Mkuu wa Wilaya ya Kyela asimamishwa kazi baada ya kufumaniwa na mkewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa Wilaya ya Kyela asimamishwa kazi baada ya kufumaniwa na mkewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkulima, Sep 28, 2008.

 1. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Kumbe baadhi ya sheria za maadili zinafanya kazi Tanzania.

  Mkuu wa wilaya ya Kyela kasimamishwa kazi baada ya kufumaniwa na mkewe akiwa na mwanamke mwingine. Inasemekana huyu mkewe anasoma Dar. Alipata habari na kuamua kutinga Kyela kimya kimya. Alipofika na kukuta huyo mwanamke ndani, akapiga kelele za mwizi na kusababaisha vurugu kubwa.

  Kwasasa mkuu wa wilaya ya Ileje ndiye kapelekwa Kyela, sijui kama ni kwa muda au la.

  Nasikia kachukuliwa hatua kwa kukiuka sheria za maadili kwa viongozi.
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkulima

  CCM wanaitwa madume wa mbegu na mabingwa wa nyumba ndogo kibao .Kama kasimamishwa ni mchezo kama ule wa EPA maana nani anaweza kusimamia maadili ndania ya serikali hii ya Mzee ?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,447
  Likes Received: 7,187
  Trophy Points: 280
  Huyo mke nae mjinga angeyamaliza na mme wake au kifamilia tu!sasa kumchafua mme wake ndo nini?kina magufuli hadi wana vimada na mke anajua na anaishi na mtoto wa kimada wa magufuli!
  Sijafurahia kitendo cha mke wa huyu mkuu wa wilaya!mimi siwezi muabisha namna hii mme wangu!wangeyamaliza kibusara tu!
   
 4. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145

  Siku za mwisho kila baya litafichuliwa japo dogo namna gani. Hata wewe usijali na kukumbatia maovu usije ishi kwa majuto.

  Sali kabla hujasaliwa.
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Very well said .Nimekubali maneno yako mkuu .Kisa nini madaraka ?No way je magonjwa vipi ?Nayo watayaficha yakisha wakamata ?
   
 6. M

  Mtu Kwao JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2008
  Joined: Jan 15, 2008
  Messages: 258
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mmmh sijui wewe kama ni mwanamke au mwanaume.lakini nataka kusema kwamba,inawezekana huyu mama alishaongea sana ila jamaa hasikii.mwache aumbuke wamezidi hawa.
   
 7. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Hasira hasara!
   
 8. D

  Dotori JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nani analiyemwaibisha mwenziwe?
   
 9. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60

  Nafikiri kwenye hili wote ni losers. Huyo mwanamke naye alijua kabisa kwamba huyo ni nyumba ndogo ya mumewe, sasa kwanini apige kelele za mwizi?

  Je watu wangeingia na kumuua huyo dada si ingelikuwa balaa kubwa kwa wahusika wote?

  Yeye angemwandama mumewe na kama mambo yameshindikana basi akaomba talaka.
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Huyo Mama ni janja yake tu...Sasa ina maana kuwa alirudi kutoka Dar kuja kufumfumania mwizi aliyeletwa na mume wake kuja kuiba mali zao?

  Kiutaratibu alitakiwa kumwuliza mumewe ni kwanini kaleta mwizi ndani ya nyumba na si kupiga kelele...Na kama asipodai talaka basi huko Dar kasukwa kwa minajili ya kisiasa..Sasa ni ethier aombe talaka ama afunguwe mashitaka ya uwizi wa mwanamke huyo kwa kushirikiana na mumewe..Otherwise ni mambo ya siasa tu yanaingizwa ndani ya familia...Kweli siasa ni ulaji...
  .
  Tumshaona mambo ya wake kushiriki kwenye mambo ya siasa na kujikuta wakiingia kwenye mitego ambayo sometimes ni mauti kwa waume zao ama wao wenyewe.

  Sasa kama mwanasiasa mpinzani anaweza kuingilia familia...Tusije kushangaa ugomvi wa kisiasa ukahamishiwa na kuendelezwa ndani ya familia na uadui kuongezeka...Kwa mfano kitendo cha Deus Mallya kufagiliwa na mke/mpenzi huyu ama ndugu huyu na kupingwa na mke/mpenzi ama ndugu yule...Tatizo lilitokea hapo mtu anazikwa tu na mambo yanaendelea kuona kuwa ni nani atakayeibuka baada ya ndugu huyo either kufa kimwili ama kisiasa ama vyote vyote yani kimwili na kisiasa.

  Ni bora kisiasa kwani inawezekana kuwa ulikuwepo upande mbaya wa siasa lakini nia yako ni nzuri..Kifo cha kimwili legacy yako sasa ndiyo hiyo...Huyo mkuu wa wilaya ndiyo hivyo tena.....Tunakoelekea huko hatahamishiwa wilaya nyingine tena..Bali kisiasa ndio hivyo tena.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,550
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Maadili ya viongozi yawe yanawabana wote wakiwemo viongozi wa juu kabisa ambao ni mafisadi, wanaosaini mikataba mibovu isiyo na maslahi kwa Watanzania na siyo viongozi wa ngazi za chini wanaofanya ngono.
   
 12. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2008
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sikujua kama Tanzania kuna sheria kama hizo....basi viongozi wote CCM na Serikali nzima wakamatwe....pamoja na makampuni yote makubwa......na waajiri (temp agencies)....etc.
   
 13. M

  Mwakaleli Member

  #13
  Sep 28, 2008
  Joined: Sep 23, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nona jinsi kila mtu anavyoijadili hii maada, mwanaume amefanya kosa la kufanya part time. Watu tunaona mkewe kakosea kwa sababu wanaume wanaona wana haki ya kuanya kazi za nje. Jamaa kaharibu, na amejiabisha wala si mkewe aliyemwaibisha. Na Kyela inavyotisha kwa ngoma lakini watu bado hawaachi kazi za nje. Tutakufa kama kuku . sasa huyo mkuu wa wilaya alikuwa anawaeleza nini kyela kuhusu ngono uzembe. tutamalizika sote namna hii.
   
 14. M

  Malila JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Waachani wafu wazikane wenyewe.
   
 15. H

  Humble Servant Member

  #15
  Sep 28, 2008
  Joined: Aug 2, 2007
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  boss lunyungu,
  kengeza lako limezidi CCM hapo inaingiaje? wanaofumaniwa wote ni CCM?Mbona Slaa nae alisha wahi kuripotiwa kuwa amefumaniwa?je na yeye atakuwa ni dume wa mbegu na mabingwa wa nyumba ndogo! Maswala haya ya mahusiono yaache tu kama yalivyo WANAUME WENGI tunaumwa ugonjwa huo sasa wewe usijifanye mtakatifu maana hata mapadre walio kula viapo na kushinda madhabauni wanaanguka.

  Tuache ushabiki wa VYAMA vinginevyo tutakuwa na hoja zenyemakengeza muda wote!
   
 16. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Lunyungu,

  Huko unakozunguka na wanasiasa huku umeacha familia yako nyumbani, angalia, next time tutakuwa tunaongelewa kufumaniwa kwako.

  Ngono haina chama, mbona hata huyo mheshimiwa wenu kazi kuvinjari na wabunge wa kuteuliwa? Kwi kwi kwi!!!
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Wakuu naomba kuuliza hivi kuwa DC wa Wilaya ni lazima uwe member wa CCM au? Eti hata ishu za uzinzi nazo ni za vyama pia?

  Na hii habari hivi ni kweli ina ukweli? Kweli kuna kiongozi wa Tanzania amekuwa relieved from power kwa sababu ya hawara? Mbona wengine wamesafiri nao huko NY?

  Naomba mwenye ukweli anihakikishie kua hii habari ni ya kweli.
   
 18. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu FMES,

  Hii habari ina ukweli. Hata mimi nimeshutuka maana sikuwahi kusikia kitu kama hicho.

  Inaelekea sababu sio kuwa na hawara bali zogo lililotokea na kumfanya DC adharauliwe na wananchi anaotakiwa kuwaongoza.

  Hivi jamaa akisema wote ni wake zake, watamfanya nini?
   
 19. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Source ya hii taarifa iko wapi?
   
 20. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  tunaisubiri sana mkuu!
   
Loading...