli ina ukweli? Kweli kuna kiongozi wa Tanzania amekuwa releived power kwa sababu ya hawara? Mbona wengine wamesafiri nao huko NY?
Naomba mwenye ukweli anihakikishie kwua hii habari ni ya kweli.
Ndio maana huwa nasema hatuwezi tukajikita katika mijadala iliyo based on mtu kusikia sikia!
Umewahi kuona wapi Sheria ina enforce maadili ya kuto chiti kwenye ndoa ?
Na hata kama ingekuwepo, kuna kitu katika Katiba ya Tanzania kinaitwa "equal protection" au "legal process," au sehemu nyingine duniani wanakiita "due process" of law. Kabla ya kuchukuliwa hatua kama hizo ilibidi huyu mfumaniwa Uzinzi nae asikilizwe (kitu ambacho Lowassa alilia Mwakyembe hakumfanyia, ) na awe na haki ya rufaa, na ifuatwe misingi anuwai ya ushahidi. Sio mke kakuta "mwizi" kimada halafu Mkuu wa wilaya akafukuzwa kazi baada ya hapo.
Haki ya Usawa mbele ya Sheria:
Sehemu ya 3, Ibara ya 13, Kipengele 6 (a)
Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia misingi kwamba:
wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kingenecho kinachohusika;