Mkuu wa Wilaya ya Hai, aamuru shamba la Freeman Mbowe la Mbogamboga liharibiwe, Mbowe alaani!

Huyu DC aulizie historia ya Hawa Nguluma kule Mbarali! Aliwatesa wafugaji wa kisukuma kwa ile operation ya mwaka 2007/2008? kwa kuondoa mifugo yao kwa lazima, huku mtoto wake akitumia muda huo kununua mifugo kwa bei za kutupa kutoka kwa wafugaji ambao hawakutaka kuona mifugo yao ikifa njiani kuelekea Lindi. Huyu mama alikuja kufa kimaskini, hadi aliomba msaada (kupitia ITV) wa kwenda kutibiwa India.
 
Mimi ni CCM damu damu , lakini kwa hili Mkuu wa Wilaya na kamati yake wamekosea sana, tena sana.
Hiyo akili ya kubomoa miundo mbinu ya shamba sijui wameipata wapi.
Na kwa hakika lazima ucunguzi ufanyike ii tuelewe wote the thinking behind kubomoa miundo mbinu ya mashamba.
 
Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Hai ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Gellasius Byakanwa wamevamia shamba la mbunge wa jimbo hilo, Mh. Freeman Mbowe lililoko nyumbani kwake Machame na kuharibu miundo mbinu na mali pamoja na mboga mboga na mimea.

Mh. Mbowe amezungumza na [HASHTAG]#Jahazi[/HASHTAG] moja kwa moja kutoka bungeni mjini Dodoma... "Ni kweli nimezipata hizi habari mkuu wetu wa wilaya akiambatana na askari na waandishi wa habari walikwenda kwenye mradi wetu na kukatakata mimea na kufanya uharibifu mkubwa, taarifa nilizozipata kutoka kwa wafanyakazi waliopo site walisema walipokea barua kutoka NEMC kuwa kilimo tunachokifanya kinaharibu mazingira na hatukustahili kuendelea na kilimo kile, ni jambo la kufedhesha sana tunawahamasisha watanzania wawekeze kwenye kilimo cha kisasa lakini viongozi wa serikali bila kuheshimiana wanakwenda kuharibu, sio kweli kilimo chetu hakiharibu mazingira, familia yetu imelima kwenye shamba hilo kwa zaidi ya miaka 80"






Hapa kuna mawili au matatu. La kwanza, hakuna jamii yoyote ambsyo KWEEELI itakubali kuona chakula shambani kikiteketezwa.

La pili, kwa Uchaggani, Mangi kihistoria alikuwa na haki zote kwa raia zake - mifugo, mashamba, hata wake zao angeweza kuchukua kadiri atakavyotaka. Maana yake ni kwamba Mbowe hana cha kulalamika kwa sababu Mangi si lazima awe CCM.

Hayo ni mawili, yote primitive, yalishapitwa na wakati. La tatu ndiyo muhimu zaidi: TII SHERIA BILA SHURTI.

Bill Marconi.
 
Kwa hiyo amemuibia nani hapo?Akili yako iko kama Panya,badala ya hasira zako kuzupeleka kwa akina JK na BM unaImalizia kwa MTU ambaye hajakuibia ni juhudi zake mwenyewe na familia yake.

Sasa baada ya huo uharibifu wewe ndugu yangu umefaidika na nini??

Roho mbaya haizijengi ndiyo sababu mnakufa masikini.
Kama ni kweli,basi hii ni zaidi ufedhuli.halafu mnataka kuwatesa watu wa Mungu kufuna na kuombea serikali hii!!!!!sio mimi!!!!!!!!!!
 
Mbona NEMC wakienda kwenye Viwanda vinavyofanya uharibifu hua wanasimamisha Uzalishaji naKuamuru kiwanda kilipe faini! Iweje huko Hai ni mkuu wa wilaya ndo afanye kax ya kuharibu na c NEMC?
 
Hii sasa ni aibu na laana kuharibu mazao wakati huu wa tatizo chakula. Miaka 19 makampuni yanachimba madini kinyume hamhavamia leo mtanzania mwenzenu kalima mnaenda kuharibu mazao. Hivi hata kama alikosea kwanini busara haikumika kusubiri mpaka avune? Huyo DC ana akili timamu kweli??!!
Ni roho mbaya tu na chuki
 
Laana za matendo haya ndio zitamfanya bwana fulani alanike na asifanikiwe kwa kila jambo analofanya au analopanga kulifanya.
 
Vyanzo vyanzo vyanzo vya maji hupaswi kufanya shughuli yoyote ya Kilimo ndani ya mita 60 sasa yeye kama kisa mpinzani basi asilete ujanja ujanja katika hilo wakati kosa analijua na akategemea kufanya hivyo kuna wenye akili timamu watamsaidia hapana labda machizi wenzake ndo watamtetea
Umeenda kupima ukakuta ni chanzi cha maji? Chanzo cha maji ni mlima Kilimanjaro
 
walihubiri sana kwenye kampeni kuwa hawataki watu wenye siasa za chuki wakimpoint lowasa, sasa nani mwenye chuki kati la lowasa na magu
 
Back
Top Bottom