Mkuu wa Wilaya ya Hai, aamuru shamba la Freeman Mbowe la Mbogamboga liharibiwe, Mbowe alaani!

Mbowe Ndio Firewall ya Chadema, Hanunuliki, Ndio Maana Wanajaribu kila Jinsi Kumvuruga. The Guy is the best Politician ever to practice in Tanzania with exception to Mwalimu Nyerere! Mbowe ni Mwanasiasa na Kiongozi Bora na Imara Mara 100% Kuliko Magufuli na Magufuli hilo analijua sana!

Safi sana, kama alivunja sharia inabidi ashughulikiwe tu. Huyu mtu alikuwa alipi kodi ya mjengo wake na kshfa kibao....ashughulikiwe haraka sana.
 
Mbowe kakwambia hilo shamba lake liko ndani ya chanzo cha maji!!?
Au hajakwambia aliahidi kuacha kulima mwezi wa 5 ili angalau asipate hasara kwenye gharama alizotumia tena aliomba aruhusiwe kwa sababu alikuwa tayari amesha otesha!!?
Au hujui wananchi waligoma kutoka kwenye vyanzo vya maji kisa Shamba la Mboe?
Kahurumiwa asipate hasara!,mkuu wa wilaya kakubali lawama za wananchi kisa mbowe kwa miezi minne,cha ajabu hujui badala ya Mbowe kulipa wema kwa mkuu wa wilaya yeye kapanua shamba tena baada ya mda alioahidi anusuriwe kupata hasara.
Bado Mbowe hasemi hayo yote!!
Tusiwe tunashabikia tu bila kuhoji sababu
Ni kweli shamba limeharibiwa vibaya mno ila Mbowe ndo kaonesha shukrani ya punda

Umemsikia Mbowe mwenyewe au umemsikia KADA wa CCM akiongea??Kama lilikuwa kwenye chanzo cha maji kwanini isiwe NEMC iwe Mkuu wa wilaya?
 
CCM mmeanza kuchanganyikiwa sasa.mnapambana na mboga. Mboga zina makosa gani,?
 
Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Hai ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Gellasius Byakanwa wamevamia shamba la mbunge wa jimbo hilo, Mh. Freeman Mbowe lililoko nyumbani kwake Machame na kuharibu miundo mbinu na mali pamoja na mboga mboga na mimea.

Mh. Mbowe amezungumza na [HASHTAG]#Jahazi[/HASHTAG] moja kwa moja kutoka bungeni mjini Dodoma... "Ni kweli nimezipata hizi habari mkuu wetu wa wilaya akiambatana na askari na waandishi wa habari walikwenda kwenye mradi wetu na kukatakata mimea na kufanya uharibifu mkubwa, taarifa nilizozipata kutoka kwa wafanyakazi waliopo site walisema walipokea barua kutoka NEMC kuwa kilimo tunachokifanya kinaharibu mazingira na hatukustahili kuendelea na kilimo kile, ni jambo la kufedhesha sana tunawahamasisha watanzania wawekeze kwenye kilimo cha kisasa lakini viongozi wa serikali bila kuheshimiana wanakwenda kuharibu, sio kweli kilimo chetu hakiharibu mazingira, familia yetu imelima kwenye shamba hilo kwa zaidi ya miaka 80"

Kwa vile wao wana miloni kumi za kununulia mboga,'basi wameona waharibie wale wengine,,
 
Umemsikia Mbowe mwenyewe au umemsikia KADA wa CCM akiongea??Kama lilikuwa kwenye chanzo cha maji kwanini isiwe NEMC iwe Mkuu wa wilaya?
Kwani kilimo huwa kinafanyika katika mazingira Yepi? " kwenye vyanzo vya maji ndio kilimo kinapo hitajika, sidhani kama kina athiri zaidi ni kuongeza vyanzo vya maji, miti na mimea huleta mvua kutoka juu na chini.. Jangwa sio sehemu ya kilimo
 
Ttaizo kubwa ni kukosa ELIMU ya green house/netting house,kwamba kilimo hiki hakiathiri Mazingira na ndicho wenzetu Israel na Uarabuni wanakitumia.
 
Kama ameonewa kwa nini asifungue kesi ya jinai dhidi ya hao waliomharibia shamba lake ili alipwe fidia? Haya mambo mengine siyo ya kugeuza kuwa ya kisiasa. Uhalifu ni uhalifu tu hata kama unafanya na mwanasiasa.
 
napenda kuandika histria kwa ufupi mnooo naona mwana sias mwenyw busara ni freeman mboe moja
Alinyanganywa shamba hakusema chochote
Alifutiwa ati miliki ya hotel napo alipiga moyo kondo
Amenyanganywa gari na bunge hajasema chocht
Hiyo ndiyo busara naamin hakuna mwananchi anae mchukis
 
Kwa uandishi huu Ngumbaru ana afadhali
 
napenda kuandika histria kwa ufupi mnooo naona mwana sias mwenyw busara ni freeman mboe moja
Alinyanganywa shamba hakusema chochote
Alifutiwa ati miliki ya hotel napo alipiga moyo kondo
Amenyanganywa gari na bunge hajasema chocht
Hiyo ndiyo busara naamin hakuna mwananchi anae mchukis
Bora awe na hekima hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom