Mkuu wa wilaya ya Chamwino msaidie Rais miradi ya ujenzi ya shule wilaya ya Chamwino

Kufa c mwiko

JF-Expert Member
May 26, 2013
732
292
Nianze kwa kumpongeza mama Samia kwa kuona mbali lakini aliona umuhimu wa kuipa kipaumbele elimu na afya hizo ndizo nguzo muhimu kwa ustawi wa maisha ya mwanadamu yeyote chini ya jua, lakini pia kimtazamo Rais angependa kuona kile alichokipanga kwa wananchi wake kinatimia na kuonekana machoni kwake lakini imejitokeza swala moja kubwa kwasababu kuna vitengo kwenye hii halmashauri ni walafi SUGU wao kama mbwai na iwe mbwai kitengo cha manunuzi chenyewe ndiyo kinafanya kazi za kamati zote za ujenzi iwe kata kijiji nk ya vijiji na kata zote halmashauri hii.

Hivi umeshawahi kujiuliza kulikuwa na umuhimu gani wa vifaa vya miradi ya ujenzi za shule zoote vinunuliwe na kurundikwa ofisi ya halmashauri yaani watu watoke km 100,80,50 nk kufata vifaa wakati huko waliko kuna maduka,kwahiyo wanachoangalia hao watu warafi wa manunuzi ni zile 10% wanazopata huko kwa wazabuni kuliko kuangalia miradi inaisha kwa wakati watoto wanaingia darasani kwa wakati miradi mingi imeshindwa kuisha kwa kwa wakati chanzo ni huo urafi tu wa watu wachache ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom