JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,315
- 5,478
Nimesoma kupitia mitandao ya kijamii kuhusu mjadala wa kukamilika kwa kituo cha Polisi Butiama kwa thamani ya sh mil 802.
Kwanza nawapongeza waandishi kwa kuibua hoja na mjadala, ingawa hoja na mjadala haukusikia wala kutaka kufahamu kutoka upande wa serikali.
Kwa kuwa serikali yetu ni serikali inayotoa uhuru kwa wanahabari na vyombo vya habari tumeitikia wito wenu wana habari,
Leo nimetembelea mradi uliotajwa hapo juu na kupokea taarifa na kukagua kituo hicho,
Hadi sasa serikali imetoa fedha kwa acc ya RPC Mara sh mil 500.
Matumizi ya sh mil 500 iliyotolewa ni kama ifuatavyo.
2. Hadi sasa sh mil 91 bado haijatumika katika mradi, mil 48 imeombwa hazina kwa matumizi haya
A. Mil 16.4 malipo ya Local fundi.
B. Retention mil 2.1
C. Diesel ya mradi mil 3.4
D. Supplier Al Nadabi mil 12.6
E. Umeme Tanesco mil 14.
Malipo haya yameithinishwa lakini hayajalipwa bado.
Aidha kwenye Acc ya mradi fedha sh mil 42.453.460.18 hazijatumika kwa sababu kazi bado inaendelea.
Kwa msingi huo fedha takriban mil 366 zimetumika hadi hapo mradi ulipofikia.
TASWIRA YA MRADI
Nimejionea ukubwa wa jengo takriban sm 737 nimepima kwa kushirikiana na wahandisi. Bado nalifanyia kazi zaid kitaalam zaid.
Jengo lina ofisi za OCD, OCCID, DTO na OCS, lina mahabusu ya watoto chini ya miaka 18, mbili, kwa wanaume na wanawake. Ina mahabusu ya walemavu na mahabusu ya wakina baba na wakina mama. Jumla mahabusu 6 zenye uwezo wa kuchukua watu kati ya 50 na 60. Vyumba 31 na vyoo 15.
HATUA TUNAYOCHUKUA KAMA SERIKALI
1. Kupitia mkaguzi wetu wa ndani RS tutakagua takwimu na kiasi cha fedha kilichotumika yaani mil 366 kama kinalingana na thamani ya fedha.
2. Tutaishauri serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani mradi huu unaweza kuisha chini ya thamani hiyo iliyotajwa.
Mwisho, eneo linahitaji uzio na canteen, endapo fedha iliyopitishwa kwenye bajeti itatolewa tuombe kibali cha kutekeleza sehemu ya pili ya mradi.
Said Mtanda
RC Mara.
19 Nov 2023
Pia soma: Kituo cha Polisi Wilaya ya Butiama chajengwa kwa Tsh. Milioni 802, kukamilika Desemba 2023
Kamati kuchunguza Kituo cha Polisi kinachojengwa kwa Tsh. Milioni 802
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani imeunda kamati maalum kuchunguza ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Butiama mkoani Mara unaokadiriwa kutumia Sh802 milioni hadi kukamilika kwake. Kamati hiyo inaundwa na wataalam wa masuala ya manunuzi, ukadiriaji wa majengo, wahandisi ujenzi na...
www.jamiiforums.com