Kamati kuchunguza Kituo cha Polisi kinachojengwa kwa Tsh. Milioni 802

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani imeunda kamati maalum kuchunguza ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Butiama mkoani Mara unaokadiriwa kutumia Sh802 milioni hadi kukamilika kwake. Kamati hiyo inaundwa na wataalam wa masuala ya manunuzi, ukadiriaji wa majengo, wahandisi ujenzi na wakaguzi wa fedha kutoka idara na taasisi mbalimba za umma.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo Jumatatu Novemba 27, 2023, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Jumanne Sagini amesema uamuzi wa kuunda kamati hiyo inayojumuisha wataalam kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa ndani umetokana mapokeo ya wananchi juu ya gharama za ujenzi wa kituo hicho kuonekana kubwa kulinganisha na majengo yanayojengwa.

Amesema pamoja na kujiridhisha na matumizi sahihi ya fedha za umma, taarifa ya uchunguzi huo pia itaiwezesha Serikali kufanya maamuzi ikiwemo kuchukua hatua stahiki za kisheria na kinidhamu iwapo patabainika ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za ujenzi na matumizi ya fedha za umma.

Uchunguzi huo umetokana na kelele zilizopigwa na umma baada ya taarifa za gharama za ujenzi wa kituo hicho kusambaa kupita mitandao ya kijamii.

Pia soma

 
Back
Top Bottom