Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,411
Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Hai ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Gellasius Byakanwa wamevamia shamba la mbunge wa jimbo hilo, Mh. Freeman Mbowe lililoko nyumbani kwake Machame na kuharibu miundo mbinu na mali pamoja na mboga mboga na mimea.
Mh. Mbowe amezungumza na [HASHTAG]#Jahazi[/HASHTAG] moja kwa moja kutoka bungeni mjini Dodoma... "Ni kweli nimezipata hizi habari mkuu wetu wa wilaya akiambatana na askari na waandishi wa habari walikwenda kwenye mradi wetu na kukatakata mimea na kufanya uharibifu mkubwa, taarifa nilizozipata kutoka kwa wafanyakazi waliopo site walisema walipokea barua kutoka NEMC kuwa kilimo tunachokifanya kinaharibu mazingira na hatukustahili kuendelea na kilimo kile, ni jambo la kufedhesha sana tunawahamasisha watanzania wawekeze kwenye kilimo cha kisasa lakini viongozi wa serikali bila kuheshimiana wanakwenda kuharibu, sio kweli kilimo chetu hakiharibu mazingira, familia yetu imelima kwenye shamba hilo kwa zaidi ya miaka 80"
Zaidi, soma:
Mahakama Moshi yaruhusu kilimo kuendelea kwenye shamba la Mbowe

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Freeman Mbowe ametoa kauli nzito baada ya mkuu wa wilaya ya Hai kuamuru shamba lake liharibiwe vibaya lenye thamani kubwa ya mamilioni ya shilingi.
Shamba hilo limeharibiwa kutokana na Mhe Mbowe kuongoza chama kikuu cha upinzani nchini na kuwa na msimamo thabiti usiyoyumba wa kukataa kuwa kibaraka wa CCM.
Mara baada ya shamba hilo kuharibiwa vibaya Mhe Mbowe bila kuterereka ametoa kauli ifuatayo:
"...Haya yanafanywa kwasababu ya misimamo yangu ya kisiasa ,Muelekeo wangu wa kisiasa ,uthabiti na uimara wa chama ninachokiongoza. Sasa Mimi Siwezi kuwa kondoo nimesema siku zote, haya mambo ya Duniani anayelipa ni Mungu si mtawala yoyote yule wala hawatanibadilisha misimamo yangu kwa kuharibu Mali Zangu, wanaweza kuharibu Mali Zangu zote, hata wakitaka roho yangu waichukue tu.
Lakini haitabadilisha Msimamo wangu ninaouamini katika kupigania Taifa na hakuna uwingi wa mali watakazoziharibu zitakazonifanya nikapige magoti kama wengine wanavyopiga magoti;Sita piga Magoti nitasimama katika kweli na haki wakati wote wa Maisha yangu , Jambo hili halinishangazi kwasababu najua gharama ninazozilipa..."
Zaidi, soma:
Mahakama Moshi yaruhusu kilimo kuendelea kwenye shamba la Mbowe