Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Chalamila astuka , Atengua zuio la kufunga Bar kuzuia Corona

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ametengua agizo la kufunga baa saa 3:00 usiku alilolitoa Aprili 17, 2020. Amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya wamiliki wa baa kuweka mikakati ya kudhibiti virusi vya corona (kuweka vitakasa mikono, kuzingatia umbali) kwenye maeneo yao.

Na nyie Watawala Siku zingine muwe mnatuliza Kwanza Akili zenu hasa pale mnapowateua Wasaidizi wenu hawa Tanzania hii.
Ulipenda nini kitokee??
 
Lazima kuna sentence ilisomeka "pumbavu wewe kwahuo ufala uliofanya kodi tutazipataje?"

Na hilo neno Pumbavu ( Popoma ) huwa analipenda sana na Mawaziri akina Mpango na Kabudi ' wameshatukanwa ' nalo mno kama ambavyo Mwenyewe alisema Siku Moja kulipokuwa na Hafla ya Uapisho kwa Wateule wake pale Jumba Jeupe Magogoni.
 
View attachment 1422530

Hapo Jana Mh Chalamila aliweka utaratibu wa wanywaji wa Mbeya , kwa kutoa muda wa hadi saa 3 usiku wawe wamepukutika kwenye mabar , kwa hoja kwamba baada ya muda huo wengi wanakuwa wamelewa kiasi cha kukiuka kinachoitwa Social Distancing ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona .

Lakini katika hali ya kushangaza leo hii amefuta amri hiyo , na kwamba wanywaji waendelee kupiga kilaji mpaka watakapotosheka , ili mradi wachukue tahadhari .

#Tuendelee kunawa mikono kwa maji Tiririka ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona
Asante kwa taarifa hii.
P
 
Back
Top Bottom