Waziri Mkuu amsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza na Mwekahazina wa Halmashauri

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Kigoma.jpg

Kufuatia maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) ya kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Zainab Mbunda na Mwekahazina wa Halmashauri hiyo Majid Mabanga, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed O. Mchengerwa (Mb) amemwelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI kutekeleza maelekezo ya Waziri Mkuu mara moja kwa kuwasimamisha kazi Mkurugenzi na Mwekahazina huyo kuanzia leo tarehe 21.09.2023 ili kupisha uchunguzi.

Uamuzi huo umefikiwa mkoani Kigoma mara baada ya Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa kukagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya, Jengo la Halmashauri ambayo licha ya Mkurugenzi kukiri kuwepo kwa fedha za utekelezaji wake tangu mwaka 2021 ujenzi wake bado haujakamilika pamoja na kutokukamilika kwa miradi ya Elimu ikiwemo Sekondari ya Mpeta.

Aidha Waziri Mchengerwa amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -TAMISEMI kuteua afisa atakayekaimu nafasi ya Mkurugenzi na Mwekahazina hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.

Vilevile Mhe. Mchengerwa amewataka Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao kwa kuzingatia thamani ya fedha na kuhakikisha inakamilika kwa wakati huku wakihakikisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri unafanyika kikamilifu ili kupeleka maendeleo kwa wananchi.

Pia amesisitiza kuwa hatua za nidhamu zitachukuliwa kwa Watendaji watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kusababisha ucheleweshwaji wa upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
 
uDED nayo imekuwa nafasi ya teuzi ya mh. rais kana kwamba ni nafasi ya kisiasa......wakati ni kazi ya kiutendaji ambayo utumishi wanatakiwa wa appoint senior officers ndani ya utumishi wa umma.
Kweli kabisa mkuu.
 
Sababu kubwa iliyowafanya wasimamishwe ni kwa sababu waligongana kauli. Mkurugenzi alidai pesa zipo na Mhasibu akadai pesa hazipo,. Sasa upelelezi itafanyika ili kuujua ukweli.
 
Hayo ndio yale makada yaliyoteuliwa bila hata kujua uwezo wao.Mengine yalikuwa hayajafanya kazi ya aina yoyote yakaja kuanzia ukurugenzi.
Inasikitisha Sana mkuu. Ndio wizi hauishi maana wakurugenzi wengi wametokea nje ya system ya halmashauri.
 
Daa aise huyu dada, mbona hana noma halafu ni mwenzao.Ndiyo maana kuanzia juzi halmshauri moja hivi watu wanatengeneza Barbara usku kucha aloo. Halafu mvua imefuliza, maana Kila PM akija jamaa wanampiga mvua ya hatari anashindwa kukagua miradi!
 
uDED nayo imekuwa nafasi ya teuzi ya mh. rais kana kwamba ni nafasi ya kisiasa......wakati ni kazi ya kiutendaji ambayo utumishi wanatakiwa wa appoint senior officers ndani ya utumishi wa umma.
Tukisema Katiba Mpya Katiba Mpya tunamaanisha. Bila hivyo hatutaweza kumfunga Break Rais.
 
Huyo Mkurugenzi na Mhasibu wake kesho utaziona ID zao mpya humu JF na wao wataanza kuiponda serikali😁
 
Kufuatia maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb)

Dina Mathamani aliyeteuliwa kwenda Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma

21 September 2023
Uvinza, Kigoma
Tanzania

Uvinza kwa waka moto, mheshimiwa waziri mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa awa mbogo


View: https://m.youtube.com/watch?v=osWgD5N1OuU

Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa akiongea akiwa ameongozana na mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna wa Polisi CP Thobias Andengenye, mkuu wa wilaya ya Uvinza DC Dina Dina Mathamani, mkurugenzi wa mtendaji wa halmashauri ya Uvinza Bi. Zainab Mbunda na vigogo wengine wa mkoa wa Kigoma, waziri mkuu ahoji uongozi kushidwa kuhakikisha majengo mapya ya hospitali na vifaa tiba kuanza kufanya kazi ya kutoa huduma kwa wananchi.


TOKA MAKTABA:
31 January 2023

RC ANDENGENYE AMUAPISHA MKUU WA WILAYA UVINZA​


Posted On: January 31st, 2023

1695377378853.png

HABARI PICHA: HAFLA YA KUMUAPISHA MKUU WA WILAYA YA UVINZA DINAH MATHAMANI ILIYOFANYIKA JANURI 31, 2023 KATIKA UKUMBI WA KATIBU TAWALA OFISI YA MKUU WA MKOA KIGOMA
Source : https://kigoma.go.tz/new/rc-andengenye-amuapisha-mkuu-wa-wilaya-uvinza-5
 
Back
Top Bottom