Maswali yaliyopaswa kuulizwa ni :
1. Je hiyo sehemu alipokuwa anajenga huyu Mheshimiwa imetengwa kwa ajili ya makazi?
2. Kama sehemu haikutengwa kwa ajili ya makazi, alipataje kibali cha ujenzi?
3. Na je hicho kibali alichokuwa nacho ni kwa eneo ambalo alikuwa anajenga?
4. Je alipata kibali cha kuendelea kujenga baada ya msingi wa nyumba kukaguliwa?
5. Je Halmashauri husika iliwahi kumtaka anayejenga hiyo nyumba kusita kujenga kwa maandishi? na kwa kuweka alama kwenye nyumba kumtaka asiendelee na ujenzi?
6.Je kuna maelekezo yeyote ya maandishi ya kuwaagiza wale mgambo kwenda kubomoa ile nyumba?
Kwa kumtia ndani huyu mama kwa kosa la kubomoa nyumba iliyokuwa inajengwa kwenye eneo lilizouiwa kujengwa kuna maana kuwa zuio hilo limeondolewa na watu waote ruksa kuendelea jenga katika eneo hilo. Hivi Mkuu wa Mkoa ana mamlaka ya kuondoa zuio hilo?
Kama nilisikia vizuri, mlalamikaji alikuwa anamtumhumu huyu mama kwa kumzuia kulala kwenye eneo ambalo anafanyia biashara. Ninavyojua mimi, hairuhusiwi kubadilisha eneo la biashara kuwa la makazi au makazi/biashara bila kupeleka maombi kwenye mamlaka husika. Kutumia sehemu ya biashara kunaweza kusababisha majanga kama moto ( kutokana na vibatali, sigara, au jiko la kupikia chakula) n.k.
Mwisho ni je hili shauri lisingeweza kushughulikiwa bila kumtia ndani yule mama? Yule mama angevuruga vipi hili shauri kwa kuwa nje?
Mimi nahisi mlalamikaji ndie aliyekuwa anawaambia watendaji kuwa hawawezi kumfanya kitu kutokana na nafasi yake ya kisiasa. Mheshimiwa alitakiwa atumie busara katika kutatua hili shauri ili kuepuka kuonekana amefanya maamuzi ya kisiasa kwenye masuala ya kiutawala. Kwa kufanya hivyo hajakitendea haki chama chake.
Amandla.............