Mkuu wa Wilaya Arusha na mbwembwe za misafara

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,919
31,161
Heshima sana wanajamvi,

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini ni kijana mdogo lakini mwenye mbwembwe nyingi na vituko vya ujana uliopitiliza. Katika siku za karibuni amekuwa na tabia ya kusindikizwa na gari la Polisi ikiambatana na ving'ora vingi pengine ungefikiri kuna mgonjwa wa COVID 19 anakimbizwa Hospitali kuwahi huduma za kitabibu.

Mwezi uliopita kama kumbukumbu zangu zipo sana alizindua mradi mdogo {mradi uchwara} wa kufyatua matofali wa halmashauri ya Jiji la Arusha. Huo msafari ungefikiri anakwenda kuzindia kinu cha Nyuklia gari zilikuwa zinakimbizwa,ving'ora na taa za magari yote zikiwashwa full light.

Tutakae tukubali Vijana wakipewa madaraka kidogo wanaharibu sana, wanaumiza wananchi sana, wanatumia madaraka vibaya sana bahati mbaya Mkuu wa Wilaya ya Arusha anaingia katika kundi hilo.

Mwaka jana alishiriki zoezi la kuwachapa viboko wafanyabiashara kwa madai ya kununua thamani za shule. DC kawa mpelelezi, akajivika ujaji na mwisho wa siku akamalizia kudhalilisha wananchi pasipo uchunguzi wa haki.
 
Kwakweli huyu mkuu wa wilaya ya Arusha simjui vizuri ila ni mtu poa sana.

Nakumbuka mwishoni mwa mwaka jana alitusaidia kupata mafao yetu NSSF baada ya kusumbuliwa karibia mwaka mzima.

Nnachokumbuka tulimfata siku moja tuna akatuambia turudi baada ya siku 3, na tulivyorudi aliondoka na sisi hadi kwenye ofisi za NSSF pale Arusha na akaingia na sisi hadi ndani, akakagua computer za pale kwa sababu tulimweleza namna tunavyopigwa danadana muda mrefu bila majibu ya kueleweka.

Meneja alijitahidi kujitetea kwa uongo mwingi lakini kupitia mkuu huyu wa wilaya tulipata mafao yetu bila kuchelewa.

Kumbuka tulikua wengi hivyo alitusaidia sana.

Namkubali sana maana amesaidia watu wengi kuanzia waliodhulumiwa maeneo yao, migogoro ya kifamilia na mengine mengi... Kwakweli nilimkubali hadi nikawa nahudhuria kwenye ziara zake za kusikiliza kero za wananchi.

Yule aliyekuwepo kabla yake tulimfata akatufukuza na maneno mbovumbovu bahati nzuri hakumaliza mwezi akaondolewa ndio akaletwa aliyepo sasa.
 
Hahah, umeamua kumsagia kunguni kwa Mama kabla mkeka haujatoka?
Unafikiri mama hamjui huyu dogo wa kucharaza viboko watu? Anamjua sana, na wengine mafaili yao yapo wazi kwake, shida tu mama anawastahi na kuwapa second chance watu wa Mwendazake. Sina uhakika kama Ali Happi atatoboa kwenye huu utawala
 
Majungu si MTAJI useme utafanikiwa.......

Baadhi ya watu wa ARUSHA NA KILIMANJARO hawawapendi MADC NA MARC wenye misimamo dhidi ya "MADILI YAO"...

Yaani kusikia tu mh.Rais anaandaa "MKEKA WA MADC" basi watu wanajiandaa kuwachafua WENGINE(TARNISHING OF IMAGE)....



#KaziIendelee
 
Back
Top Bottom